Hakunaga maisha ambayo yatakutaa kabisa ukose mfumo wa kuishi na kujenga familia. Tatizo katika mahusiano ya miaka hii na hawa wanawake wa kizazi cha kuanzia 1985 kuja huku mbele ujuaji ni mwingi.
Mwanamke hataki kuanzia chini anataka kuanzia level ambayo inawataka muwe na kipato cha kuanzia milioni 3 kwa mwezi huku yeye haweki hata buku mezani na anaishia kukwambia wewe si ni mwanaume.
Kuna brother m'moja nimejifunza kwake. Alianza na mkewe walifunga ndoa huyo bro akiwa anakaa kwao yaani vyumba vya uwani. Wakakaa miezi michache wakaenda kupanga sehemu hapo vyumba vya 30,000 viwili yaani chumba na sebule. Na hiyo sehemu ni bondeni mvua ikinyesha unacheza twist na tope na madimbwi ya maji hadi ukome mixer vyura wanakutumbuiza hadi alfajiri, ila ndipo walipoanzia.
Leo wana nyumba nne moja ndio wanaishi tatu wamepangisha, wana magari mawili mke analake mume ana lake. Wana watoto 4.
Kimsingi maisha yanataka utulivu na projection nzuri ya mnaelekea wapi pamoja. Hizo fujo za nataka mwanaume mrefu, awe ana akaunti yenye seven figures, awe na gari na nyumba nzuri ya kupanga kuanzia vyumba vitatu iwe ndani ya fensi. Haya maisha ya ndoto za mchana huwa yanawagharimu sana mabinti wa kisasa na tamaa zao.
Mwanaume ukute amejiimarisha hivyo halafu awe anakungoja wewe tu utokee akushobokee? So wewe ni nani aisee.