Je, umewahi kutamani kifo chako kiwe cha namna gani?

Jukwaa huru mkuu,
Unaweza kuuliza usiwe na shaka na privacy yangu, nitakujubu yaliyopo ndani ya uwezo wangu.
Karibu
 
Kuna kitu kinaitwa the art of dying ambacho wengi huwa wanakikwepa kwa sababu ya hofu ya kisaikolojia waliyo nayo.
Yes kaka
Kuogopa kuwaza mwisho wa maisha huku unawaza mwanzo na ulipofika kwa muda huo hiyo nayo ni ajabu sana
👏👏👏 kama kawaida yako bro point tupu
Usipokua tayari kuongelea kifo then you are not actually ready to live 📌❤️

Karibu tena The Thinker 😊
 
Hata hapo saivi ukute umelewa

Kuna mdau hapo juu amesema kufia bar ukiwa umelewa ndio kifo kibaya
Huyo mdau labda anataka kufia nyumbani kwa bwana ake. Maana wana mabwana zao skuhizi.

Sisi wengine tulewe mpaka makaburini
 
Ndugu mdau,
binafsi kwa Neema na Baraka za Mungu, natamani kuishi maisha marefu na yenye kheri duniani,
Amen Amen Brother
sifikirii habari ya kufa kabisa, kama ambavyo sikufikiria kuzaliwa.
Acha basi 😁 Enjoy bro
NB kufa ni lazima🐒
In fact,
kwa kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.

na kwa mapenzi ya Mungu ikiwa ataniita, ni imani na matumaini yangu kuwepo kwenye kitabu cha uzima kufurahi pamoja nae kwenye kiti cha enzi cha ufalme.🐒
Amen naona umekuja kama mwana kondoo wa bwana hongera Apostle
 
Wakati huku kwetu ikionekana ni uchuro, katika baadhi ya nchi kama Ghana au baadhi ya jamii za Asia, watu hujiandaa kwa kifo kwa kutengeneza majeneza ya kifahari mapema (fantasy coffins) na kuweka fedha za msiba ili wasiachie familia mzigo wa madeni.
Ukweli ni kwamba, kujiandaa na kifo (kama kuandika urithi au kupanga taratibu za mazishi) ni ishara ya ukomavu wa hali ya juu wa kifikra, ingawa unahitaji ujasiri mkubwa kupingana na mtazamo wa kawaida wa jamii.
 
kuumwa sana, ama kupata accident na kukaa kitandani kwa muda naogopa duuh,,

Nikiwa mzima miaka 70 inanitosha kabisa ikiongezeka ni khery.... Ila 70 inatosha

Ningetamani nichomwe moto kuzikwa kwenye jeneza sitamani kabisa,, kushindiliwa kifusi naogopa duuuh

Kwann nilizaliwa 😓
 
Ahsante sana Madam.
 
Mtu anaewaza kifo chake anakua kavuka level fulani ya ujasiri, sio kitu kibaya ila binafsi naona huyu mtu ana ujasiri fulani ambao si ajabu hiyo energy anaweza ihamisha na kuleta madhara kwa wengine.

Wapo wale wanaopenda kwenda na wengi, yaani yeye siku yake ikifika au akihisi imefika basi asiwe peke yake.

Kuna wa kujitoa muhanga, kuna wale hataki kuacha wapendwa wao kwenye dhiki yeye akiona hatoboi basi anatanguliza na wenae,ndgu au marafiki na mwisho wa siku si ajabu yeye akaogopa kufa na asijiue.

Uliwahi kupata ile story ya wanandoa waamerika?? Walipofika uzee mume aliumwa sana na ikaonekana hatoboi, akamwita mkewe ambae nae tayari ni ajuza akamwambia afate bunduki yake nyumbani, aje ampige shaba awahi ili aepukane na maumivu.

Mke akaona ni kheri waende wote, yaani amchape shaba mume na yeye ajiue na wakakubaliana hivyo.

Siku imefika, mke kweli kaja na mguu wa kuku, huku na huku baada ya maagano kamchapa ya kichwa mume.
Yeye akashindwa kujiua mpaka polisi wanakuja kumkamata.

Acha ibaki kua siri yako mkuu.
 
Wapo sahihi kujiaanda kwa namna hiyo ni vizuri sana
 
kuumwa sana, ama kupata accident na kukaa kitandani kwa muda naogopa duuh,,
Hiii hua mbaya sana
Nikiwa mzima miaka 70 inanitosha kabisa ikiongezeka ni khery.... Ila 70 inatosha
Vizuri sana
Ningetamani nichomwe moto kuzikwa kwenye jeneza sitamani kabisa,, kushindiliwa kifusi naogopa duuuh
Kushindiliwa kifusi unaogopa
So bora moto
anyway kama unaweza waambie ndugu zako
Kwann nilizaliwa 😓
Usijitutie furahia maisha
 
Wapo sahihi kujiaanda kwa namna hiyo ni vizuri sana
Kimsingi, kupanga mambo yako mapema ni kuwajali na kuwapenda wale unaowaacha, hata kama jamii wakati mwingine haielewi uamuzi huo kwa haraka maana wengine huwa wanachelewa kuelewa
 
Mtu anaewaza kifo chake anakua kavuka level fulani ya ujasiri, sio kitu kibaya ila binafsi naona huyu mtu ana ujasiri fulani ambao si ajabu hiyo energy anaweza ihamisha na kuleta madhara kwa wengine
sijui kama itawezekana kubadili huu mtazamo wako

Mf: mimi kwa wanaonijua wanajua moyo wangu ulivyo clean kabisa

siwezi sipendi kuumiza wengine
Wala kushiriki kua sehemu ya mtu yoyote kuumia nakusahihisha kua mawazo yako hayana ukweli wowote

So ningekuomba tu mkuu kama unavyowaza future yako
Basi usiache kuwaza na mwisho wako
Marcostilone ongezea hapa kwa hii hoja ya huyu mdau
Hawa wanaofanya hivi ni wabinafsi wa kutupwa na pengine wana matatizo ya Afya ya akili na msongo wa mawazo
Hii story yako ina funzo lipi
Au inahusiana vipi na hii mada?
 
Kimsingi, kupanga mambo yako mapema ni kuwajali na kuwapenda wale unaowaacha, hata kama jamii wakati mwingine haielewi uamuzi huo kwa haraka maana wengine huwa wanachelewa kuelewa
EXACTLY 💯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…