Swali ambalo mimi najiuliza, kama kupiga kura ni haki je hiyo si mpaka huo mchakato mzima ujengwe kwenye misingi ya haki pia? Au hakuna ulazima?
Ikiwa kama misingi ya uchaguzi haijazingatia haki, tutaanzaje kusema kitendo cha kupiga kura katika mazingira hayo ni kutimiza haki ya mpiigaji?
Kwanza siamini kuwa wanaoshiriki huu uchaguzi hawajui kuwa ni uchafuzi. Ni kwasababu wana bei ndogo na wamekubali kuingia kwenye huu uchaguzi kwasababu ya hongo waliyopewa.
Mgombea uraisi wa TLP hata mkoani hajafika, anapiga kampeni kwenye mkutano wa watu 10 halafu anasema anauhakika atashinda. Kweli nasisi tunaamini huyu mtu hajui ukweli wa huu uchaguzi na matokeo yatavyokuwa?
Vyama vilivyoshiriki kimsingi ni vyama vya CCM ambavyo vilitengenezwa kama backup pale ambapo chama chenye misimamo cha upinzani kitaenda tofauti.
Kuzuia aina hii ya uchaguzi naona ni fair kwasababu ni kiini macho tu, umekosa uhalali wa kusema ni uchaguzi ambao unaweza kumpa heshima au haki ya kweli anayepiga kura.
Mimi binafsi naona sio kila inayoitwa haki basi ni haki kweli nadhani haki lazima ipimwe, haki yako inaweza kuwa na umuhimu pale tu ambapo mifumo ya utekjelezaji hiyo haki inakuwa imejengwa kwa misingi ya haki.
Huko nyuma kulikuwa na haki ya kumiliki mtu (mtumwa) lakini saizi hatukubaliani kuwa ile ni haki licha ya watu wa miaka hiyo kuiita haki ni kwasababu tukiipima katika mizania ya haki kweli hatuoni uhalisia wake.
Mkuu,
Suala la haki ni nini ni pana sana na mara zote huwa tunatumia approximation, crude versions, agreements, etc.
Yani ni hivi, ukitaka kufuatilia haki pasu pasu always kuna room kwamba uchaguzi haukufuata haki.
In fact kifalsafa haki is a Selassian illusion, to be pursued, but never attained.
Yani unaweza kuhoji mpaka kwa nini baba yako kakuzaa wewe na wewe hujamzaa yeye, hiyo si haki.
Unaweza kusema kwamba kwa miaka yote iliyotawala CCM hata wafanye nini, hata wajiondoe kumchagua mwenyekiti wa tume, hata walete katiba mpya ya kumpunguzia rais madaraka, hata wakiue chama na kuwaachia wapinzani tu uchaguzi, ukitaka kusema uchaguzi haukuwa wa haki kwa sababu ya utawala wa CCM unaweza kujenga case hiyo, kimantiki kabisa. Kwa sababu ya legacy ya CCM. Yani hata ukiwaondoa ma CCM wote wasishiriki uchaguzi hiyo nayo itakuwa si haki.
Point ya msingi hapa, ambayo watu wengi wana i miss, ni discussion ya individuals rights.
Kama watu wameamua kushiriki katika uchaguzi, bila kujali huo uchaguzi ni wa haki au si wa haki (this is not the discussion, the discussion is about if wanaharakati wana haki ya kuwalazimisha wengine wasipige kura).
Wanaharakati wana haki ya kuwaingilia wanaotaka kupiga kura katika haki yao hiyo ya kushiriki katika uchaguzi?
Kama wanayo hii haki, maana yake kundi moja linaweza kulazimisha kundi jingine lifanye tofauti na linavyotaka.
Hili lina maana gani kwa wanaharakati?
Hawaoni kuwa hili linafungua mlango kwa wanaharakati nao kulazimishwa wapige kura katika uchaguzi wasioutambua?
I am more interested in the abstract philosophical points than the concrete politics of Tanzanian elections which many people seem to focus on.