Sasa ndugu tutakubali wangapi ina maana kila anaenitafuta basi nikubali tu…
Imagine upo kwenye mahusiano serious then atakee mwanaume anamtafutatafuta mwanamke wako utajisikiaje???
Nyie wanaume mnapenda kuwalaumu wanawake kwa vitu ambavyo kiuhalisia sisi hatuna maamuzi mimi siwezi kumkataa mtu wakati sina mtu ukiona mtu anazingua ujue ana mtu wake sasa unataka amuache mtu wake awe na wewe???
Sio kwamba tunaringa ni vile tu tunaamini kwamba tulio nao watatuoa… kama mtu anajua kabisa huyu mtu awezi kumuoa sidhani kama ataendelea na mahusiano tatizo nyie vijana ni waongoo
Hahaha wanawake saa ingine mnanifurahishaga, sisemi ukubali kila mtu anaekutongoza, ila utakuta unamfata mdada anakukataa kwa kukwambia ana mtu wake, hiyo kukataliwa ni sawa haina shida, ila sasa ukichunguza, mara nyingi utakuta huyo mtu mwenyewe anaeitwa boyfriend, ukijilinganisha nae unajiona bora hata wewe uliekataliwa, mtu mwenyewe sasa
1)Mume wa mtu
2)Babu mzee mstaafu
3)Kijana wa hovyo kitabia, muonekano rafu, anaekaa mtaani bila mishe.
4) Anadai ana mtu wake, ila utaona kabisa huyo mwanaume hamuhudumii huyo mdada, wala kumjali kwa chochote, unaona huyo mwanaume anafata sex tu toka kwa huyo mdada, mdada nywele anasuka twende kilioni, smartphone ina crack za kutosha, unajiuliza boyfriend wa huyu mdada anashindwa kumpa mwanamke wake monthly expenses for her upkeep, mdada apendeze, unajiuliza boyfriend wa huyu mdada haoni thamani ya alicho nacho.
Au utakuta mfano mwanamke anafanya kazi zisizoendana na hadhi yake k.v kuosha nywele saluni za wanaume, au baa, halafu anakukataa kwa kusema ana boyfriend, imagine huyo ni boyfriend wa namna gani.
Basi utakuta mwanaume unakosa cha kufanya, unaangalia tu kwa uchungu, jinsi mdada uliempenda alivomchagua baraba na kumkataa Yesu
mamamzungu