Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Hakuna mwanamke ambaye ana haki ya kusema yeye hana bahati ya mahusiano kiukweli ni uongo. Wanawake wengi ule umri wa kuwa mabinti na kuwa na mvuto wao huwa wanautumia kuleta maringo na kuruka na wanaume tofauti wakiamini hakuna kuzeeka.

Mwanamke ana miaka 10 tu ya kucheza karata zake na kuwa na uhakika wa kushinda nje ya hapo ni kubet na maisha yake.

Binti ana advantage ya kufanikiwa kimahusiano akiwa kati ya umri wa miaka 16 hadi 25. Kuanzia 26 hadi 30 huo ni umri wa nenda kwa tahadhari au lala salama.

Akivuka tu hizi stage mbili ndio basi. Huko mbele ni kubahatisha kwenda mbele.
 
Kwa mwanamke kufika 30s si nzuri though sio umri ulioenda saana.

Usiogope,AMUA.
Hata mimi nipo tayari niishi nawe,natakupenda nitakujali nitakuheshimu. Na tupate watoto wetu 2 wazuri wa interval ya miaka 2.
 
Mmmmmmhmn. Unajua mtu mzima kumdanganya mtu mzima mwenzake kama mtoto mdogo sio uungwana. Hivi mtu yupo 30,watoto wengi wanatokea wapi labda kama ata adopt wengine.

Hebu tazama, mtoto anabebwa tumboni miezi 9. Kumlea hadi kuwa tayari kumuachisha kunyonya ili usim'bemende yaani uzazi na malezi ya mtoto mchanga ni miaka si chini ya mitatu, so ukijumlisha na ile miezi tisa ya kubeba tifanye ni mwaka kabisa so ni miaka minne hiyo imekwenda. Miaka 30 + 4 ni miaka 34. Akiongeza mtoto wa pili bila kupumzika ni 38 hiyo wa tatu mfululizo itakuwaje sasa?

Kimsingi ni mtego mbaya sana wa kujiingiza mwenyewe. Hapo pia uombe MUNGU sasa awe na experience nzuri ya malezi ya watoto ama kama sivyo anaweza pata kichaa maana kudeal na watoto wadogo umri ukiwa mkubwa nayo inataka utulivu na ujuzi kuwalisha,kuwatrain,kuwafunza tabia,etc sio kazi ya dakika tano plus mtoto wako ni jukumu lako 100% bila kusaidiwa, bado maisha yanakusubiri, huku mume ambaye hamjuani maana m'mekutana mkiwa wakubwa umri umeenda so una struggle kubalance ndoa, familia, uchumi,malezi na afya yako ya akili na mwili. Hii ni kujipa kazi ambayo ungeanza mapema at 20s ungekuwa salama zaidi.

Kitu sipendi ni kumshauri mtu kinadharia bila kuzingatia uhalisia wa maisha yanakwendaje. Mwanamke suala na mahusiano na uzazi na ujenzi wa familia anatakiwa kulichulia serious kuliko kitu chochote hapa duniani maana lina limit ya muda na haliwezi kusubiria.

Shule unaweza soma hata ukiwa na 30 utaenda kusoma, ila ukifika 30 unakuwa na mitihani mingi sana kuanzisha familia kama mwanamke wa kawaida na kujenga mahusiano mazuri na mwanaume maana wanaume wengi utakaokutana nao huko ni reject au complicated.
 
Wapi sasa?
 
Okay wacha tuone. Kinachowafelisha wengi ni kutafta perfect match.
Humu watu wanatoa ushauri utadhani mtu anataka kununua kiwanja kumbe mtu anataka kujenga mahusiano ili aanzishe familia masikini.

Mimi nawaonea huruma sana mabinti wa kizazi hiki maana jamii imewaachia uhuru fulani hivi wa kucheza na maisha yao wakidhania huko mbeleni wanadhamana ya kutoboa kifamilia na kimahusiano. Huwa nawaonea huruma sana nikiwa natafakari future zao.
 
Kwa wanaume ukiwa senior bachelor basi ukimpata binti kwa gia ya kumuoa unakuwa na test ya kumshawishi tena aamini hujawahi kuoa na ukisema huna hata mtoto basi ujieleze tena kwa nini huna![emoji16]
Mimi huo muda siwezi kuwa nao. Kwa mtu mwenye akili timamu atajua ukiona mtu anakuuliza maswali ya kipuuzi jua hatumii akili anatumia hisia
 
Cha ajabu unaweza kuja kumuoa binti yangu[emoji23][emoji23][emoji23]. Wanaume mna raha kweli
Unasema hivi kuna mdada tulicheza sote utotoni huko. Mdogo wake wa mwisho mimi siwezi kudate nae kwa sasa maana ameshakuwa mama, mtoto wake huyo dada mzaliwa wa mwaka 2000 akiniona anaona mimi chaguo lake.[emoji23][emoji23][emoji23]

Ni vile tu wengine maadili yametushika ningeweza mtembezea moto dada mtu mdogo wake na mtoto wao pia.
 
You are right. Lakini msizipuuze love language zetu 🀣🀣
 
Hakunaga maisha ambayo yatakutaa kabisa ukose mfumo wa kuishi na kujenga familia. Tatizo katika mahusiano ya miaka hii na hawa wanawake wa kizazi cha kuanzia 1985 kuja huku mbele ujuaji ni mwingi.

Mwanamke hataki kuanzia chini anataka kuanzia level ambayo inawataka muwe na kipato cha kuanzia milioni 3 kwa mwezi huku yeye haweki hata buku mezani na anaishia kukwambia wewe si ni mwanaume.

Kuna brother m'moja nimejifunza kwake. Alianza na mkewe walifunga ndoa huyo bro akiwa anakaa kwao yaani vyumba vya uwani. Wakakaa miezi michache wakaenda kupanga sehemu hapo vyumba vya 30,000 viwili yaani chumba na sebule. Na hiyo sehemu ni bondeni mvua ikinyesha unacheza twist na tope na madimbwi ya maji hadi ukome mixer vyura wanakutumbuiza hadi alfajiri, ila ndipo walipoanzia.

Leo wana nyumba nne moja ndio wanaishi tatu wamepangisha, wana magari mawili mke analake mume ana lake. Wana watoto 4.

Kimsingi maisha yanataka utulivu na projection nzuri ya mnaelekea wapi pamoja. Hizo fujo za nataka mwanaume mrefu, awe ana akaunti yenye seven figures, awe na gari na nyumba nzuri ya kupanga kuanzia vyumba vitatu iwe ndani ya fensi. Haya maisha ya ndoto za mchana huwa yanawagharimu sana mabinti wa kisasa na tamaa zao.

Mwanaume ukute amejiimarisha hivyo halafu awe anakungoja wewe tu utokee akushobokee? So wewe ni nani aisee.
 
Hapa bado unatoa faraja. Kidonda hakiponi kwa kupulizwa ndugu, kinatakiwa kusafishwa kwa dawa na kupakwa dawa ya kukausha kisizidi kuambukiza na kuoza.

Kusafisha kidonda si kazi ndogo aiseee maumivu huwa ni makali. Sasa wewe ni kama mtu anae mwambia mleta mada asikubali kusafishwa ataumia ila atulie wewe umpulize hata umia.

Sasa jiulize unamsaidia au unataka alale usingizi wa nusu kaputi huku anachelewa kuamka kutatua changamoto zake?

Wanaokupenda na kukujali wanakupa makavu live.
 
Hivi kwanini Mwanamke akifika miaka 25+ kama hana Mtoto wala Mume anachanganyikiwa alafu Mwanaume anaweza kua na 32+ hana Mtoto wala Mke alafu fresh tu hata hapagawi???
Wala siyo wao ni jamii ndio imewajengea wanawake hasa wa kiafrika hiyo mentality so wanakuwa hivyo kwa sababu wanaogopa jamii itawachukuliaje, laiti kama jamii ingeacha kuwasema vibaya wanawake wanaochelewa kuolewa au kuzaa kama kwa wenzetu wazungu basi mtashangaa wanafika hadi miaka 40 na hata hawashituki, kitu ambacho wanaume hamtaki ndio maana mnaendelea kuwasema na kutumia ndoa kama fimbo ya kuwachapia ili waolewe mapema iwe faida kwenu na wawe watumwa wenu
 
Tumetofautiana kwa namna tunavyoyatazama mambo...... inawezekana upande uliotazama wewe sio niliotazama mimi hivyo nimeamua kuheshimu maoni yako.........

NB;
Huwezi kujua kuwa dunia ina mambo mpaka likukute jambo.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…