Kama kazini analipwa elfu 7 kwa siku akibeba mizigo je? ๐๐๐๐
Mahusiano ya Tz yana kizungumkuti sana, wengine chuoni tulikuwa na boyfriends mnaishi kila mtu anatumia pesa yake aliyopewa na wazazi wake,wanawake wenzio wanakuambia huyo atakupa nini. Huku kwetu ndio maana wasichana wadogo wanadate wakaka wakubwa au watu wazima, utasikia watu wazima wametulia na wanajielewa, huu ni uongo, sababu kubwa ni kutaka Kuhudumiwa utadhani yatima. Ni sahihi mpaka umri fulani msichana kuendelea kupata huduma kwao.
Watoto wa kiume nao kuruka stage, unaanzaje kuhudumia ikiwa hujasimama kiuchumi, bora kwa kipindi fulani uachane na suala la mapenzi hadi utakapokuwa tayari kimajukumu.
Wamama tulee watoto wakike vizuri, tuwapeleke shule na tuwafundishe majukumu yao ikiwa watakuwa wamefikia umri wa kutaka mahusiano, vivo hivyo kwa wanaume.
Kwenye ndoa tu ndipo mwanaume anapaswa kuhudumia, huku kwingine ibaki zawadi na motisha tu, tena ikiwa he can afford them.