Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Mkandara...

Umesema mambo muhimu sana kwenye hili.

a. Kuna suala la jamii ya watu fulani kufanikiwa ambalo kwa watu wengine wanaonekana ni kubebana au kupendeleana. Si kwa sababu watu wanajiona ni bora bali ni kwa sababu kama jamii ya watu wamepiga hatua sana, yawezekana kwa kazi zao na kujituma na kuhangaika na sasa wanakula matunda ya jasho lao. Je tuwakataze kwa sababu wamefanikiwa?

Wayahudi wa Ulaya walikuwa wanalaumiwa sana katika karne nyingi kuwa ni wabahili na wanapeana misaada wao wenyewe na kufanikiwa. Kila mahali wayahudi walipokwenda walifanikiwa kama jamii (haina maana wayahudi wote walifanikiwa). Walikuwepo Ujerumani wamefanikiwa, wamekuja Marekani wamefanikiwa sana n.k Tunajiuliza kwanini? Mtu wa haraka haraka atasema kwa sababu wanapendeleana au wanabebwa. Lakini kuna sababu kubwa zaidi ya hiyo. Hakuna kitu kama hofu ya kutokuwepo. Jamii ya Wayahudi katika historia yake yote wamekuwa wakiishi na hii hofu ya kufutwa katika ulimwengu. Na zaidi ya yote lile suala la kutokuwa na mahali unaweza kupaita kwako.

Kwa upande wa jamii ya Wachagga tofauti na ya Wahaya na Wanyakyusa, wao mafanikio yao ya kiuchumi yanaendana kwa namna mmoja na hili suala la uwepo. Katika nchi yetu hakuna mahali ambapo kuna ugumu wa kupata ardhi mpya kama Kilimanjaro. Kama huna ardhi kilimanjaro, ardhi ambayo imepitishwa toka kwa wazazi wako ni vigumu sana kupata ardhi mpya. Ni hili tatizo la ardhi kwanza kabisa lililowasukuma wachagga wengi kuondoka Kilimanjaro na kwenda kuchangamkia tenda maeneo mengine. Tofauti na mikoa ambayo watu wake wana ardhi ya kutosha na hivyo wanaitegemea, Wachagga hawategemei ardhi yao isipokuwa utajiri ambao mwenyezi kawapa wao na sisi, yaani Ubongo.

Ni hili la kutokuwa na mahali pa kuendeleza Ardhi ndiyo kimekuwa chanzo cha wao kufanikiwa. Kama Wayahudi wao pia wanajikuta wanalazimika kufanya kila kitu kwa jitihada zaidi kwani wasipofanya hivyo watoto na watoto wa watoto wao wataishi wapi na vipi. Wengi wetu hapa kikiungua mjini tuna rudi kijijini kwetu, tuna uwezo wa kwenda kwenye maeneo ya nasaba zetu na kumegewa kipande cha ardhi toka shamba la babu, Wachagga hilo ni ngumu kweli kweli.

Hivyo, hili lilionekana tangu zamani. Wachagga walianza kuondoka Kilimanjaro na kwenda miji mingine mapema sana baada ya suala la ardhi kuanza kuonekana. Huku walikokwenda walikuwa wafanye nini, wengi walijiingiza kwenye biashara, wamekuwa na haraka sana ya kuchangamkia nafasi ya biashara. Hasa kupeleka kwa watu ambao ni jamii ya wakulima au wafugaji au jamii ya wavuvi. Wachagga wakawa wanaleta huduma na bidhaa zinazohitajika kwa jamii hizo.

Hili linalingana na Wayahudi vile vile, kwamba Wayahudi walikokwenda wamejiingiza kwenye sekta ya biashara katika kutoa huduma, miaka ya mwanzoni kama kule Ujerumani walijiingiza kwenye mambo ya kibenki, na hata walipokuja Marekani walichangamkia huduma za kibenki na mambo ya fedha. Walifanya hivyo wakijua kwamba jamii mpya ya Kimarekani inahitaji utaalamu katika sekta hizo, utaalamu ambao wao Wayahudi wamekuwa wakiutumia kwa karne nyingi. Wakafanikiwa katika biashara.

Sasa hivi sitoshangaa jamii ya Wachagga siyo tu wanaenda kwenye huduma za vitu muhimu, wataanza muda si mrefu kuingia katika mambo ya burudani (kama bado hawajaanza). This is a natural progression.

Nitaachana na wachagga na wayahudi kwa sekunde. Hapa Detroit kuna eneo linaitwa Dearborn. Eneo hili ndilo linamkusanyiko wa waarabu wengi zaidi kuliko eneo jingine lolote nje ya Mashariki ya Kati. Wengi wa waarabu waliokuja hapa walikuja kutokana na mabadiliko ya kisiasa ya Mashariki ya Kati miaka ya sabini na themanini na wale ambao walihamia huku miaka ya ugunduzi wa mafuta.

Waarabu (na hapa nazungumzia waarabu na wakaldeani) walipokuja hapa, kama jamii wakaanza kupeana huduma wao wenyewe. Biashara yao ya ndani na kusaidiana kupeana mikopo nje ya mfumo wa kawaida wa mikopo. Wafanyabiashara wa kiarabu wakiwa wameunganishwa na hasa na dini (Uislamu) wakaweza kuanza kujikita katika kutoa huduma. Walichokifanya ni kile kile kilichofanywa na Wayahudi, na kilichofanywa na Wachagga; wakaingia katika jamii ya watu weusi na wakaanza kufungua maduka ya huduma za haraka haraka (convenient stores) hasa baada ya maduka makubwa kama Farmer Jack, Meijers, na Kroger kufunga malango yao Detroit. Leo hii ukija Detroit, usishangazwe kukuta duka la mwarabu karibu kila baada ya mtaa.

Wanatoa huduma ile ambayo wanajua kuwa watu wa Detroit wanaihitaji. Na hapa napo kuna sentiments dhidi ya waarabu kwa sababu imekuwaje waje muda mfupi ulipita na wafanikiwe kiasi hicho. Utashangaa kuona kuwa waarabu wanashirikiana sana katika kufungua vituo vya mafuto, au maduka haya. Watu weusi hawawezi kukaa chini na kushirikiana kufanya biashara pamoja bila kushukiana (at least kwa mtazamo wangu na ni kuhusu baadhi yao). Jiji la Detroit ni asilimia 80 watu weusi, lakini ukija kwenye biashara za maduka haya karibu asilimia tisini yanamilikiwa na waarabu. Na cha kuchekesha ni kuwa wengi ya hawa waarabu hawatothubutu kuona mtoto wao wa kike anamdate mtoto wa mweusi!

Lakini na wao kinachowasukuma ni kile kile, siyo tu tamaa ya fedha (kama inavyohusishwa kwa wayahudi na wachagga japo waarabu hapa wanaonekana wana tamaa sana ya pesa) ni ile haja ya wao kuendelea kuwepo kama jamii ya watu na hasa wakijua ni nini walikiacha kule Iraq, na maeneo mengine ya mashariki ya Kati.

Hivyo basi utaona kuwa tatizo tunalolizungumzia ni suala la kijamii zaidi ambalo lina maelezo ya kisayansi lakini kwa vile baadhi ya watu hawataki kuliangalia kisayansi wanataka kutafuta sababu za kugeresha.

Tatizo kubwa ambalo ninaliona ni pale jamii hizi wayahudi, wachagga, na waarabu wanapoanza kuishi kana kwamba wao ni zawadi ya Mungu kwa wanadamu, na ya kuwa wao ndio "Taifa Teule". Ni hisia hizi za kujiona bora ndizo wakati mwingine zinasababisha hiyo resentment. Kufaninkiwa kwa jamii hizi kunaelezeka intellectually, na haihitaji divine providence kuelezea.

Hivyo ukweli huu wa kufanikiwa namna hii unaweza kupata watu wowote na mark my words ndio utakaofuel mafanikio ya Rwanda pia.
 
Kungurumweupe said:
Nashukru kwa kutuletea huu mjadala. Ni ukweli ulio wazi kwamba watu kutoka makabila mengi hapa nchini hawawapendi wenzao wa kabila la kichaga.

Sababu kubwa na ya pekee wanayodai ni kwamba, wachaga waliweza kusoma na kuendelea kutokana na pesa waliyokuwa wakipata wakati ule vyama vya ushirika vilikuwa vinapata RUZUKU kutoka SERIKALINI. Ruzuku hiyo ilitokana na pesa za serikali ambazo hasa zilitokana na aidha MASHIRIKA YA UMMA au KODI za watanzania waliokuwa wanalipa KODI YA KICHWA au KODI WALIYOKUWA WANAKATWA KWENYE MISHAHARA YAO WAKIWA WAFANYAKAZI WA HAYO MASHIRIKA YA UMMA.

Nikutokana na hiyo elimu waliyoipata katika mazingira hayo, makabila mengi yanadai kuwa, wachaga waliweza kunyakua kazi zile zenye kipato cha juu na hasa serikalini na kwenye mashirika ya umma. Huko serikalini na kwenye mashirika ya umma, Wachaga waliweza kunyakua nafasi kubwa kubwa na za kiutawala ambazo ziliwawezesha KUWAVUTA WATOTO WA WAJOMBA NA SHANGAZI ZAO nao wakapewa nafazi za upendeleo zenye ulaji.

Kwa mfano, makabila mengi yanadai kwamba, wachaga waliweza kuingiza watoto wao wengi kwenye jeshi la polisi ati kwa vile tu chuo cha jeshi hilo la polisi kilijengwa nyumbani kwao moshi. Nia na sababu kubwa ni kuwa na access na silaha yaani bunduki ambazo wangeweza kuzitumia wapendavyo!

Haya ni madai ya watu wengi niliowahi kukumbana nao katika mijadala mbalili mbali hasa mashuleni, vyuo vyetu vya hapa nchini na katika vikao vya kijamii na hata kwenye mikutano ya kidini, japo mimi binafsi sidhani kama yana ukweli asilimia 100.

Kungurumweupe,

..kwanza vyama vya ushirika vilikuwa na nguvu ya kiuchumi na financially independent. si kweli kwamba serikali ilikuwa ikivigawia ruzuku.

..serikali kwa kuvionea gele iliamua kuvivunja vyama vya ushirika na kuanzisha mamlaka ya mazao[mamlaka ya kahawa,pamba,...]

..pia serikali ilitaifisha mali nyingi za vyama vya ushirika kama viwanda, vyuo,mashule,mabenki,etc etc. Benki ya CRDB ilikuwa mali ya chama cha ushirika.

..lakini vyama vya ushirika vilikuwepo pia Mwanza,Kagera, na maeneo mengine. sasa kwanini Wachaga peke yao wachukiwe kwa maendeleo waliyoyapata kutokana na vyama vya ushirika? au vyama vya ushirika Kagera,Mwanza, na kwingineko, vilikuwa havipati "ruzuku"

..tangu kuvunjwa kwa vyama vya ushirika maendeleo yamedorora ktk maeneo mengi ya Kilimanjaro.

..kuna article niliisoma kuhusu Mangi Marealle kuhimiza vijana WASOMI wa Kichaga kujiunga na jeshi la POLISI. hata JWTZ kuna maofisa wengi tu wasomi wa Kichaga. msisitizo hapo uwe WASOMI/ELIMU.

..pamoja na hayo, Wachaga do not make the majority of the rectruits in the army or police force.

..pia nashangaa kwamba wananchi wanalalamika zaidi pale wanapohisi Wachaga wamezidi katika taasisi fulani.

..uwingi wa wenyeji wa Musoma ktk majeshi ya ulinzi na usalama ni jambo la wazi kabisa. lakini wananchi wameamua kulifumbia macho na badala yake kuwashutumu Wachaga walioko ktk taasisi nyingine za serikali.

..naomba Watanzania mtafute interview ya Raisi Kagame na kuzingatia majibu yake kuhusu kilichopelekea Wahutu kuwaua Watutsi. kitu cha kushangaza kabisa ni kwamba ktk Chuo Kikuu chao, wanafunzi 500 kati ya 2000 walipoteza maisha.

..Kagame alieleza kwamba hizi tuhuma za ukabila zikiendekezwa sana zinaweza kumteka akili/mawazo mtu yeyote yule hata wasomi tunaowategemea.
 
JokaKuu.. tatizo la mambo ya Ukabila ni kuwa it is not rational. Mtu mwenye kuona ukabila anaitikia jambo hilo kwa hisia na vionjo na siyo kwa akili, kwani ukimuuliza onesha ukabila yeye atakuonesha namba. kama vile mtu mwenye udini akatavyoonesha namba. Wote wawili mkabila na mdini hawaangalii hoja za kiakili kwani wanaitikia kivionjo na hisia.

Ukiangalia humu utaona jinsi gani watu kwa mbali wanavumbi vumbi la ukabila dhidi ya Wachagga, si kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa wivu wa kwanini wao wamefanikiwa kuliko watu wengine.

Ni kwa sababu hiyo mimi naamini mtu wa hatari sana kwenye suala hili sasa hivi atasikika Bungeni siku moja akimwaga sumu yake ya ukabila.
 
Mwanakijiji,

Binafsi nimesema sintapenda kabisa kuingia ktk mada hii na kutoa hoja yangu.. isipokuwa nitazungumza kwa fikra huru ambazo zinalitazama swala zima ktk mapana yake bila kuweka wahusika.
Huo mfano wa Wayahudi hauwezi kubeba mzigo wa wachagga.. hizi ni kesi mbili tofauti kwani Myahudi alikuwa akishika Ulaya nzima kabla ya Hitler.. Ni ukweli usiopingika. Ndio maana hata rais wa Iran alisema ikiwa Wayahudi waliteswa na Hitler why mliwapeleka Palestine hali kulikuwa na sehemu nyingi Ulaya ambazo zingeweza kuwaweka!.. Why kuwapeleka mbali ni nchi walizozaliwa,.Myahudi wa Ulaya ni Mpolish, Mrusi, Mfaransa, Muingereza na kadhalika why unawapeleka watu wa makabila tofauti sehemu moja kwa sababu ya dini yao..What about wale walioishi pale na wakabadilisha dini kuwa waislaam ama wakristu lakini bado ni kabila la sehemu hiyo! hawa kweli hawana haki na nchi ile?
Ni swali ambalo hadi leo halina jibu hata kidogo na pengine Mungu anatuonyesha yanayotokea leo huko Palestina kwa nini Wazungu waliwatenga Wayahudi na kuwapeleka Palestina....wanajua madudu yao vizuri. Hawa watu wanafikiria kuwa wao ni SUPERIOR human being na vitabu vitakatifu vyetu wenyewe tunavyosoma vinasema hivyo!..Then unategemea kweli kuna usawa hapa ya kwamba Myahudi ndiye anaye onewa!.. Mimi nadhani kinachotakiwa kuzungumzwa ni mauaji ya Hitler kuwa ya kinyama na Wayahudi walikuwa victims tu ktk matendo yale lakini hiyo haiwezi kuwasafisha mabaya yao..Sawa kabisa mna Mtusi ambaye kwa karne nzima alikuwa akiwatenga Wahutu, kuwanyanyasa na kuwanyima haki zao za msingi dunia ilikuwa kimyaaaa, siku dau lilipo geuka Mtusi kuwa victim dunia nzima ilipiga kelele..Hakika binafsi nalaani tu ile genocide besides that sidhani kama mtusi ni mtu mzuri. Ninalaani Makaburu kwa yote waliyoyafanya miaka yote na leo hii nitalaani vitendi vya Mugabe dhidi yao (Makaburu) lakini siwezi kuondoa fikra kwamba Kaburu ni mshenzi!
Wote hawa mkuu wanadai kwamba utajiri wao ana nguvu zao ni matunda ya kile walichopanda..mafanikio yao yametokana na jitihada zao ktk kujituma na kwamba makabila mengine yanawaonea wivu.. Kitu wanachosahau kutenganisha ni kwamba huwezi kwenda pandikiza mbegu ktk shamba la mwenzako hata siku moja! Ukaja dai mafanikio kuwa ni yako wewe..Malalamiko ya watu wengi ni ktk kutazama uhalali wa nguvu zako ktk shamba lake.

Hii habari ya wivu na kadhalika ndio lugha za viongozi wetu kina Lowassa, Mkapa na wengine ambao Utajiri wao umetokana na matumizi mabaya ya shamba la wananchi... hivyo mali inayopatikana siii halali ya kwao.
Ni lugha ya kila mtu mshenzi ambayo naomba sana tena kwa kutoa tahadhali Wachagga wasitake kuitumia. Lugha hii inabomoa haijengi!
 
Mwanakijiji,
Mkuu mimi nashindwa kabisa kuchangia mada hii kwa sababu pande zote mbili mnashindwa kunipa darasa...Yaani hakika mada hii inachusha sana na haitakiwi kabisa kuendelea.
Mfano huko nyuma umenambia kuwa kuna tofauti ya Mzungu na Mchagga ni swala la Ugeni, lakini mkuu kwa uhakika nani aliyepanga mipaka hii haswa ikiwa kuna swala la Uraia. Mapoambano ya Uhuru hayakuwa kuhusiana na Utawala tu hata Wazungu wenyewe walikuwa ni adui iwe Kaburu ambaye hakuwa mgeni huko South ama Utawala wa Malkia, Mjarumani, mwarabu au Mreno.
Kwa mfano wa ugeni na kutawala kwa nguvu, hata huyo Mchagga anapokuwa Mwanza ni mgeni vile vile akinyimwa haki fulani kwa sababu ni mchagga basi bila shaka tutasema Wasukuma wametumia Ukabila ktk kum profile huyo jamaa au sio. Na Mchagga akitumia Ubabe wake ndani ya Wasukuma kwa sababu ni Mchagga hapa lugha itakuwa bado ni Ukabila... sioni mipaka ya ugeni au mwenyeji..
Mazungumzo yote humu ukiyageuza kidogo tu kuondoa mchagga ukaweka mzungu ama Mhindi watu watakuwa na hukumu tofauti hata kama mzungu/mhindi huyo ni Mtanzania. Watakao tetea upande huo nina hakika ni wale wenye ukaribu na Wazungu/wahindi..kama vile wachagga wanavyofanya hapa.
Na kibaya zaidi ni kwamba wale wanaotetea Wachagga wanazunguza lugha ya mkoloni, lugha ya Makaburu ambao waliyasema hayahaya kwamba kuwepo kwao Afrika ndiko kumeleta Ustaarabu na maendeleo yaani wengine sisi kina Yakhe ni wanyama, wavivu na kadhalika..
Inashangaza sana kuona mwafrika akimwita mwafrika mwingine kwa majina hayo kisha anaendelea kudai kuwa hakuna Ukabila na hata kudiriki kuwaita watu wa makabila mengine wana inferiority complex... Kwa nini isiwe Wachagga wanajiona wao ni superior kuliko makabila mengine?... Jamani jamamni Ukabila ni sisi wenyewe hizi lugha mnazozitumia ndio zinajenga Ukabila.
Wala sio swala la kupeleka mali zetu nje ndio kilichotufanya sisi waafrika tupiganie Uhuru wetu. Makaburu tayari walikwisha fukuzwa huko Holland wakatupwa South na wengine Australia. Hawa watu walikuwa wabaguzi hawakutawala kwa nguvu isipokuwa utawala wa malkia ambao kama unakumbuka kina Smith, Botha na hata Zanzibar ulitangazwa Uhuru ambao bado ulijengwa kwa matabaka..
Ni pale binadamu mmoja anapojiona yeye Superior kuliko wengine ndipo Ukabila unapotumika ktk matendo yetu. Ukabila siku zote ni yule mwenye nguvu (Power) mwenye uwezo wa kupanga na kuamrisha sera ambazo hazina haki kutumika iwe kimaandishi ama kwa vitendo tu. Mnyoinge asiyekuwa na uwezo huo ambaye ktk Mada hii mnamwita ana inferiority ni mpambanaji mtu asiyekubali kuonewa na anapoyataja mabaya ya huyo mwqenye nguvu ni jukumu letu sisi Watanzania kuyasikia malalamiko hayo na kuyatafutia ufumbuzi.. Mkuu Vita ya Rwanda ilianza hivi hivi taratibu na propaganda ambazo kwa wale mnaowaita wenye elimu duni zilianza ku sink in. Wakayatazama matendo ya Watusi dhidi yao wakaziona tofauti ktk ajira, ktk utawala, ktk urafiki wao na kadhalika...Hapakuwepo mgeni pale wala mtu anayechukua mali na kupeleka nje!.. Ni swala la ndani...
Kwa hiyo jamani acheni kabisa hizi habari za Wachagga na watu wa makabila mengine. Ni propaganda chafu sana, na laukama kuna ukweli fulani basi nawaombeni hao Wachagga msijione Miungu watu hata kidogo wala msifikirie hii ni fun thing to talk about!.. Inaonyesha wazi jinsi mnavyowaona binadamu wengine kama walivyofanya Makaburu huko South, lugha ya dharau na kujitanua kifikra kwa sababu tu ya elimu ya kuiga!...Waswahil wanasema kutangulia sio kufika wala mjanja sio kuwahi ila ni Kupata!...
Mkianza na matusi madogo yenye imani kama hizi baadaye itakuja fuata vitendo, Mchagga ataanza kujitenga na kujiona mbora zaidi, ili kufanya hivyo itabidi ajenge ngome zake ambazo ndizo zitakuwa chanzo cha Ugonvi mkubwa..

Mkandara,
Ninakubaliana na maelezo yako kwa asilimia kubwa,lakini hicho anachofanya mwanakijiji,kitafanya hayo makabila yazidi kuziba mianya kwa wengine ili kuunyesha kuwa si lolote si chochote.Ombi je hii mada inaweza kufungwa??? kwa mawazo yangu inazidi kuchochea chuki zaidi kuliko kutatua tatizo!
 
Tuipendenchiyetu, tunaweza kujificha na kukwepa kuzungumzia tatizo na kuweka vichwa vyetu mchangani kama mbuni au tunaweza kukaa chini na kusema wana ndugu tatizo liko wapi. Tukiogopa kuzungumzia mambo haya siku moja yakifumuka tutashindwa pa kuanzia. Wakenya kwa muda mrefu hawakuwa tayari kukiri hadharani ukabila wao hadi hivi majuzi lilipofumuka. Binafsi sitoshtushwa siku moja mtu akifanya jambo dhidi ya mchagga/ au wachagga solely kwa sababu ya kabila lake kwani mbegu hii ya chuki dhidi ya wachagga inakua taratibu kati yetu na watu wanaogopa kuionyeshea kidole.
 
Mwanakijiji,
Hapana isifungwe kabisa kwani haya tunayoandika sasa hivi yasingweza kuonekana kama ingekuiwa imefungwa na mawazo ya watu wengi bado yangekuwa akilini mwao.
Mimi nasoma hizi hoja humu ndani na tutagusia hapa na pale kila inapohitajika.
Kinachonisikitisha tu ni pale Wachagga wanapokuja hapa na kuonyesha wazi kuwa wao wanajiona superior... hii inatisha sana. Tujaribu kufikiria kwanza kabla hatuajaandika kitu maanake huu mjadala unawakilisha makabila 120 +
Hapendeewi mtu hapa..
 
Mwanakijiji,
Hapana isifungwe kabisa kwani haya tunayoandika sasa hivi yasingweza kuonekana kama ingekuiwa imefungwa na mawazo ya watu wengi bado yangekuwa akilini mwao.
Mimi nasoma hizi hoja humu ndani na tutagusia hapa na pale kila inapohitajika.
Kinachonisikitisha tu ni pale Wachagga wanapokuja hapa na kuonyesha wazi kuwa wao wanajiona superior... hii inatisha sana. Tujaribu kufikiria kwanza kabla hatuajaandika kitu maanake huu mjadala unawakilisha makabila 120 +
Hapendeewi mtu hapa..

WE DARE TO TALK OPENLY IN JF. Hakifichwi kitu vyote ukweli na uongo vina nafasi.
 
Duuh. kweli mmenipa wazo raha. ila mwanakijiji unafikiri sana. \wote wanaolia naweza toa konklusheni WIVU TUU HAMNA JINGINE. hii ni impact ya nyenyere na Mkapa Mungu wasamehe.
wachaga tusonge mbele
 
Mkandara, upande mwingine wa hoja ambao hatujaugusa na si suala la wachagga tu bali kuna watu (kama siyo makabila yote kwa kweli) ambayo yanaamini kwa namna fulani wao wamebarikiwa zaidi na wanastahili zaidi. Wakati mwingine ni sentiments hizi ndizo zinarudisha nyuma yake resentment dhidi yao.

Kuna makabila ambayo watu wake hujinyanyua kama walio bora zaidi na wanaopenda kujitamba hata kwa kitu cha kijinga. Lakini hilo la kuweka fahari ndani ya watoto wetu msingi wake uwe katika kutukuza ubinadamu wetu wote. Inapotokea watu wa kabila fulani wanajinyanyua kana kwamba wao ni "special" utaona majibu ni kuwa wanachukiwa.
 
lakini at least hii mada imeweza kuonyesha jamii kwa kiasi fulani imesimama katika upande gani kuhusiananahili la ukabila.unajua kuna wakati nilikua nawashangaa wakenya sana kwa jinsi walivyojikita kwenyeukabila,kumbe na hapa kwetu hiyo spirit ipo sana ila ni dormant tu
 
Duuh. kweli mmenipa wazo raha. ila mwanakijiji unafikiri sana. \wote wanaolia naweza toa konklusheni WIVU TUU HAMNA JINGINE. hii ni impact ya nyenyere na Mkapa Mungu wasamehe.
wachaga tusonge mbele

mkuu,
sasa hizi conclussion za aina hii ndizo wengine watachukulia light,wengine ndio watakomaa nazo ili mradi tu hapatoshi
 
[QUOTE=Mzee Mwanakijiji;241891]Sipendi... umeuliza kitu muhimu. Yoyote anayefikiria kuwaondoa wachagga katika kufanikiwa atakuwa na kazi kubwa sana. Badala ya watu kukaa chini na kuona wivu dhidi ya Wachagga hatuna budi kujiuliza kwanini wao wamefanikiwa na ni nini wengine tunaweza kufanya kufanikiwa.

Wachagga siyo chanzo cha matatizo ya Tanzania. Chuki dhidi yao inaonesha zaidi jinsi gani wengine tunavyojiona duni.[/QUOTE]


Wachagga siyo chanzo cha matatizo yetu. Na pia hata wahindi siyo chanzo cha matatizo yetu. Lakini pia tatizo siyo WIVU wa makabila mengine. Tatizo ni kanuni zetu za uongozi ambazo zinatoa nafasi kwa watu kujipendelea. Na hapo inaleta chuki kwa watu hasa watu wa kabila au jamii nyingine inapopata uwakilishi mkubwa kwenye taasisi za umma ambazo ndizo zina jukumu la kugawa keki ya taifa. Kwa sababu kama ni wivu mbona watu hawawaonei wivu wakinga ambao na wao ni wajasiriamali na wachapakazi wa kutupwa? Lazima taasisi za umma ziweke mfumo mzuri wa utawala ikiwemo kutoa mamlaka katika mikoa kupanga mambo yao ya maendeleo kama elimu, afya, maji na biashara. Na pia mikoa iachwe kujifunza kutoka kwa mikoa mingine ambayo inakuwa inafanya vizuri katika sekta fulani. Ukiweka hii dhana ya utawala wa makao makuu (Serikali Kuu) kuamua kila kitu siku zote tutatpata shida maana ni lazima kuna kabila au jamii ambayo itakuwa overrepresented. Kwa mwanakijiji tuache kusimplify mambo, hizi sentiments against wachagga zipo na si kwa sababu ya wivu bali kwa sababu ya mfumo mbovu wa utawala. Kitu kingine siyo vizuri kusema kuwa kuna kabila ambalo ni wavivu na kabila ambalo si wavivu hata wazungu wakati wa ukoloni na wakati wa ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini walitumia maneno hayo hayo. Walisema waafrika hawajaenda shule, wavivu na hawafikirii. Kitu ambacho si kweli maana sijaona Tanzania nzima wakitegemea chakula kutoka Kilimanjaro tu ambako watu wana bidii na wanalima. Kila sehemu katika nchi hii watu wanaweka juhudi kutokana na teknolojia waliyokuwa nayo na wanazalisha wanachoweza. Malalamiko kwa wachagga ni kwa sababu watu wanaona kunaoverrepresentation basi.
 
Mkodoleaji hivi wewe unafikiri watu hawawaoni wivu Wakinga? Nenda Mbeya utashangaa... tena wao wanadaiwa kupata utajiri wao kwa njia mbaya kweli...
 
Mkodoleaji hivi wewe unafikiri watu hawawaoni wivu Wakinga? Nenda Mbeya utashangaa... tena wao wanadaiwa kupata utajiri wao kwa njia mbaya kweli...

Kwa hiyo tuseme Mwanakijiji kuwa watanzania wamejaa WIVU wanawaonea wote waliofanikiwa yaani wachagga, wakinga, wahindi na wengineo? Kama ni hivyo basi badilisha kichwa cha maada.

Mimi nilijaribu kukupa sababu za kitaasisi ambazo zinaweza kuchangia hali hiyo sasa kama itakuwa kwamba wanawaonea wivu wote waliofanikiwa kama wakinga na wahindi basi nadhani hapo tutahitaji sababu za kijamii na kisaikolojia zaidi.
 
Mkodoleaji... we angalia tu... kwanini hakuna hizi sentiments dhidi ya wasegeju, dhidi ya Wazaramo, Wazigua, au Wamatengo?... kuna sababu na baadhi ya hizo sababu msingi wake ni wa mambo ya kijamii zaidi...
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini.



Vumbi la mambo yote ya kibaguzi husababishwa na UMASKINI wa hoja. Kichwani sifuri kabisa. Uwe ubaguzi wa kikabila, rangi, jinsia au aina yoyote ile, CHIMBUKO ni MUFILISI wa hoja tu. Sasa huu mufilisi wa hoja unakujaje? Ufisadi is one. Just angalia vituko vya yule Wangwe wa CHADEMA: I am avoiding kuandika, ...yule mkurya wa CHADEMA. It is very easy to use such accolades, but then one has to be VERY THICK indeed to remain with such shallow generalizations.
My hat off to MKJJ! Its a nice piece. What lies behind the word is really impressive
 
MKJJ mimi sijui historia vizuri lakini kipindi kulikuwa na sentiments kama hizi kwa kiasi kikubwa kwa wahaya na hata wanyakyusa. Lakini kwa kiwango kikubwa kwa haya makabila zimeshuka sana. Kwa wachagga zimeongezeka ni kwa sababu hapo awali wahaya na wanyakyusa walikuwa wengi tu kwenye mashirika ya umma. Kwa sasa nafasi yao imechukuliwa na wachagga na hapo ndiyo sababu sentiments nyingi zimehamia kwao. Watu wengine wanaoshambuliwa ni wahindi na wao ni kwa sababu wamekuwa wakionekana na watu wengi kuwa ni kundi linalojinufaisha na keki ya nchi kwa kupitia viongozi wa umma. Kwa hiyo hutapata hizo sentiments kwa wasegeju na wengineo kwa sababu hawaonekani kunufaika zaidi kuliko makabila/jamii nyingine nchini kwenye keki ya taifa.
 
Naomba niwape story kidogo (with a light touch).

Baada tu ya kupata uhuru, idadi ya wasomi ilikuwa ndogo sana na wasomi wa kike hao ndio usiseme. Waziri Mkuu, Mwalimu Julius K Nyerere alikuwa na "choice" ndogo sana katika kuteua watu wa kushika uongozi kwenye idara mbalimbali za serikali. Jimbo la Kaskazini ndilo lililoongoza katika idadi kubwa ya wasomi na hasa wale wa kike. Hali hii ilisababisha wengi wa walioteuliwa kutoka majimbo mengine kujitafutia ujiko kutoka jimbo la kaskazini ili kupata ujiko msomi. Na hata walio waliokwisha pata ujiko mapema walijikuta wakiwa"dump" wenzi wao wa kijijini na kutwaa ujiko msomi kutoka Kilimanjaro.

Hii hali ilizua manung'uniko kwa ndugu na jamaa wa hao ma"graduates" kwani walipoanza kupofushwa na manjonjo ya wasomi wakasahau walikotoka. Hii lilileta hali ya kutooaminiana na chuki dhidi ya wakwe kwani mara nyingi maendeleo yalihamia kwa wakwe wa jimbo la kaskazini. Idadi ya waliojikuta kwenye mtego huu ilifikia kilele kwenye miaka ya sitini na sabini. Usemi wa nyakati hizo ulikuwa "mwanao akioa uchagani, basi umeula wa chuya".
 
Tukiuliza maswali yafuatayo hapa, utashangaa majibu yake ambayo ni imani za watu (hakuna takwimu za kisayansi kuthibitisha imani hizo - oxymoronic?)

a. Ni kabila gani linapenda fedha zaidi Tanzania?
b. Ni Kabila gani linapenda kujitukuza zaidi?
c. Ni Kabila gani linapenda ufuska?
d. Ni kabila gani wanapenda kujinyonga?
e. Ni Kabila gani hawapendi kufanya kazi ngumu?
f. Ni kabila gani wanapenda kupiga wake zao?
g. Ni kabila gani wanapenda kuficha hela zao na hawataki kuziweka benki?
h. Ni Kabila gani wana dharau sana na wanyanyasasi wa wafanyakazi wao?

Nawahakikihishia nikipiga kura ya siri.. karibu asilimia 70 majibu yenu yatafanana!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom