Je, unajua kuwa Roho huwa ina kawaida ya kutoka tulalapo?

Umbo lingine ndio kama Hilo la ujana na Katu hakuna kuzeeka,kwani Mtume Muhammad rehma na Amani ziwe juu yake ndio alitufahamisha natambua unajua kuna mambo mengine yametafsiriwa vizur na mtukufu WA daraja


Umesema roho itahukumiwa,je itayopata adhabu ni roho pasina mwili au na mwili?
 


Allah anasema sura tusiyoijua, sasa kwanini wewe tayari umeishaijua??

Tuaposema roho itahukumiwa ni sababu yenyewe ndio mbeba taarifa za matendo ya mtu, mfano wa Roho ni kama black box kwenye ndege, na ndio maana mfano muuaji watu wanaweza kumuita mtu mwenye roho mbaya kwasababu ni roho yake ndiyo inabeba taarifa za maovu yake.

Unauliza inayoadhibiwa na kuhukumiwa ni roho na mwili au??, inayohukumiwa na kuadhibiwa ni roho mwili ni kama chombo tu cha kubeba huo mwili na ndio maana Allah kauita huo mwili umbo tusilolijua. Roho ndani ya huo mwili ni sawa na dumu la mafuta ya taa ndani ya nyumba, ukipiga kiberiti dumu ndilo litashika moto na mafuta yakiisha moto utazimika, hapo sasa utaona kwamba mafuta ndio dhambi, dumu ndio roho na nyumba ndio huo mwili tusioujua na moto ndio afhabu ya jehanamu, huo ni mfano tu waila الله يعلم.
 
Yote mnayo jadili hapa myth sio kweli hakuna kitu kama hicho

Huyo ni michezo ya ubongo tu unapokua umelala ndo maana huewezi kumbuka ata siku moja ndoto yako ilivyoanza.


Rejea wavuta bangi wanapo kuwa high. Nao huona hivyo hivyo


Msidangayike.
 
Ntarudi
 
Mkuu naona hapa unachanganya madesa.

Kwanza umeniuliza je imekuwaje Hilo umbo nimeshalijua nilikwambia kutokana na melezo ya Mtume.

Lakini pili, je unajua upi ni msingi WA hiyo Aya ya 56:60?

Msingi WA hiyo ni Aya ya 47 ya Sura hiyo hiyo


"Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?"
57:47

Allah anawazungumzia watu ambao wanaona ni vigumu baada ya kuoza na kubakia mifupa kuwa hataweza kufufuliwa, ndio inakuja hii aya


نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ
Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ
Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
56:60-62

Ukiangalia Aya hii Allah anajaribu kuwaeleza au kuwafahamisha kwamba hata Sisi tukifa au baada ya umauti wetu Kwa uwezo wake hashindwi kuleta viumbe wengine,maana wao walidhani ni vigumu kufufuliwa ndio anazidi kuwaambia kana kwamba sio kufufua Tu Bali hata viumbe wengine anaweza kuwaleta

Na

Amesema hashindwi kuleta kutuumba katika umbo tusilolijua,hapo inaonyesha kwamba ametoa mfano Tu lakini hajasema kuwa tutakuwa katika umbo tusilolijua na akaendelea katika ya 62 Kwa kusema bilashaka tulishajua umbo letu la awali alilotuumbia je ni kipi cha ajabu mpaka hatukumbuki uwezo wake?

Na Mimi kukuuliza wewe je inaadhibiwa roho na mwili au roho peke yake?

Ni kwamba Allah amesema ataujaza Moto WA jahanamu Kwa majini na watu, na hakusema atajaza huo Moto na roho.

Vile vile anaendelea katika Aya nyingine Kwa kusema kuwa kila mwanadamu atakapo kuwa anaungua basi atambadilishia ngozi nyingine ili machungu yaendelee ,na kwanini ngozi?

Kwasababu ngozi ndio organ ambayo inahusika na hisia za maumivu.

Natumaini umepata mwanga kidogo
 
Hii ilinitokea kama mara 2.
 
Fikra za Mtu si zinasababishwa na Brain itself Mkuu
 
Wakati Niko advance niliota niko chuo kikuu fulani....nimemaliza advance kweli nikapangwa hicho chuo[emoji848]
 
Niliposoma uzi wako akili iliwaza de javu nikaona niende kweny quran kusoma hyo aya ya juu yake na inayofwata kisha nikaenda kwenye tafsir ya ibn kathir , hakika quran haijaacha kitu na ni kitabu kisicho na shaka ndani mwake Allah Akbar,
Nimependa kuona comment leo za watu zimekubaliana na hili ila niwakumbushe mwisho wa aya hiyo
"hakika katika hayo bila shaka zipo ishara kwa wanao fikiri"
Na kumalizia dua ni muhimu sana kabla ya kulala , baada ya kukung'uta kitanda hata kama ni kisafi tauri basi dua hii ni muhimu
" In Your Name, O Lord, I lay down my side and in Your Name I raise it up; if You take my soul, have mercy on it, and if You send it back, protect it with that which You protect Your righteous servants.''
 
roho yangu jana nimeota eti nimemnyakua pande la samaki makamu wa rais maana alikua anakula bila kuniita hivi inawezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…