Habari ya weekend great thinkers?
Maisha yananipa experience tofauti, Sikuwahi kufikiria kama ningefika third floor bila kuwa na familia wala watoto, kuna muda nahisi kupanic nahofia watoto wasije kuniita bibi badala ya mama, au kukosa kabisa sababu ya umri mkubwa🤔
Enzi hizo nilikua nashangaa mtu hasa mdada unafikaje hadi 30s huna familia, aisee kumbe ni kweli now ni mimi mwenyewe.
Mlioanza familia mkiwa 30s je ni kweli au mnaona dalili za watoto wenu kuwaita bibi au babu? Vipi changamoto za uzazi sababu ya umri mkubwa?😔
Nipo tayari kwa comments zote.
Happy valentine's day in advance 👏🥰
Ingawa sina hakika kama ni kweli au unafurahisha genge, Pole sana mkuu.
Ndoa ni ishara ya ushindi na mafanikio kwa Wanawake wengi Duniani hasa Barani Afrika, middle east na Asia. Hivyo, wakigusa 30 bila ndoa hujiona kuwa wameshindwa kufikia lengo muhimu na kuianguasha jamii yao hasa wazazi.
Uzoefu unaonyesha hakuna kanuni ya upi muda sahihi wa kuoa au kuolewa, wewe mwenywe ndio determinant ya lini ni muda sahihi kuolewa. Ila kuna muda sahihi wa kuzaa kwa mwanamke 24- 36. Ukizaa ukiwa mzee kuna hatari za kiafya kwa mtoto. Sayansi inaonyesh ukizaa ukiwa kwenye 20s kuna tija zaidi kwa mtoto.
Ila unapaswa kutambua facts zifuatazo ili uweze kujua namna ya kutoboa. Kwanza, mwanamke ana nafasi ndogo sana ya kuamua nani amuoe na lini. Fact nyingine ni kuwa kwa kadri umri unavyosonga ndivyo mvuto wa kimapenzi wa mwanamke unapungua na eventual rate ya watia nia sahihi nayo inapungua. Fact nyingine ni kuwa ukiwa mrembo na ukiwa na umri mdogo na ukiwa na uwezo mkubwa wa kumpa furaha mwanaume unakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuolewa mapena. Bahati mbaya warembo wengi Duniani huwa hawana uwezo wa kuwapa furaha wanaume kutokana na demnd yao kuwa kubwa. Fact nyingine unapaswa kuelewa kuwa wanaume regardless ya utajiri au level ya elimu huwa wanatafakari sana kabla ya kufanya maamuzi ya kuoa, wanawahofia sana wanawake. Wanaume wanataka mwanamke atakayempa heshima, furaha na amani. Ingawa siku hizi kuna wavulana ambao wao wanapenda zaidi physical materials kutoka kwa mwanamke. Mwisho wanaume wengi wenye akili na wanaojiamini huwa hawapendi mwanamke mwenye akili sana au mtafutaji sana kwa sababu wanaamini kuwa wao wanajimudu. Kujua Kudeka, kubembeleza, sauti na ufundi wa ngono ni silaha muhimu za ushindi.
Kwa umri ulio nao unaweza ukafanya yafuatayo:
Kuzaa bila kujari suala la kuolewa. Athari yake ni kuwa utapunguza zaidi fursa ya kuolewa na mwanaume wa maana na unaweza kumpa mtoto changamoto ya kimalezi na tabia. Wenzenu Ulaya, America na Asia uenda Baa na kujitegesha kwa walevi.
Oa, tafuta kijana anayetaka kulelewa muoe.
Boresha tabia, kuwa msafi (ng'aring'ari) ndani na nje muda wote, kuwa simple, usiwe much know kwa sana, safiri mara kwa mara, kata mawsiliano na EXs, take risk ukiombwa mzigo. Usiende kwenye game bila kuoga, kamwe.
Kamwe usimwambie mwanaume kuwa upo jamii forum na ukiwa na mwanaume punguza kuwa busy na simu.
Ukiwa kwenye dating ukakutana na mtu unayemfahamu msarimie then mpotezee focus kwa mwanaume wako.
Usiwe mtu wa kutoa options za hoteli au sehemu nzuri ya kutoka out. Ukipewa nafasi ya kuchagua mwambie sijui akikulazimisha, chagua kati ya maeneo ambayo amewahi kukupeleka.
Usiombe pesha, omba kitu
Ukiwa na mwanaume mweleze watu muhimu kwako na namna unavyo link nao. Likewise mbembeleze naye akwambie watu wake wa muhimu.
Mhaminishe mwanaume kuwa unatamani kumzalia wato, kamwe usimwombe akuoe.
Mwisho, hakuna kanuni kwenye kumpata mwenza, hivyo yote haya yanayosemwa ni kubahatisha tu.
Mungu akubariki upate itaji la moyo wako.