Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #301
Mkandara...
Umesema mambo muhimu sana kwenye hili.
a. Kuna suala la jamii ya watu fulani kufanikiwa ambalo kwa watu wengine wanaonekana ni kubebana au kupendeleana. Si kwa sababu watu wanajiona ni bora bali ni kwa sababu kama jamii ya watu wamepiga hatua sana, yawezekana kwa kazi zao na kujituma na kuhangaika na sasa wanakula matunda ya jasho lao. Je tuwakataze kwa sababu wamefanikiwa?
Wayahudi wa Ulaya walikuwa wanalaumiwa sana katika karne nyingi kuwa ni wabahili na wanapeana misaada wao wenyewe na kufanikiwa. Kila mahali wayahudi walipokwenda walifanikiwa kama jamii (haina maana wayahudi wote walifanikiwa). Walikuwepo Ujerumani wamefanikiwa, wamekuja Marekani wamefanikiwa sana n.k Tunajiuliza kwanini? Mtu wa haraka haraka atasema kwa sababu wanapendeleana au wanabebwa. Lakini kuna sababu kubwa zaidi ya hiyo. Hakuna kitu kama hofu ya kutokuwepo. Jamii ya Wayahudi katika historia yake yote wamekuwa wakiishi na hii hofu ya kufutwa katika ulimwengu. Na zaidi ya yote lile suala la kutokuwa na mahali unaweza kupaita kwako.
Kwa upande wa jamii ya Wachagga tofauti na ya Wahaya na Wanyakyusa, wao mafanikio yao ya kiuchumi yanaendana kwa namna mmoja na hili suala la uwepo. Katika nchi yetu hakuna mahali ambapo kuna ugumu wa kupata ardhi mpya kama Kilimanjaro. Kama huna ardhi kilimanjaro, ardhi ambayo imepitishwa toka kwa wazazi wako ni vigumu sana kupata ardhi mpya. Ni hili tatizo la ardhi kwanza kabisa lililowasukuma wachagga wengi kuondoka Kilimanjaro na kwenda kuchangamkia tenda maeneo mengine. Tofauti na mikoa ambayo watu wake wana ardhi ya kutosha na hivyo wanaitegemea, Wachagga hawategemei ardhi yao isipokuwa utajiri ambao mwenyezi kawapa wao na sisi, yaani Ubongo.
Ni hili la kutokuwa na mahali pa kuendeleza Ardhi ndiyo kimekuwa chanzo cha wao kufanikiwa. Kama Wayahudi wao pia wanajikuta wanalazimika kufanya kila kitu kwa jitihada zaidi kwani wasipofanya hivyo watoto na watoto wa watoto wao wataishi wapi na vipi. Wengi wetu hapa kikiungua mjini tuna rudi kijijini kwetu, tuna uwezo wa kwenda kwenye maeneo ya nasaba zetu na kumegewa kipande cha ardhi toka shamba la babu, Wachagga hilo ni ngumu kweli kweli.
Hivyo, hili lilionekana tangu zamani. Wachagga walianza kuondoka Kilimanjaro na kwenda miji mingine mapema sana baada ya suala la ardhi kuanza kuonekana. Huku walikokwenda walikuwa wafanye nini, wengi walijiingiza kwenye biashara, wamekuwa na haraka sana ya kuchangamkia nafasi ya biashara. Hasa kupeleka kwa watu ambao ni jamii ya wakulima au wafugaji au jamii ya wavuvi. Wachagga wakawa wanaleta huduma na bidhaa zinazohitajika kwa jamii hizo.
Hili linalingana na Wayahudi vile vile, kwamba Wayahudi walikokwenda wamejiingiza kwenye sekta ya biashara katika kutoa huduma, miaka ya mwanzoni kama kule Ujerumani walijiingiza kwenye mambo ya kibenki, na hata walipokuja Marekani walichangamkia huduma za kibenki na mambo ya fedha. Walifanya hivyo wakijua kwamba jamii mpya ya Kimarekani inahitaji utaalamu katika sekta hizo, utaalamu ambao wao Wayahudi wamekuwa wakiutumia kwa karne nyingi. Wakafanikiwa katika biashara.
Sasa hivi sitoshangaa jamii ya Wachagga siyo tu wanaenda kwenye huduma za vitu muhimu, wataanza muda si mrefu kuingia katika mambo ya burudani (kama bado hawajaanza). This is a natural progression.
Nitaachana na wachagga na wayahudi kwa sekunde. Hapa Detroit kuna eneo linaitwa Dearborn. Eneo hili ndilo linamkusanyiko wa waarabu wengi zaidi kuliko eneo jingine lolote nje ya Mashariki ya Kati. Wengi wa waarabu waliokuja hapa walikuja kutokana na mabadiliko ya kisiasa ya Mashariki ya Kati miaka ya sabini na themanini na wale ambao walihamia huku miaka ya ugunduzi wa mafuta.
Waarabu (na hapa nazungumzia waarabu na wakaldeani) walipokuja hapa, kama jamii wakaanza kupeana huduma wao wenyewe. Biashara yao ya ndani na kusaidiana kupeana mikopo nje ya mfumo wa kawaida wa mikopo. Wafanyabiashara wa kiarabu wakiwa wameunganishwa na hasa na dini (Uislamu) wakaweza kuanza kujikita katika kutoa huduma. Walichokifanya ni kile kile kilichofanywa na Wayahudi, na kilichofanywa na Wachagga; wakaingia katika jamii ya watu weusi na wakaanza kufungua maduka ya huduma za haraka haraka (convenient stores) hasa baada ya maduka makubwa kama Farmer Jack, Meijers, na Kroger kufunga malango yao Detroit. Leo hii ukija Detroit, usishangazwe kukuta duka la mwarabu karibu kila baada ya mtaa.
Wanatoa huduma ile ambayo wanajua kuwa watu wa Detroit wanaihitaji. Na hapa napo kuna sentiments dhidi ya waarabu kwa sababu imekuwaje waje muda mfupi ulipita na wafanikiwe kiasi hicho. Utashangaa kuona kuwa waarabu wanashirikiana sana katika kufungua vituo vya mafuto, au maduka haya. Watu weusi hawawezi kukaa chini na kushirikiana kufanya biashara pamoja bila kushukiana (at least kwa mtazamo wangu na ni kuhusu baadhi yao). Jiji la Detroit ni asilimia 80 watu weusi, lakini ukija kwenye biashara za maduka haya karibu asilimia tisini yanamilikiwa na waarabu. Na cha kuchekesha ni kuwa wengi ya hawa waarabu hawatothubutu kuona mtoto wao wa kike anamdate mtoto wa mweusi!
Lakini na wao kinachowasukuma ni kile kile, siyo tu tamaa ya fedha (kama inavyohusishwa kwa wayahudi na wachagga japo waarabu hapa wanaonekana wana tamaa sana ya pesa) ni ile haja ya wao kuendelea kuwepo kama jamii ya watu na hasa wakijua ni nini walikiacha kule Iraq, na maeneo mengine ya mashariki ya Kati.
Hivyo basi utaona kuwa tatizo tunalolizungumzia ni suala la kijamii zaidi ambalo lina maelezo ya kisayansi lakini kwa vile baadhi ya watu hawataki kuliangalia kisayansi wanataka kutafuta sababu za kugeresha.
Tatizo kubwa ambalo ninaliona ni pale jamii hizi wayahudi, wachagga, na waarabu wanapoanza kuishi kana kwamba wao ni zawadi ya Mungu kwa wanadamu, na ya kuwa wao ndio "Taifa Teule". Ni hisia hizi za kujiona bora ndizo wakati mwingine zinasababisha hiyo resentment. Kufaninkiwa kwa jamii hizi kunaelezeka intellectually, na haihitaji divine providence kuelezea.
Hivyo ukweli huu wa kufanikiwa namna hii unaweza kupata watu wowote na mark my words ndio utakaofuel mafanikio ya Rwanda pia.