Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Awamu inaisha lini?Samia ni Rais wa sita wa JMT ila ni wa awamu ya tano
Si ni wewe mwenyewe ndie ulisema Samia anaendeleza Awamu ya 5?! Bora umegundua kosa lako!!!Kwa mujibu wa Ibara ya 40 (4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa sasa amefungua awamu ya sita. Hayo ya Z'bar sina information ya kutosha kwa sasa.
Mjadala ngumu huuKwa maelezo yako Nyerere kwa hiyo alikaa awamu 2 na nusu yaani miaka 25 maana kama ulivyosema awamu 1 ina mihula 2 yaani miaka 10, inakuaje mpaka sasa jpm alikua wa awamu ya tano?
Acha uongoMheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita na moja kwa moja anakuwa Rais wa awamu ya 6. Awamu zinahesabiwa kutokana na mabadiliko ya Rais, sio vipindi vya U Rais. Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wa awamu ya kwanza lkn yeye alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20... Waliofuata walikaa madarakani kwa vipindi vya miaka 10, kasoro Hayati Dr. John Joseph Pombe Magufuli ambaye yeye awamu yake amehudumu kwa miaka mitano na miezi michache. Huyo Mtangazaji yupo sahihi.
Upo sahihiSamia ni Rais wa sita wa JMT ila ni wa awamu ya tano
Kisheria si vile. Katiba inajua "terms" (vipindi). Term = Kipindi ni miaka 5. Inaruhusu vipindi viwili kwa kila mmoja aliyechaguliwa akichaguliwa upya. Awamu ni kitu kingine, haipo katika sheria. Ukipenda kuhesabu vipindi viwili vya rais mmoja kama "awamu" moja, ni hiari yako. Vipi kama rais harudishwi kwa kipindi chake cha pili? Amefanya nusu awamu tu? Vipi kama anachaguliwa, mara ya pili hachaguliwi, lakini anagombea mara ya tatu na kushinda?Inawezekana maneno 'awamu' na 'kipindi' yanazaliwa au ni tafsiri ya ibara ya 40 (1) na (2).
Yaani hii nchi tunakwenda tu maana si katiba wala utaratibu vyote vinachanganya kwa kweli.Leo asubuhi nememsikia mtangazaji mmoja wa East Africa Radio (kwenye kipindi cha 12:00- 04:00) akisema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya sita. Yawezekana wengi wakawa na mtazamo huo, au wengi wakafuata mtazamo huo baada ya kumsikia mtangazaji huyo. Je, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 20 Juni 2005, Rais wa sasa anamalizia awamu ya tano au anaanza awamu nyingine, yaani ya sita?
Je, awamu ya tano (phase 5) imekuwa na Marais wawili? Mmoja ameshika kipindi cha kwanza (1st term) na mwingine karibu kipindi cha pili (2nd term) kwa sababu yule wa kwanza amefariki dunia?
Ikumbukwe kuwa awamu moja ina vipindi viwili (one phase has two terms).
Je, mwanahabari huyo aliptitia katiba ya nchi kabla ya kuongelea facts?
Kwa mujibu wa ibara ya 40 (4), jibu sahihi la swali juu ya kuanza kwa awamu ya sita au la, ni kuwa Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan amefungua awamu ya sita. Hivyo ndugu mtangazaji alikuwa sahihi! Je, amebahatisha au alikuwa na uhakika?
Rejea ibara ya 37, kifungu cha 5.
Umechemka mkuu.Samia ni Rais wa sita wa JMT ila ni wa awamu ya tano
Unajua maana ya Awamu?Litakapovunjwa na kuundwa tena sasa hapo ndio tutasema serikali ya awamu ya sita...
Hapo tutakua sawa ila mpaka sasa hii ni serikali ya awamu ya tano, muendelezo wake baada ya aliyekua madarakani kufariki, ni rais wa sita ila awamunya tano bado.
Kuendelea na Baraza ni utashi wa Rais mwenyewe maana hazuiliwi popote kulivunja, anaweza kulivunja na kuumda jipya muda wowote au asilivunje akafanya mabadiliko kidogo kazi ikaendelea.Alipotoka na kuingia mwingine aliendelea na baraza la mawaziri la mwinyi au lilivunjwa?
Ujuaji mwingi alafu hujui kitu!!!Samiah Hassan Suluhu, Rais wa sita wa awamu ya tano ya JMT.
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Ninvyoelewq, awamu ni administration ya rais.Leo asubuhi nememsikia mtangazaji mmoja wa East Africa Radio (kwenye kipindi cha 12:00- 04:00) akisema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya sita...