Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Mpe talaka dada ake.
 
yani umeniua mbavu sina sikutegemea kucheka kwa sauti ivi,umewaqza nini?
aiseee walikasirika nini?dah umewaza nini kiongozi naiyo sentensi yako
 
Mkuu Godee jr ushauri ni huu japo waweza kuwa hauna manufaa kwako, hebu mwachie Mungu, mlilie Mungu anayejua jasho ulivyolipata, nakuhakikishia Mungu hatakutupa atakupatia riziki nyingine na nyumba yako itaisha utahamia. Huyo shemeji yako hata ukisema ugombane naye italeta ugomvi mkubwa hadi kwa dada yako na wapwa zako.
Piga goti kwa Mungu, mwambie yote (japo anayajua) na bila hiyana atakuwezesha kukamilisha nyumba yako na mambo mengine mengi ya maendeleo.
 
Aisee kwenye suala la pesa sitakaa nimuamini mtu yeyote... Mpaka leo bado nina majeraha ya dhuluma niliyodhulumiwa mwezi wa 5. Almanusura nilazwe, niliumwa mno...
Duuh pole sana mkuu? Ilikuaje?
 
Nilimfungulia mdogo angu wa damu duka la karibu ml12 baada ya mwaka naenda pale nakuta limefungwa na yeye kakimbia, mpaka leo mwaka 4 hatuongei tukikutana kwenye msiba km hatujuani sana sana yeye ndio ananipiga chenga, nilipo hakai wala haji, alafu hiyo ni biashara ya pili anaiua.
 
Nimelizwa mpaka sasa simuamini mtu yeyote Yule yaani yeyote Kama ni pesa nitatoa lakini Sio kukopesha
Wee kama mimi mkuu,
Watu ninaowadai wakiamua kunilipa hiyo ela naweza kula miaka mitano bila kufanya kazi
 
Nshakua mwema sana mwishowe wanaishia kuniumiza tuu,
Hapa natafuta mganga wa uhakika nianze kuwaloga mmoja baada ya mwingine wawe mashoga haswa.
Hahahahaaaa mkuu nilkuwa na huzuni ya ajali ya meli ila komenti yako imenichekesha balaa. Utaroga mmoja mmoja
 
Kwahiyo ulikwichi kwichi chini??
 
Mimi kuna tajiri bwege wa tanzanite toka mwaka jana mwezi wa 7 kanirusha pesa ndefu,ila bado namlia timing kipindi hiki cha ukuta nitamuuza siku anavusha production yake ndio atazimia nami ntakua nimerudisha pesa yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…