Je, unaweza kurogewa viwakilishi vya starehe?

Sasa mkuu Tunawezaje kupambana na haya mapepo? Kwa mfano pepo la pombe , Ngono na kadhalika?


Na je, Mtu anaweza kulogwa akawa na matumizi mabaya ya pesa? Yaani kila ukipata pesa haikai hata kidogo? Au hilo nalo ni pepo au ni Ukosefu wa nidhamu tu?

Mshana Jr
 
Nitakurejea
 
Sifa za aina Hii Ya Mwanamke Mlango wa nane Mkuu.
Sifa zao Za Njee.
Hawana alama ...mara nyingi ni kitu kilichopo kwenye familia zao ndio maana ni muhimu kufanya background check kabla hujaamua kuoa ama kuanzisha mahusiano
 
Changamoto kubwa ipo kweny kujua chanzo ama asili ya tatizo.. Ni muhimu sana kufahamu msingi wa tatizo na baada ya hapo ndio unaweza sasa kuelekezwa namna ya kutatua
Wengi tunafeli kwakuwa hatutibu chanzo bali matokeo ...na wengi wanadhani matatizo yanafanana hivyo nikitumia njia fulani mwingine naye anadhani akitumia njia hiyo atafanikiwa
.
Pata chanzo ama asili ya tatizo mengine yote ni mepesi
 
Nina bro alifukuzwa shule akiwa form 3 kwa sababu ya pombe. Kila akipata hela inaishia kwenye pombe then akilewa atafanya matukio kama kuiba , ashakaa jela mara kadhaa ila akitoka mwendo ni uleule , dingi kazunguka nae sehemu nyingi adi amekata tamaa, sehemu nyingi wanaambiwa karushiwa pepo ila hamna dawa aliyotumia akapona Mshana Jr
 
Msafisheni kwanza kwa kutumia chumvi ya mabonge kisha mengine ndio yatafuta
 
Nimepata shida kidogo kusoma hii 'chovywa chovywa',nikajaribu kusoma hata kwa sauti pia naona imekuwa ngumu,ingawa nimekuelewa mkuu....
 
Hapo uliposema, "Ni muhimu kujua chanzo cha tatizo." Nimekuelewa vizuri sana mkuu Mshana Jr ,watu wengi tumezoea kuhukumu mtu, jambo au kitu kwasababu za nje tu pasipokutafuta source yake. Kila jambo unaloliona kwenye ulimwengu huu wa mwili halipo kwà bahati mbaya, lazima lina chanzo au sababu zake. Tulio wengi ni vipofu wa rohoni hivyo hatuna uelewa wowote wa mambo ya kiroho.
Ombi langu kwà wadau wa elimu hizi hasa kwà wakuu akina Mshana Jr Pascal Mayalla Rakims MziziMkavu na wengineo wenye uelewa wa mambo haya ya kiroho, wawe wanakazia Sana kwenye mada hizi ili na wengine ambao bado wachanga kiroho tupate kujifunza. Kwani elimu hizi ni adimu Sana huwezi kukuta popote wanafundisha hovyo, na hata wakitokea watu wakufundisha huwa wanashambiliwa Sana kwani wanaharibu biashara za watu. Hao wanaowashambulia na kuwakatisha tamaa waalimu wa hizi elimu wakihofia kuumbuliwa mambo yao.
 
Tulio wengi ni vipofu rohoni hivyo hatuna uelewa wowote wa mambo ya kiroho.[emoji1752][emoji1752][emoji1534][emoji1534][emoji1534][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Ninakubaliana na wewe unavyo sema kam mchawi anataka kukuroga anakuroga kw amaradhi ambayo yanatibika hospitali kw amfano maradhi ya kifua kikuu na maradhi mengine ukienda hospitali kutibiwa lakini huwezi kupona na lengo lake mchawi akutese kimaradhi . Na pepo mchafu anakuingia katika zile starehe unazozipenda kwamfano ukipenda wanawake sanautampata pepo wa wanawake ,ukipenda pombe sana utampata pepo aka shetani wa pombe na kadhalika.
 
[emoji1752][emoji1545]Heri ya mwaka mpya kaka
 
Nashuka Na Visa Viwili
1.Miaka ya 2000+ baba yangu alikuwa mfanyabiashara wa mabasi ya mkoani pamoja na maduka ya jumla akishirikiana na Mdogo wake ambae ni mtoto wa baba ake mkubwa....
Miaka ile biashara hasa ya mabasi ilikuwa inakwenda kishirikina sana sana katika biashara yao akatokea Mtu mmoja wakawa wana ushindani mkubwa sanaa,,miaka hiyo wote baba na baba mdogo walikuwa wanywaji wa pombe sema uwezi wakuta wanakunywa mida ya kazi ila lile bifu na ile ligi ilivokuwa kali nao ulevi uliwazidi wakawa hawapo tena makini na kazi,,walikunywa haswa kama unakumbuka ile miaka Safari lager waliendesha shindano la kushinda kontena,,basi mzee alishinda lile kontena likiwa na bia kreti mia mbili,jenereta,tv nk...ebwana eeh kwa kushirikiana na yule mdogo wake walizinywa ikawa hakuna cha kazi tena jambo la kumshukuru MUNGU mama yetu alikuwa imara sana akaamua simamia biashara zote(wapare wapambanaji sana) bahati mbaya upande wa baba mdogo yeye hakutaka maduka yake mke wake asogelee,,kama mwaka toka wapate lile kontena baba mdogo aifariki gafla tukazika,,wakati ule anafariki mama alikuwa amefanikiwa kununua basi jipya 2by2 kwa wakati ule ni moja ya Luxury bus za mwanzo mwanzo,,basi yule mzee alokuwa wanashindana nae akaanza sambaza maneno kuwa mama ndo kamuua shemeji yake,,kwa bahati hazikufanikiwa,,siku zikaenda mzee akizidi kuwa mlevi haswa,,mama akaenda kwa mtaalamu mmoja akaambiwa baba alilogewa Pombe na ilikuwa lazima anywe hadi afe pia wakadai kuna sijui namna wamefanya hata atakapokufa atakaerithi au msimamizi wa mali ambae angekuwa kaka yetu nae angekuwa mtu wa starehe mpaka auze kila kitu tunashukuru kwa dawa zile mzee aliacha pombe 2008 na hadi leo hagusi na hapendi tunywe basi tu tunakunywa kibishi,,na mwaka huo huo yule mzee alomfanyia hivo mzee alifia gest moja buguruni akiwa na kimada wenye kumbukumbu watakumbuka maana iliripotiwa kwenye magazeti ya udaku(Sijui ni alikufa kwa mapenzi ya Mungu au nao walimfanyia jambo)

2
Kisa cha pili kinatokana ndani ya cha kwanza

Yule baba mdogo alipofariki Mali ziliamuliwa zitakuwa chini ya Mama na Mtoto ake mkubwa wa kiume,,wakati ule mtoto mkubwa alikuwa form 3 hivo akabaki mama anasimamia mpaka yule jamaa alipomaliza masomo yake ya chuo,,akarudi wakati huo Walikuwa wana duka kubwa tu la jumla na reja reja pia walikuwa wanauza vinywaji mshkaji akaanza rasmi kusimamia kama miaka mitatu hivi akawa vizuri sana na maarufu sana ila kwenye 2015 akaanza katabia kaulevi badae akawa mlevi haswaa ndani ya muda mfupi mtaji wa duka ukakata,alifungua baa ikafa,,kwa ufupi kufika 2018 akawa kafirisika,,ndugu tulijitahidi kuna maelekezo tulipewa tukafanye tumpeleke huko ila amegomaga kabisa tumeamua kumuacha,,hadi leo hii anafanya kazi za kidananda tu mara vibarua,mara saidia fundi mara umkute yupo studio za wasanii anawaandikia nyimbo,,mara usikie anaishi na jimama linamlea ila akipata tu hata 10k anaenda lewea yote yani ili asilewe ni asiwe na helaa........

Uchawi/ushirikina mbaya sanaaa


NB:mimi sio mzuri sana kuandika visa ila enzi zile za mpambano wa barabarani nilishuhudia mengi ya ajabu na ni kisa cha kusisimua siku nikipata mwandishi mzuri au kama Mshana Jr utakuwa tayari nikusimulie ukiandike ili wasioamino waamini ila yote kwa yote HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA MUNGU

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
NB:mimi sio mzuri sana kuandika visa ila enzi zile za mpambano wa barabarani nilishuhudia mengi ya ajabu na ni kisa cha kusisimua siku nikipata mwandishi mzuri au kama Mshana Jr utakuwa tayari nikusimulie ukiandike ili wasioamino waamini ila yote kwa yote HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA MUNGU[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Simulizi zako zimenisisimua sana ...tuwasiliane kwa ajili ya hiyo story nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…