hongera kwa kufanya kazi UN ila tambua: mara nyingi hao UN hawasupply vifaa vyote bali wanatutaka tutumie vyetu kisha watulipe. tena wameshalalamikiwa na nchi nyingi kutolipa kwa wakati.tafuta kauli ya CDF Mwamunyange alipowaaga wajeda walioenda CONGO DRC. pili jiulize kwanini mission nyingi tuombwe sisi wakati wengine wapo? ni kwa sababu ya uwezo! hata kama vifaa ni vya UN maana yake tunajua kuvitumia vizuri na kwa lugha nyingine tunavyo kama hivyo ndo maana tunachaguliwa sisi zaidi. tatu mission nyingine hatuendi kwa sababu hatuwezi kujigawa sehemu zote zenye migogoro. tuko LEBANON, DARFUR na CONGO bado twende na kwingine, kwetu atalinda nani?