Kitaa kulikua na pisi moja matata sana, lakini alikua mtoto wa geti kali dadeki, mbaya zaidi bro wake tulikua tunakutana maskani tunapiga zetu kaya fresh kiufupi alikua mshikaji wangu na mimi nilimzimia sista ake,
Ile pisi ilikua kuiona kitaa peke yake nadra sana nakumbuka kuna siku nilijitosa nikaenda kwao eti kumuulizia bro wake, manzi kanifungulia geti fresh akasema bro hayupo, najipanga niombe namba nasikia sauti ya maza ake ananikaribisha ndani, damn! Zoezi likafeli,
Kuna mwanangu sana ule mchezo aliuelewa kua namzimia mrembo ila kumwambia shughuli,
Siku hiyo nimekaa zangu home nashangaa ugeni mzito ukanijia, ile pisi kali imefatana na mshikaji, kamfikisha halafu akajifanya kapigiwa simu anatoka one time, akanitumia msg "maliza leo leo, baada ya saa moja namrudisha kwao",
Aisee nilihaha, namwambia nini huyu mrembo, mbona ghafla sana sijajipanga, nikaweka movie mrembo yupo interested na movie, ananiuliza tu maswali kuhusu movie,
Baadae nikajiambia niache kupanic, nikarelax, tukaangalia movie yetu kweli baada ya saa moja mshikaji karudi, manzi kashukuru sana akaahidi kurudi weekend ijayo, nikawa gentleman sana sikumgusia chochote mpaka siku ya siku tukajikuta kitandani mahaba kama yote,
Sijui kutongoza naamini kuhusu chemistry, kama tunaendana tutakua kama hatuendani itaishia juu kwa juu, mimi ni demisexual na sapiosexual napenda kudate sapiosexual women.