Je, tofauti na kuishi milele ni kitu gani kingine sisi wakristo tutapewa?

Pepo kama Pepo watafasiri wa bibilia ndo walichanganya kumbuka biblia walitafsiri watu wa wapwani waislamu na ndio maana unaweza kuta maneno kama Shekh ikimaanisha wazee nk.

Kiswahili tuna paradiso mkuu hata ukisoma kiingereza (paradise)utakuna na neno hili hilo la paradiso.
Hata Kwenye Quran Ni paradise au Paradiso..
Kwa Kingereza Na Kiarabu Ni Janat
 
Mkuu hao ni waislamu sisi waziristan tumeahidiwa uzima wa milele tu. Na ndio maana nikauliza tofauti na huo uzima kuna kingine huko

Mkuu hao ni waislamu sisi waziristan tumeahidiwa uzima wa milele tu. Na ndio maana nikauliza tofauti na huo uzima kuna kingine huko?
Biblia imeongea hapo kuwa licha ya kupewa cheo cha juu kabisa kuwahi kutokea kwa Kiumbe chochote. Cheo cha "Uwana wa Mungu", pia Mungu ametuandalia mambo ambayo hayajawahi kufikiriwa katika ufahamu wa Mwanadamu:
Mambo ambayo tukiambiwa sasa hatuta yaelewa kutokana na kuwq na akili ya Kimwili:
Roho ina mambo yake tofauti kabisa na mahitaji ya Kimwili:

Ndio maana Yesu aliposhuka dunia hakufanya starehe yoyote na hakutaka kuishi sana hapa duniani:
Alirudi haraka mbinguni baada ya kumaliza kazi yake:

Mfano:
Mtoto mdogo ukimwahidi ahadi ya Ngono hatakuelewa kwakuwa hajafikia level ya ukubwa, hajapevuka: labda umwahidi soda ndio atakuelewa:
Hivyo Ahadi za Kiroho ni tofauti na hizi za Kimwili:
Ushanifaham hapo ?
 
Waislamu wao wakifika peponi Allah amewaofa mabikira 72 kwa kila mwanaume halafu wakaongezewa na pombe.

Upande wetu wakristo kwa madhehebu yetu yote tunaamini huko mbinguni hakuna koa wala kuolewa.
Sisi Yehova ametueahidi uzima wa milele (nijuavyo mimi).

Biblia inatoa sifa za ile mbingu mpya na nchi mpya baadhi ya sifa hizo ni kama.......

Hakutakuwa na kifo,jua wala mwezi ,magonjwa maandiko yanasema mji ule ni mzuri sana njia zake ni dhahabu safi malango yake ni lulu ule mji hautafungwa ( Mji ulikuwa unang'aa kwa utukufu wa Mungu. Ulikuwa unang'aa kwa uangavu kama yaspi, kito cha thamani sana. Ulionekana kwa uwazi kama kioo "ufunuo 21:11")

zaidi soma hapa Bible Gateway passage: Ufunuo 21 - Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi

Ukisoma kwa umakini wote utagundua hakika sifa nyingi umepewa ule mji wa wateuli biblia haijasema kama kutakuwa burudani zingine kama wenzetu wao waziwazi bila kufichwa wameahidiwa wanawake bikra tena warembo wenye macho kama bilauri.

Maswali yangu ya msingi ni haya JE TOFAUTI NA KUISHI MILELE NI KITU GANI KINGINE SISI WAKRISTO TUTAPEWA?
JE KAMA HAKUNA STAREHE KUNA HAJA GANI YA KUISHI MILELE?

KaribuniView attachment 3315146
Masuala ya kiroho sio marahisi kihivyo. Tatizo la binadamu anatafsiri mambo kwa kutumia akili za kimwili. Kama wewe ni Mkristo ngoja nikufundishe jambo:
1. Uzima wa milele tunaupata hapahapa duniani. Uzima huo upo ndani ya Yesu Kristo Yohana 17:3. Yeyote aliyemwamini Yesu Kama Bwana na Mwokozi wake tayari anao huo uzima. Yohana 3:36.
2. Ukimtafuta Mungu ukiwa hapa duniani kwa kuomba na kufunga utajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na utaanza kuonja uzuri wa mbinguni. Wakati mwingine ukiwa ktk maombi na ukafunikwa na nguvu za Mungu hisia za kimwili huondoka na unakuwa ktk roho kiasi kwamba mambo ya dunia hii hayaingii akinili. Huwezi kufikiria hata kula au kunywa kwa uzuri wa Mungu unao experience. Ndio maana ukiwa ktk uwepo wa Mungu ukitoka unashangaa muda ulivyokwenda. Ni kwasababu ulikuwa umeingia ktk realm ya kiroho ambayo haina Time.

3. Mtu akifa anaondoka ktk mwili. Hivyo huko anakokwenda hakutakuwa na hisia za kimwili bali za kiroho. Ndio maana huko mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa. Hakutakuwa na jinsia huko maana wote tutakuwa viumbe wa kiroho kama malaika. Lakini maandiko pia yanasema kuna kula na kunywa. Lakini ni vyakula na vinywaji vya kiroho sio kimwili.
Hao wenzetu Waislamu dini yao imewapotosha ndio maana wana mawazo potofu ya kuwatumia wanawake kama bidhaa. Mwanamke ni mtu kama alivyo mwanamume. Ndio maana Mungu aliamuru ndoa ni ya mke mmoja. Sasa niwaulize Waislamu, je kama mtapewa mabikira huko peponi je wanawake watapewa nini? Au wao sio binadamu? Hayo ni mawazo potofu ya zinaa!
 
Hahahaha!
ni tatizo sana Hahah Na wale waliofia Huko Kwenye Space na wenyewe Watarudishwa huku 🤣🤣
Tupo ndani ya Mungu ....hata huko ni ndani ya Mungu hakuna awezaye kuwa nje ya mungu ...sisi ni sehemu ya uungu wa mungu ..kisayansi wanasema vitu vyote ni energy matters na nafsi na ufahamu na akili na nguvu vyote ni energy sasa kama ni hivyo unawezaje kusrma hakuna mungu wa milele wakati tunajua uwezi kuidestroy energy wala kuunda bali energy inabadilikq tu kutoka formu moja hadi nyingine .
 
Masuala ya kiroho sio marahisi kihivyo. Tatizo la binadamu anatafsiri mambo kwa kutumia akili za kimwili. Kama wewe ni Mkristo ngoja nikufundishe jambo:
1. Uzima wa milele tunaupata hapahapa duniani. Uzima huo upo ndani ya Yesu Kristo Yohana 17:3. Yeyote aliyemwamini Yesu Kama Bwana na Mwokozi wake tayari anao huo uzima. Yohana 3:36.
2. Ukimtafuta Mungu ukiwa hapa duniani kwa kuomba na kufunga utajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na utaanza kuonja uzuri wa mbinguni. Wakati mwingine ukiwa ktk maombi na ukafunikwa na nguvu za Mungu hisia za kimwili huondoka na unakuwa ktk roho kiasi kwamba mambo ya dunia hii hayaingii akinili. Huwezi kufikiria hata kula au kunywa kwa uzuri wa Mungu unao experience. Ndio maana ukiwa ktk uwepo wa Mungu ukitoka unashangaa muda ulivyokwenda. Ni kwasababu ulikuwa umeingia ktk realm ya kiroho ambayo haina Time.

3. Mtu akifa anaondoka ktk mwili. Hivyo huko anakokwenda hakutakuwa na hisia za kimwili bali za kiroho. Ndio maana huko mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa. Hakutakuwa na jinsia huko maana wote tutakuwa viumbe wa kiroho kama malaika. Lakini maandiko pia yanasema kuna kula na kunywa. Lakini ni vyakula na vinywaji vya kiroho sio kimwili.
Hao wenzetu Waislamu dini yao imewapotosha ndio maana wana mawazo potofu ya kuwatumia wanawake kama bidhaa. Mwanamke ni mtu kama alivyo mwanamume. Ndio maana Mungu aliamuru ndoa ni ya mke mmoja. Sasa niwaulize Waislamu, je kama mtapewa mabikira huko peponi je wanawake watapewa nini? Au wao sio binadamu? Hayo ni mawazo potofu ya zinaa!
Mbinguni hakuna jinsia ya Kike:
Mungu na Malaika wote ni Wanaume ndio maana tunasali Baba yetu uliye Mbinguni: ( angalia majina ya Malaika hakuna la Kike)

Hebu soma hapa:

Isaya 50:1
Bwana asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo naliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.

Kutokana na Biblia Mwanamke wa kwanza ni Hawa:
Na Mwanamke aliumbwa kwa sababu ya kumpatia mwenza Adamu:

Yesu alishuka kama Mwanamume:
Hivyo hivyo huko Mbinguni wanawake watabaki na jinsia yao ya Kike, huku wakipata mema yote kama jinsia ya Kiume:
 
Uzima wa milele siyo tu maisha yasiyo na mwisho, bali ni maisha yenye maana ya kumjua Mungu na kumfurahia. Yohana 17:3 yasema: "Na uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma." Kumjua Mungu kikamilifu ni furaha kuu kuliko kitu chochote duniani. Hilo ndilo lengo la uzima wa milele kuishi kwa ukamilifu ndani ya mapenzi ya Mungu.

Kwa hivyo, hata kama hakutakuwa na starehe za kimwili kama ndoa, kula au burudani za duniani, maisha ya mbinguni yatakuwa ya furaha ya kweli, yenye kujaa upendo, utukufu, na ushirika wa milele na Mungu. Mathayo 22:30 inasema: "Kwa maana katika kiyama hawaozwi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika wa Mungu mbinguni." Furaha yetu haitatokana na mahitaji ya kimwili, bali kutoka kwa Mungu mwenyewe.

Hivyo, maisha ya mbinguni yameandaliwa kuwa ya uzuri wa kipekee, siyo kwa starehe za mwili bali kwa kushiriki utukufu, upendo na furaha ya Mungu isiyo na mwisho. Kama Paulo anavyosema katika 1 Wakorintho 2:9: "Mambo ambayo jicho halikuona, wala sikio halikusikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao." Hivyo, Wakristo wana tumaini la maisha ya kweli yenye maana, ya milele, na ya uzima mkamilifu kwa pamoja na Mungu.
Mkuu umejitahidi sana kuelezea na nikweli itakuwa hivyo lakini maandiko yamejikita kuelezea kile kitakachokuwa kwenye mji ule mpya. Swali langu bado limejikita kumuhusu binadamu atakaye faulu kuingia kwenye makao hayo haipo starehe ambayo ameandalia mbadala ya kumfanya afurahie zaidi.

Mwanzo2:1-2 inatuambia Mungu baada ya kumaliza kazi zake zote alistarehe maana yake kuna vitu Mungu vilikuwa tofauti na kazi zake zote za siku sita alizofanya kuistarehe haimaniishi kupumzika tu ni jambo pana sana ndio maana hapa duniani watu siku za kupumzika huwa wanaenda beach na sehemu maalumu za starehe.

Kwenye maandishi ya kijani hiyo furaha ya kweli itatoka wapi kama hakuna burudani?

Kama ndo ni jambo Takatifu kwanini mbinguni lisiwepo tena jamani.....hapahapa duniani tunahubiliwa na wahubili kuwa Ndoa ni paradiso ndogo itakuwaje kwenye paradiso kubwa isiwepo tena?
 
Ndio maana Yesu aliposhuka dunia hakufanya starehe yoyote na hakutaka kuishi sana hapa duniani:
Alirudi haraka mbinguni baada ya kumaliza kazi yake:
Huenda yesu alipofikisha miaka13-29 alikuwa anafanya starehe na kula bata za kila aina ndio maana kwa kipindi cha miaka hiyo haijaandikwa popote.

Historia ya yesu ni fupi sana ukiingalia kaelezewa kuanzia maandalizi ya mimba alipozaliwa na ikakoma akiwa na miaka12 then ikaibuka ghafla akiwa na miaka30. je umewahi kujiuliza ujana kamili wa yesu ulifichwa?

Umesema kitu muhimu sana mkuu kuwa kuna mambo mazuri na hayana mfano kwa akilizi zetu hata tukiambiwa hatutaelewa na ukatoa mfano wa mtoto. hapo nimekuelewa sana.

Ila kwa habari za yesu kuwa hakufanya starehe yoyote siwezi kukataa wala kukubali maana kuna miaka imekatwa makusudi tu bila sababu.

Baada ya kuikata hiyo miaka17 wakaja na stori kuwa "Kuna mambo mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo kama yangeandikwa yote, moja baada ya lingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa."(yohana 21:25)

Ukisoma kwa akili ya kawaida tu utangudua aliyaandika hapa siyo yohana bali ni watu fulani waliokubaliana na kupachika hayo maneno.

Injiri zote zna same story ya yesu kwanini luka au marko badala ya kukopi na ku paste yaleyale kwanini asingeliandika sehemu ya miaka 17 ambayo wenzie hawajaiandika?
 
Waislamu wao wakifika peponi Allah amewaofa mabikira 72 kwa kila mwanaume halafu wakaongezewa na pombe.

Upande wetu wakristo kwa madhehebu yetu yote tunaamini huko mbinguni hakuna koa wala kuolewa.
Sisi Yehova ametueahidi uzima wa milele (nijuavyo mimi).

Biblia inatoa sifa za ile mbingu mpya na nchi mpya baadhi ya sifa hizo ni kama.......

Hakutakuwa na kifo,jua wala mwezi ,magonjwa maandiko yanasema mji ule ni mzuri sana njia zake ni dhahabu safi malango yake ni lulu ule mji hautafungwa ( Mji ulikuwa unang'aa kwa utukufu wa Mungu. Ulikuwa unang'aa kwa uangavu kama yaspi, kito cha thamani sana. Ulionekana kwa uwazi kama kioo "ufunuo 21:11")

zaidi soma hapa Bible Gateway passage: Ufunuo 21 - Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi

Ukisoma kwa umakini wote utagundua hakika sifa nyingi umepewa ule mji wa wateuli biblia haijasema kama kutakuwa burudani zingine kama wenzetu wao waziwazi bila kufichwa wameahidiwa wanawake bikra tena warembo wenye macho kama bilauri.

Maswali yangu ya msingi ni haya JE TOFAUTI NA KUISHI MILELE NI KITU GANI KINGINE SISI WAKRISTO TUTAPEWA?
JE KAMA HAKUNA STAREHE KUNA HAJA GANI YA KUISHI MILELE?

KaribuniView attachment 3315146
Assume mtu ni mkristo amekufa hajawahi kuoa wala kuzini akifika mbinguni kwenye uzima wa milele na kusifu na kuabudu hauoni kama atakuwa amaeonewa kwa kutopatiw nafasi ya kuonja duniani?
 
Masuala ya kiroho sio marahisi kihivyo. Tatizo la binadamu anatafsiri mambo kwa kutumia akili za kimwili. Kama wewe ni Mkristo ngoja nikufundishe jambo:
1. Uzima wa milele tunaupata hapahapa duniani. Uzima huo upo ndani ya Yesu Kristo Yohana 17:3. Yeyote aliyemwamini Yesu Kama Bwana na Mwokozi wake tayari anao huo uzima. Yohana 3:36.
2. Ukimtafuta Mungu ukiwa hapa duniani kwa kuomba na kufunga utajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na utaanza kuonja uzuri wa mbinguni. Wakati mwingine ukiwa ktk maombi na ukafunikwa na nguvu za Mungu hisia za kimwili huondoka na unakuwa ktk roho kiasi kwamba mambo ya dunia hii hayaingii akinili. Huwezi kufikiria hata kula au kunywa kwa uzuri wa Mungu unao experience. Ndio maana ukiwa ktk uwepo wa Mungu ukitoka unashangaa muda ulivyokwenda. Ni kwasababu ulikuwa umeingia ktk realm ya kiroho ambayo haina Time.

3. Mtu akifa anaondoka ktk mwili. Hivyo huko anakokwenda hakutakuwa na hisia za kimwili bali za kiroho. Ndio maana huko mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa. Hakutakuwa na jinsia huko maana wote tutakuwa viumbe wa kiroho kama malaika. Lakini maandiko pia yanasema kuna kula na kunywa. Lakini ni vyakula na vinywaji vya kiroho sio kimwili.
Hao wenzetu Waislamu dini yao imewapotosha ndio maana wana mawazo potofu ya kuwatumia wanawake kama bidhaa. Mwanamke ni mtu kama alivyo mwanamume. Ndio maana Mungu aliamuru ndoa ni ya mke mmoja. Sasa niwaulize Waislamu, je kama mtapewa mabikira huko peponi je wanawake watapewa nini? Au wao sio binadamu? Hayo ni mawazo potofu ya zinaa!
Mkuu ukisema kila kitu tukijadili kiroho sidhani kama itakuwa rahisi hivyo ndio maana hata yesu mwenyewe alikuwa anatumia mifano ya duniani hapahapa.

Inasemekana baadhi ya wanafunzi wa yesu walimuacha wakaendelea na kazi zao sasa ujiulize hao walikuwa wanatembea na yesu na kuona miujiza kwa macho yao lakini ilifika mahali hata wao hawamuelewi ikabidi wawe wanamuuliza wakiwa falagha rejea mfano wa mpanzi.

Yesu walimuacha hadi akawauliza na ninyi mnataka kuniacha? petro akajibu akasema hasha Bwana tukuache twende kwa nani?.........
 
Back
Top Bottom