GE2025 Je, Uharam wa ‘Candidacy’ ya Rais Samia hauwezwi kupingwa mahakamani?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mahakama zimekuwa za kihuni zikitumika kisiasa kwa ushirikiano na dipipi. Sidhani kama huyu mgombea wa viti maalumu anaweza kufanyiwa chochote
 
Urahisi mtamu,,,, Januari alichokifanya huyu Mama ni kiboko
 
Tatizo ni moja tu, jee tunazo Mahakama Tanzania? Kwa kinachoendelea kwenye kesi ya uhaini ya Lissu na ile ya Wazanzibari vs uongozi wa Chadema ni dhahiri hatuna Mahakama Tanzania.
Na ieleweke, tunapachukua hatua zisizo halali na kufanya mahakama zetu kuwa rubber stamps, haitaishia kwa wapinzani tu,kuna siku zitakosa maana na kwenu mnaozitumia vibaya!
 
Kama una vielelezo vyote uoga wa nini wa wewe kwenda kufungua kesi? Au ni yaleyale ya waende wengine?
 
Namuonea huruma sana mama Samia kila kona mishale sio ccm sio upinzani sio wananchi binafsi niliahidi kwa mara ya Kwanza kura yangu kumpigia mama Samia Kama mgombea wa CCM hapo mwanzo kabisa ghafla akaanza kufanya vitu vya kunihudhunisha na kunivunja moyo daah ila bado anakura yangu ikiwa tu atafanya reforms za uchaguzi. Mama Samia mimi nakupenda sana fanya reforms acha kuyabeba hayo maccm hayakupendi yanakung'ong'a tu Turudishie haki yetu yakuchagua Viongozi tunaowataka na hata wewe ukishindwa bado Taifa Lita kukumbuka kwa ujasiri wa kurudisha nguvu kwa wananchi. Mungu wa Mbinguni akulinde
 
Urahisi mtamu,,,, Januari alichokifanya huyu Mama ni kiboko

Amegoma kujadiliwa akiwa hayupo ndani ya ukumbi, amevunja kanuni, taratibu, desturi na kuwatisha wajumbe wasiwe huru katika zoezi la kujadili kama anafaa au la.
 
 
 
Mkuu Tz kuna mahakama inayoweza kutoa haki?

Mahakama zingelikuwa 'dependent', tungeliweza kujadili agenda yako, lakini kwa mahakama hii iliyojaa genge la machawa ni kupoteza muda, hakuna haki pale.
 
Atakayeenda Mahakamani atauawa haraka sana
 
Maombi hayawezi itoa serikali mbaya mahakamani
 
Mimi naongeza hoja, juu ya hoja.
Akitokea/wakitokea wa aina hiyo; basi waiombe mahakama isitishe shughuli zote za chama hadi swala hilo litakapo tolewa uamzi.
 

Uchumi unapaa sekta zote
Sekta ya huduma za jamii ni bora kuliko awamu zote.
Uchumi upi umepaa? Bei za bidhaa zinapaa kila siku
Huduma za jamii zipi ni bora? Hospitali hazina dawa ni mwendo wa kujinunulia tu.
 
Naona upo umekumbatia buyu la asali na huelewi kitu kingine chochote nje ya hilo buyu!

Hao waTanzania wanaoPotea na wengine kuuliwa, kwako hayo ni matukio yasiyoweza kukusumbua kutokana na utamu wa asali ulivyo kuingia akilini?

Taarifa ni hii mkuu, Samia anataka kukiuka taratibu zote, siyo ndani ya chama pekee, bali hata nje ya chama ili abaki madarakani nje ya taratibu kwa kutumia njia haramu zote.

Sasa, kama mnampenda kiasi hiki unacho onyesha, na jinsi unavyo mumwagia sifa nyingi hivi; kuna sababu gani ya kuhofia juu yake. APitie tu kwenye taratibu, na mambo yote yatanyooka, kwani shida ni nini hasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…