Je, ukweli ni upi kuhusu vyombo tunavyotumia Kwa chakula?

Je, ukweli ni upi kuhusu vyombo tunavyotumia Kwa chakula?

Wale jamaa wanapika machapati makubwa kwanin wanatumia sponji kugeuzia Ile michapati Yao! Sio salama Ile sponji
Watu hawana Elimu sahihi, ukiwauliza Kwa nini mnafanya hivi , mbona wengine wanafanya, tumefundhishwa na vikundi vya usajiriliamali kufanya hivyo.

Elimu sahihi ni muhimu sana 🙏 ✅
 
Kuna research yeyote iliyothibitisha kua hayo matatizo ya ugonjwa wa Kansa yamesababishwa na hayo masufuria?

Unaweza kulaumu masufuria kumbe tatizo kuu ni Pombe fake zinazouzwa huko mitaani,na watu wanazifakamia kama maji,unaweza kulaumu masufuria,kumbe tatizo ni Energy drinks.
Upo utafiti tele wa kisayansi unaoonyesha "forever chemicals" za kundi la PFOA ni kisababishi kikubwa zaidi cha kansa. Hizi Sufuria non-stick zinazoingiziwa Tanzania na nchi nyingine nyingi masikini za Africa na kwingine duniani kutoka China kuna uwezekano mkubwa zinazalishwa kwa materials zenye forever chemicals zilizopigwa marufuku kwingine duniani kwenye nchi zilizoendelea kwa sababu ni materials za bei rahisi.
 
Upo utafiti tele wa kisayansi unaoonyesha "forever chemicals" zenye PFOA ni kisababishi kikubwa zaidi cha kansa. Hizi Sufuria non-stick zinazoingiziwa Tanzania na nchi nyingine nyingi masikini za Africa na kwingine duniani kutoka China kuna uwezekano mkubwa zinazalishwa kwa materials zenye forever chemicals zilizopigwa marufuku kwingine duniani kwenye nchi zilizoendelea.
Hujaelewa comment yangu,

Sijaongelea Kisababishi cha ugonjwa wa kansa bali nimeongelea Kinachofanya ugonjwa huo kuongezeka huko Bongo,

Ndio maana nikauliza,kuna research kua ni masufuria ndio yameongeza idadi ya wagonjwa wa kansa na sio pombe fake au energy drinks au sababu zingine zozote?
 
Hizo hazitumiki kutengenezea vyombo sasa zina kazi zingine kabisa na zinawekwa mahali salama, so hazitahusika kwenye hoja ya mtoa mada basi!
Ulaya, Marekani na nchi zilizoendelea ndio wamepiga marufuku kutengenezea au kuuza vyombo vyenye PFOA lakini sisi huku Africa sidhani kama kuna serikali hata moja ina habari ya haya mambo au kuzingatia kwa hiyo Wachina wanaweza kuwa wanaendelea kutuuzia tu Sufuria za material ya aina hiyo hasa ukizingatia sio hata muda mrefu sana zimepigwa marufuku kwenye hizo nchi zilizoendelea.
 
Back
Top Bottom