Je, TRA wamesikia kilio chetu cha Ushuru wa kuingiza magari?


Mama SSH nimemkubali sanaa,kuna gari wakati wa JIWE kodi ilikuwa 6m ila sasa nimeona ni 4.5m....#SSH_MIKUMI_TENA_MATHA(MAKE TANZANIA HAPPY AGAIN).

JIWE alikuwa hataki watu wapate raha,alikuwa anataka watu waishi kama mashetani.
 
Si kweli. Usitumie mfano mmoja tu kutaka kuwapa matumaini watu. Ushuru uko vilevile.
 
Kikokotoo kinaonesha ushuru kushuka kwa magari yote au hayo makubwa kubwa wanayoyaita ya "kifahari"
 
Kwa nini?

Ni kwamba kati ya Watanzania takriban milioni 60, ni yeye tu mwenye kuiweza hiyo kazi mpaka alazimishwe kuifanya hata kama hataki?

Fikra dhaifu sana hizo katika karne hii ya 21!
Mkuu na wewe unataka? wewe kabisa? au unafanya udalali?
 
Yaani sijui tulichelewa wapi kumpata huyu mama yetu . Ila wanasema Majira ya Mungu yakitimia hakuna wa kupiga.

From now, huyu ndio raisi wangu bora kuliko wote waliopita. Ndani ya mwezi mmoja tumeona mabadiliko, Mungu amsimamie kwakweli. Huu mwaka tutaona mengi tusubiri, na Mungu awe pamoja naye
 
Magari yanayoagizwa sana, mfano Toyota iSt bado umeng'ang'ania palepale kwenye ongezeko
 
Si kweli. Usitumie mfano mmoja tu kutaka kuwapa matumaini watu. Ushuru uko vilevile.

Magufuli nilikua nampenda, lakini huyu mama vitu ambavyo hatukuwahi wala kutegemea kama vitakuja kubadilika yeye kavibadilisha. Ushuru ushuru ushuru hii kitu hatukutegemea kabisa yeye kaweza. Aise Mungu ambariki.
 
Kwa nini?

Ni kwamba kati ya Watanzania takriban milioni 60, ni yeye tu mwenye kuiweza hiyo kazi mpaka alazimishwe kuifanya hata kama hataki?

Fikra dhaifu sana hizo katika karne hii ya 21!
Yani hii comment imenifanya mpaka niwaze facial expression yako wakati unaiandika,ni kama ulitamani mtoa comment awe mbele yako umnase kibao๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚!Mama oyeeee
 
Mm nasoma nabaki nacheka tu.

Kuna mtu kabisha hapo kuwa bei za gari ni ndogo ndo maana kodi ni tofauti. Sasa si akaombe zawadi ya gari huko nje asilipe kodi.
 
Mkuu hebu tuwekee na data za gari ya uchumi wa kati IST
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ