Je, Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Tano au ya Sita kwa mujibu wa Katiba ya nchi?

Je, Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Tano au ya Sita kwa mujibu wa Katiba ya nchi?

Hapana! Awamu inaendana na kuisha na rais anayetawala. Hata Magufuli angetawala miaka 20, yaani mihula minne, bado angeitwa rais wa awamu ya 5.

Ni kama ambavyo Nyerere alitawala zaidi ya miaka 20 na bado akabaki kuwa wa awamu ya kwanza. Samia ni rais wa 6 awamu ya 6! Ali Hassan Mwinyi alitawala Zanzibar muda mfupi sana na bado akawa rais wa 3 awamu ya 3!
Upo sahihi

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Sawa kabisa!
Ninvyoelewq, awamu ni administration ya rais.

Ndiyo maana rais Mwinyi ni rais wa awamu ya pili, lakini rais Nyerere alitawala kwa miaka zaidi ya 20.

Hivyo hii ni awamu ya sita.

The Hassan administration.
 
Hapana!
Yaani hii nchi tunakwenda tu maana si katiba wala utaratibu vyote vinachanganya kwa kweli.

Ebu acha nikokotoe nione kama inakuja , tukianza na awamu ya hayati Mwalimu hii itakuwa ni ya kwanza lakini si kwa hesabu ya miaka maana utaratibu wa kikomo ulianzia kwa Mwinyi. Kwa maana hiyo awamu itategemea mazingira ya upatikanaji wa rais.
Kwa nini? Kwa sababu rais anapatikana kwa sanduku la kura ama kwa makamo kurithi kiti ikihitajika kufanya hivyo.

Hapa sasa ndio tuanze mjadala iwe ni wa kikatiba, utaratibu ama vyovyote itakavyo kuwa.
Nimesoma hapa kwamba baraza la mawaziri (serikali) inahesabika pia kama awamu, kama ni sawa basi tuanze na hesabu za karibu, je mzee kikwete aliongoza awamu (serikali) ngapi kwa kuwa alivunja baraza la mawaziri (serikali).
Na kwa mfumo huo huo wa baraza la mawaziri (serikali) tunajua adi sasa hivi ni baraza lile lile la awamu ya 5.
Sasa inakuaje rais awe ni wa awamu ya 6 lakini serikali yake ni ya awamu ya 5?

Tukikubaliana kwamba mama Samia ni rais wa awamu ya 6, je muhula wake wa kwanza ni miaka mingapi kwa mujibu wa katiba/utaratibu? Na ni mawaziri gani wameapa mbele ya rais ili kuunda baraza la mawaziri (serikali) awamu ya 6?

Sasa nimalizie kwa maoni yangu binafsi:
Mama Samia ni rais wa 6 wa JMT katika awamu ya 5, kwa sababu urais wake si wa uchaguzi wala si wakuanza awamu, bali ni wa kurithi kiti kilicho achwa wazi kufuatia kifo cha rais aliyekuwa madarakani. Kama ataitisha uchaguzi mpya hapo ndio angekuwa rais wa awamu ya 6. Lakini haja hitisha uchaguzi bali anaendelea na awamu ile ile ambayo uchaguzi wake ulisha fanyika. Kwa maana hiyo amerithi kiti cha urais na awamu ambayo ilisha anzwa na mtangulizi wake kwa miaka mitano na siku 114.

Kwa mfano kama akiunda baraza jipya la mawaziri (serikali) ili awe rais wa awamu ya 6 itabidi tufute zile siku 114, yaani tubadilishe tarehe za uchaguzi mkuu ili kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano.
 
Umeeleza vizuri sana. Awamu huendana na rais anayefuata.
Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita na moja kwa moja anakuwa Rais wa awamu ya 6. Awamu zinahesabiwa kutokana na mabadiliko ya Rais, sio vipindi vya U Rais. Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wa awamu ya kwanza lkn yeye alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20... Waliofuata walikaa madarakani kwa vipindi vya miaka 10, kasoro Hayati Dr. John Joseph Pombe Magufuli ambaye yeye awamu yake amehudumu kwa miaka mitano na miezi michache. Huyo Mtangazaji yupo sahihi.
 
Hapana! Awamu inaendana na kuisha na rais anayetawala. Hata Magufuli angetawala miaka 20, yaani mihula minne, bado angeitwa rais wa awamu ya 5.

Ni kama ambavyo Nyerere alitawala zaidi ya miaka 20 na bado akabaki kuwa wa awamu ya kwanza. Samia ni rais wa 6 awamu ya 6! Ali Hassan Mwinyi alitawala Zanzibar muda mfupi sana na bado akawa rais wa 3 awamu ya 3!
Awamu maana yake ni awamu za uchaguzi.Rais anayeingia kwa uchaguzi ndiye anayepewa awamu.Awamu hii ni ya Magufuli isipokuwa Samia amechukulia katikati kabla Magufuli hajamaliza,Hivyo awamu inabaki ya tano ila rais ni wa sita.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Ujuaji mwingi alafu hujui kitu!!!
Kila Rais ana awamu yake, ungejua kwanza maana ya awamu usingeandika ulichoandika.
Samia ni Rais wa Sita (Awamu ya sita)
Acha upuuzi hiyo awamu ya sita uchaguzi uliitisha wewe? Unaelewa maana ya awamu?
Awamu maana yake ni awamu za uchaguzi.Rais anayeingia kwa uchaguzi ndiye anayepewa awamu.Awamu hii ni ya Magufuli isipokuwa Samia amechukulia katikati kabla Magufuli hajamaliza,Hivyo awamu inabaki ya tano ila rais ni wa sita,Uchaguzi ujao ndio utakaomuweka rais wa awamu ya sita.Usijifanye mjuaji kumbe hujui.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Leo asubuhi nememsikia mtangazaji mmoja wa East Africa Radio (kwenye kipindi cha 12:00- 04:00) akisema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya sita. Yawezekana wengi wakawa na mtazamo huo, au wengi wakafuata mtazamo huo baada ya kumsikia mtangazaji huyo. Je, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 20 Juni 2005, Rais wa sasa anamalizia awamu ya tano au anaanza awamu nyingine, yaani ya sita?

Je, awamu ya tano (phase 5) imekuwa na Marais wawili? Mmoja ameshika kipindi cha kwanza (1st term) na mwingine karibu kipindi cha pili (2nd term) kwa sababu yule wa kwanza amefariki dunia?

Ikumbukwe kuwa awamu moja ina vipindi viwili (one phase has two terms).

Je, mwanahabari huyo aliptitia katiba ya nchi kabla ya kuongelea facts?

Kwa mujibu wa ibara ya 40 (4), jibu sahihi la swali juu ya kuanza kwa awamu ya sita au la, ni kuwa Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan amefungua awamu ya sita. Hivyo ndugu mtangazaji alikuwa sahihi! Je, amebahatisha au alikuwa na uhakika?

Rejea ibara ya 37, kifungu cha 5.
Uchaguzi na mapinduzi ndivyo hubadilisha awamu, hivyo ni ya 5.
 
Kwanini sasa Ali Mwinyi ni wa awamu ya 3 Zanzibar? Usipoelewa hadi sasa nikuachie ujuavyo na uwe na amani. Una uhuru wa kuelewa au kutotaka kuelewa. Usiwe na shaka, nitaheshimu mtazamo wako.
Awamu maana yake ni awamu za uchaguzi.Rais anayeingia kwa uchaguzi ndiye anayepewa awamu.Awamu hii ni ya Magufuli isipokuwa Samia amechukulia katikati kabla Magufuli hajamaliza,Hivyo awamu inabaki ya tano ila rais ni wa sita.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kwa maelezo yako Nyerere kwa hiyo alikaa awamu 2 na nusu yaani miaka 25 maana kama ulivyosema awamu 1 ina mihula 2 yaani miaka 10, inakuaje mpaka sasa jpm alikua wa awamu ya tano?
Ndio, Nyerere amekaa awamu mbili na nusu kwa formula ya sasa. Yaani Rais wa kwanza kwenye awamu 2.5!
 
Mwandishi alitakiwa awe mgambo wa jiji maana akili yake haiwezi kutafakuri
Mgambo wa Jiji anasema kuwa ukomo wa chini wa Rais madarakani ni miaka 8 na ule wa juu kabisa ni miaka 12 kutokana na mazingira. Endapo Mhe. Hayati Dr Magufuli angekuwa kabakiza miaka miwili muda wake uieshe, basi Mhe. Samia Suluhu angemalizia kwanza awamu ya 5 halafu angewania yake ya 6. Lakini kwa sababu ilikuwa zaidi ya miaka miwili, basi hii ni awamu ya 6 yenye miaka 9 na miezi kadhaa.
 
Acha upuuzi hiyo awamu ya sita uchaguzi uliitisha wewe? Unaelewa maana ya awamu?
Awamu maana yake ni awamu za uchaguzi.Rais anayeingia kwa uchaguzi ndiye anayepewa awamu.Awamu hii ni ya Magufuli isipokuwa Samia amechukulia katikati kabla Magufuli hajamaliza,Hivyo awamu inabaki ya tano ila rais ni wa sita,Uchaguzi ujao ndio utakaomuweka rais wa awamu ya sita.Usijifanye mjuaji kumbe hujui.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Samia ni Rais wa ngapi?
Jibu utakalopata ndiyo awamu yake pia hiyo. Hilo neno awamu linawachanganya wengi na mnajikuta mnabisha bila kujua!
 
Ndio, Nyerere amekaa awamu mbili na nusu kwa formula ya sasa. Yaani Rais wa kwanza kwenye awamu 2.5!
Daaah! Huko shule (kama kweli umepita) husa mnaenda kufanya nini!!?? Inasikitisha sana Tanzania yangu.
 
Mgambo wa Jiji anasema kuwa ukomo wa chini wa Rais madarakani ni miaka 8 na ule wa juu kabisa ni miaka 12 kutokana na mazingira. Endapo Mhe. Hayati Dr Magufuli angekuwa kabakiza miaka miwili muda wake uieshe, basi Mhe. Samia Suluhu angemalizia kwanza awamu ya 5 halafu angewania yake ya 6. Lakini kwa sababu ilikuwa zaidi ya miaka miwili, basi hii ni awamu ya 6 yenye miaka 9 na miezi kadhaa.
Miaka 9 inakujaje!!?? Vipi kama asipogombea 2025 hiyo miaka 9 itakuwa imetimia!?
 
Kweni nimeandika kuuwawa peke yake Mimi nilipigwa hadi kupoteza fahamu kwa kosa la kumpelekea chakula msimamizi wangu wa Chadema wakati wa Uchaguzi mkuu uliovurugwa
Embu tuondolee utopolo wako we pumbaf na hicho chakula chako kimba wee
 
Je, hotuba fupi ya Mhe. P. Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM taifa upande wa Tanzania Bara, inatoa mwanga zaidi juu awamu na mihula ya uongozi wa juu wa nchi?

Ingekua hivy

Ingekua hivyo iwapo tunge review katiba! Nyerere umsemae umeshafikiri alikua kwenye mzingo upi kikatiba dhidi ya muda wa utawala, alikanyaga katiba kwa kutawala miaka 20?
Ni wazi hapa kuwa Kuna kitu rahisi unashindwa kukuelewa mpaka nashangaa kwanini ujiite mwalimu. Umeelezwa humu kuwa neno awamu halijatajwa kwenye kipengele chochote cha katiba kinachohusu muda wa Rais madarakani. Neno awamu kwenye siasa zinazohusu muda wa Rais madarakani limetungwa tu ili kwa maslahi ya aliyelitunga na wanaolitumia.

Hapa kwetu mpaka sasa limetumika mara sita kutaja vipindi walimo Marais waliyopita na WA sasa lakini sio takwa la kikatiba. Unapozungumza habari ya kubadilisha katiba ili neno awamu litumike kikatiba unamzungumzia utopolo, hakuna mashiko hapo.

SSH angeweza kujiita Rais wa awamu ya sita au ya tano. vyovyote hakuna kosa. Lakini SSH amejitanabaisha kuwa yeye ni Rais wa JMT wa awamu ya SITA. wapi pagumu kuelewa hapo?
 
Back
Top Bottom