Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Hakuna mwanamke ambaye ana haki ya kusema yeye hana bahati ya mahusiano kiukweli ni uongo. Wanawake wengi ule umri wa kuwa mabinti na kuwa na mvuto wao huwa wanautumia kuleta maringo na kuruka na wanaume tofauti wakiamini hakuna kuzeeka.Acheni kumpa moyo kinafiki, mwambieni ukweli hasa ninyi wanawake wenzie.
Iko hivi;
Mara zote maisha ya mwanamke huwa yanakuja na expire date kinyume na kwa mwanaume. Muda ambao binti unakuwa unapigiwa miruzi mingi, kijana wa kiume kwa muda huo ni sifuri kabisa ila ikifika muda sasa kila mtu anajitenga na wewe ndipo kijana huyu wa kiume unaelingana nae kiumri ndipo anaanza kuhesabu namba zake.
Nachokiona kwako ni ile kawaida yenu ya nyodo kupitiliza uliyokuwa nayo kwa waliokuwa wakikufuata. Kuchagua halijawahi kuwa tatizo kwangu ila hapo kwenye nyodo hapo ndipo panapokujaga kuwasurubu wengi wenu
Mwanamke ana miaka 10 tu ya kucheza karata zake na kuwa na uhakika wa kushinda nje ya hapo ni kubet na maisha yake.
Binti ana advantage ya kufanikiwa kimahusiano akiwa kati ya umri wa miaka 16 hadi 25. Kuanzia 26 hadi 30 huo ni umri wa nenda kwa tahadhari au lala salama.
Akivuka tu hizi stage mbili ndio basi. Huko mbele ni kubahatisha kwenda mbele.