Nimesoma historia yake, kwa kweli inatisha. Sikujua kama alikuwa mtu katili wa kiwango cha juu kiasi hicho dhidi ya wananchi wake.
Kuna wakati Mungu hutenda kwaajili ya kuwaokoa watu ambao kama kiongozi kuishi, wangeteketea wengi. Huyu bwana alikuwa ni mkono wa chuma ambao haukuthamini uhai wa Wairan wengine, hasa wenye kuthubutu kumkosoa. Maandamano ya akina mama yalishuhudia mauaji ya watu zaidi ya 500. Lakini pia kabla yake alitoa idhini ya mauaji ya wafunfwa zaidi ya 5,000 na majani 6!! Leo naye amewafuata aliowatanguliza.
Uwe kiongozi, uwe tajiri, uwe msomi au maarufu kiasi gani, juu yako kuna mamlaka iliyo juu zaidi kuliko kiumbe chochote. Yawezekana kuna watu wenye ujuzi na uwezo mkubwa, walimtafuta, lakini wote walishindwa. Ila kwenye muda ulio sahihi, Mungu ametimiza mapenzi yake kwa namna aliyoitaka.