Je, Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Tano au ya Sita kwa mujibu wa Katiba ya nchi?

Je, Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Tano au ya Sita kwa mujibu wa Katiba ya nchi?

Mkuu sio lazima awamu MOJA iwe na vipindi viwil Kama ulivyoainisha hapo juu
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 40 (4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa sasa amefungua awamu ya sita. Hayo ya Z'bar sina information ya kutosha kwa sasa.
Si ni wewe mwenyewe ndie ulisema Samia anaendeleza Awamu ya 5?! Bora umegundua kosa lako!!!
 
Kwa maelezo yako Nyerere kwa hiyo alikaa awamu 2 na nusu yaani miaka 25 maana kama ulivyosema awamu 1 ina mihula 2 yaani miaka 10, inakuaje mpaka sasa jpm alikua wa awamu ya tano?
 
Rais akifa ikibaki miaka mitatu au zaidi makamu wa rais anaanza awamu yake na muhula wake. Awamu (phase) inaendana na rais aliyepo. Samia sasa ni rais wa awamu ya 6, yaani ni rais wa 6 tangu Nyerere.

Muhula (term) ni muda anaotawala kabla ya uchaguzi mwingine. Katiba yetu inaruhusu mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja ikiwa rais atachaguliwa tena. Magufuli ni rais wa awamu ya 5 ambaye hakumaliza mihula miwili. Katawala miaka mitano na miezi minne na siku 12 tu.

Kwa Samia imebaki miaka minne na miezi zaidi ya 6 kufika 2025. Huu unakuwa muhula wake wa kwanza. Akigombea na kupita 2025 utakuwa muhula wake wa pili na wa mwisho hadi 2030.
 
Maze tumekuacha rekebisha saa hii ni swami ya sita mama ndiyo anaanza kuhesabiwa sasa, swami ya tano imesha kwa style hiyo
 
Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita na moja kwa moja anakuwa Rais wa awamu ya 6. Awamu zinahesabiwa kutokana na mabadiliko ya Rais, sio vipindi vya U Rais. Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wa awamu ya kwanza lkn yeye alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20... Waliofuata walikaa madarakani kwa vipindi vya miaka 10, kasoro Hayati Dr. John Joseph Pombe Magufuli ambaye yeye awamu yake amehudumu kwa miaka mitano na miezi michache. Huyo Mtangazaji yupo sahihi.
Acha uongo

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana maneno 'awamu' na 'kipindi' yanazaliwa au ni tafsiri ya ibara ya 40 (1) na (2).
Kisheria si vile. Katiba inajua "terms" (vipindi). Term = Kipindi ni miaka 5. Inaruhusu vipindi viwili kwa kila mmoja aliyechaguliwa akichaguliwa upya. Awamu ni kitu kingine, haipo katika sheria. Ukipenda kuhesabu vipindi viwili vya rais mmoja kama "awamu" moja, ni hiari yako. Vipi kama rais harudishwi kwa kipindi chake cha pili? Amefanya nusu awamu tu? Vipi kama anachaguliwa, mara ya pili hachaguliwi, lakini anagombea mara ya tatu na kushinda?
Haidhuru kikatiba.
 
Leo asubuhi nememsikia mtangazaji mmoja wa East Africa Radio (kwenye kipindi cha 12:00- 04:00) akisema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya sita. Yawezekana wengi wakawa na mtazamo huo, au wengi wakafuata mtazamo huo baada ya kumsikia mtangazaji huyo. Je, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 20 Juni 2005, Rais wa sasa anamalizia awamu ya tano au anaanza awamu nyingine, yaani ya sita?

Je, awamu ya tano (phase 5) imekuwa na Marais wawili? Mmoja ameshika kipindi cha kwanza (1st term) na mwingine karibu kipindi cha pili (2nd term) kwa sababu yule wa kwanza amefariki dunia?

Ikumbukwe kuwa awamu moja ina vipindi viwili (one phase has two terms).

Je, mwanahabari huyo aliptitia katiba ya nchi kabla ya kuongelea facts?

Kwa mujibu wa ibara ya 40 (4), jibu sahihi la swali juu ya kuanza kwa awamu ya sita au la, ni kuwa Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan amefungua awamu ya sita. Hivyo ndugu mtangazaji alikuwa sahihi! Je, amebahatisha au alikuwa na uhakika?

Rejea ibara ya 37, kifungu cha 5.
Yaani hii nchi tunakwenda tu maana si katiba wala utaratibu vyote vinachanganya kwa kweli.

Ebu acha nikokotoe nione kama inakuja , tukianza na awamu ya hayati Mwalimu hii itakuwa ni ya kwanza lakini si kwa hesabu ya miaka maana utaratibu wa kikomo ulianzia kwa Mwinyi. Kwa maana hiyo awamu itategemea mazingira ya upatikanaji wa rais.
Kwa nini? Kwa sababu rais anapatikana kwa sanduku la kura ama kwa makamo kurithi kiti ikihitajika kufanya hivyo.

Hapa sasa ndio tuanze mjadala iwe ni wa kikatiba, utaratibu ama vyovyote itakavyo kuwa.
Nimesoma hapa kwamba baraza la mawaziri (serikali) inahesabika pia kama awamu, kama ni sawa basi tuanze na hesabu za karibu, je mzee kikwete aliongoza awamu (serikali) ngapi kwa kuwa alivunja baraza la mawaziri (serikali).
Na kwa mfumo huo huo wa baraza la mawaziri (serikali) tunajua adi sasa hivi ni baraza lile lile la awamu ya 5.
Sasa inakuaje rais awe ni wa awamu ya 6 lakini serikali yake ni ya awamu ya 5?

Tukikubaliana kwamba mama Samia ni rais wa awamu ya 6, je muhula wake wa kwanza ni miaka mingapi kwa mujibu wa katiba/utaratibu? Na ni mawaziri gani wameapa mbele ya rais ili kuunda baraza la mawaziri (serikali) awamu ya 6?

Sasa nimalizie kwa maoni yangu binafsi:
Mama Samia ni rais wa 6 wa JMT katika awamu ya 5, kwa sababu urais wake si wa uchaguzi wala si wakuanza awamu, bali ni wa kurithi kiti kilicho achwa wazi kufuatia kifo cha rais aliyekuwa madarakani. Kama ataitisha uchaguzi mpya hapo ndio angekuwa rais wa awamu ya 6. Lakini haja hitisha uchaguzi bali anaendelea na awamu ile ile ambayo uchaguzi wake ulisha fanyika. Kwa maana hiyo amerithi kiti cha urais na awamu ambayo ilisha anzwa na mtangulizi wake kwa miaka mitano na siku 114.

Kwa mfano kama akiunda baraza jipya la mawaziri (serikali) ili awe rais wa awamu ya 6 itabidi tufute zile siku 114, yaani tubadilishe tarehe za uchaguzi mkuu ili kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano.
 
Litakapovunjwa na kuundwa tena sasa hapo ndio tutasema serikali ya awamu ya sita...
Hapo tutakua sawa ila mpaka sasa hii ni serikali ya awamu ya tano, muendelezo wake baada ya aliyekua madarakani kufariki, ni rais wa sita ila awamunya tano bado.
Unajua maana ya Awamu?
Rais wa sita anakuwaje wa awamu ya tano!!?? Hiyo ni sawa na kusema " Rais wa sita wa tano!"
Mama Samia ni Rais wa Sita (Awamu ya Sita) ma ndiyo maana atagombea awamu moja tu kama akitaka kuendelea.
 
Alipotoka na kuingia mwingine aliendelea na baraza la mawaziri la mwinyi au lilivunjwa?
Kuendelea na Baraza ni utashi wa Rais mwenyewe maana hazuiliwi popote kulivunja, anaweza kulivunja na kuumda jipya muda wowote au asilivunje akafanya mabadiliko kidogo kazi ikaendelea.
 
Leo asubuhi nememsikia mtangazaji mmoja wa East Africa Radio (kwenye kipindi cha 12:00- 04:00) akisema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya sita...
Ninvyoelewq, awamu ni administration ya rais.

Ndiyo maana rais Mwinyi ni rais wa awamu ya pili, lakini rais Nyerere alitawala kwa miaka zaidi ya 20.

Hivyo hii ni awamu ya sita.

The Hassan administration.
 
Back
Top Bottom