Blue Bahari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,851
- 2,171
Naungana na wewe Mwaisa.sio kua mtoto anapigwa kila dakika au kila kosa, kuna kosa unaona kabisa hapa bila kumkanda huyu hatutasikilizana vizuri ili iwe wakat mwnegine akikosea ukimwambia anaelewa, ukimlea mtoto akakosea ukawa unasema tu ntakupiga ntakuchapa utanitambua huyu anakua anajua huna cha kumfanya zaidi ya maneno matupu kiboko sometimes ni kizuri.
Kenya walifuta kabisa viboko mashuleni. Matokeo yake..................Hizo nchi ambazo watoto hawachapwi zina mmonyoko mkubwa wa maadili pia ,sisi tunajiona hatuna maadili ila ukitembelea kwa wenzetu utaona bado sisi tuna maadili sana😁
Iv kulitokea nini mpaka wanataka kurudisha?Kenya walifuta kabisa viboko mashuleni. Matokeo yake..................
Kwa Sasa wanajadili Tena kuvirudisha viboko mashuleni.
Mimi nilishapigwa sana, sasa ni zamu ya watoto wangu kuchezea mbalata hasa first born ni mtundu kinoma. Nawaza tu kama na mimi niliwasumbua wazazi kama yeye anavyonivuruga mimi basi Mungu awabariki wazazi wangu 😁Kupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.
Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
Mtoto kama hana kazi atamtunzaje mzazi wake🤣? Baba alikuwa mwajiriwa akalea familia. Mtoto kamaliza shule ni afisa ubashiri au boda boda. Atatunzaje familia yake na mzazi kwa pamoja?Ahsante Sana kwa mada yako. Ndiyo Iko x usiku kucha jana na inaendelea.
Naongezea; tuna wazee wengi hawatunzwi na watoto wao waliowachapq Sana kwa madai ya kuwatengeneza. Je hii siyo MOJAWAPO ya athari ya mpasuko wa mahusiano ya watoto na Wazee ? Kwamba nguvu kubwa ilitumika kuumiza mwili badala ya ku transform akili ya ndani ya mtoto? Sasa mtoto kawa mkubwa, Tabia zake zilizokandamizwa kwa hofu ya kipigo, sasa zinaanza kushamiri na kumea maana hakuna wa kumpiga tena?
Nini maoni yenu?
Mtoto mtundu unaweza ku discuss naye kitu gani?😁 Nyie endeleeni na negotiations tu. Mtoto wangeni wamekuja anaanza kuchezea vyakula vyao mlivyowatengea kwenye sahani na wewe unacheka cheka tu eti junia usifanye hivyo bana.Unawajengea nidhamu ya uwoga watoto wako .
Ikiwa hawawezi kukusikiliza mpaka utumie viboko basi ujue hata wakikusikiliza ni kwakuwa wanaogopa viboko.
Ahsante Sana kwa neno. Nadhani pia, katika kutoa adhabu kwa watoto, wengi wetu hatuna kabisa ufahamu kuhusu hata Sheria ya mtoto inasemaje na tafiti kuhusu mengi kwenye malezi na makuzi. Mara ingine tunasahau kuwa, huenda kuna watoto wagumu kwa Sababu zingine ambazo zinahitaji mtaalamu kuzibaini, kuna wenye shida ya afya ya akili, utapiamloa ulioathiri makuzi ya mifumo ya akili, kuna wazazi na Walezi pia Wana dhida zao vilevile, yaani unaweza Kuta mambo ni vurugu na mtoto haelewi na mzazi haelewi na vipigo vikizidi mtoto anakimbia nyumbani anaingia mtaani anajifunza mabaya zaidi basi mzazi naye anasema nimemsusa.sio kua mtoto anapigwa kila dakika au kila kosa, kuna kosa unaona kabisa hapa bila kumkanda huyu hatutasikilizana vizuri ili iwe wakat mwnegine akikosea ukimwambia anaelewa, ukimlea mtoto akakosea ukawa unasema tu ntakupiga ntakuchapa utanitambua huyu anakua anajua huna cha kumfanya zaidi ya maneno matupu kiboko sometimes ni kizuri.
Kuna kliniki za watoto watundu na watukutu. Utakuja umuumize bure na sisi tuje na hii hapa 👇Mtoto mtundu unaweza ku discuss naye kitu gani?😁 Nyie endeleeni na negotiations tu. Mtoto wangeni wamekuja anaanza kuchezea vyakula vyao mlivyowatengea kwenye sahani na wewe unacheka cheka tu eti junia usifanye hivyo bana.
Kuiba ni subjective. Mkiamua kuchagua mtoto ambaye hana malezi mkampa uongozi ndiyo yanatokea haya yaliotokea.Waafrica na wazungu
Kuhusu maadili hatuwafikii
Ebu tazama tu viongozi wetu wanaiba mpaka unaogopa sasa unajiuliza maadili ya MTU mweusi ni yapi hayo
Sisi ni wahuni Sana hatuna maadili yoyote
Tumebaki kusema kuwa hatufanyi ushoga basi hayo ndo maadili
Mtoto analelewa na mikono mingi na Sasa kuna Hadi program za malezi na makuzi na marekebisho ya tabia. Adhabu za watoto tuwe makini nazo hasa watu wengi wanaoamini kwenye kupiga na kutoa frustration watoto kumbe mtoto naye ana yake mengine ikiwemo ya afya ya akili nk na mzazi naye anaweza akawa na yake vilevile, kisha likazaliwa janga jipya kumbe kliniki za kufanya. Diagnosis zipo.Sisi wa africa bila kunyukwa hatuendi jamii nyingi tunazotamani kuziiga nao wana mambo yao ya ajabu , sio kitu cha ajabu watoto wakizungu kuwaambia wazazi wao wanavutiwa na mahusiano ya jinsia moja na kwao ni kawaida tu.
Mda mwingne tusipuuze desturi zetu na kuiga za watu ambazo kiundani zina madhara yake pia.
Hakika, Ili mradi tu unaenda sambamba na uwepo wa hii hapa 👇Mi nachanganya vyote ,siku Moja Moja nawachangamsha na njiti na ninaona naenda vizuri.
Mazingira ,makuzi, maisha, DNA...Inategemea mkuu na mazingira mtoto alipo kulia,
Na pia hakikisha unatambua uwepo wa hii hapa 👇Njiti na kwenzi muhimu sana. Ila kubalance muhimu, wakati mwingine msomee Matayo sometimes piga nakoz
Hakika, na ndiyo maana watoto hukandamiza tabia zao kwa hofu tu, ila wakiwa wakubwa wanaibuka nazo kwenye ndoa huko, Kila siku kupigana. Maana zinakuwa zilikandamizwa kwa hofu badala ya kung'olewa na mwenye tabia kumiliko ung'oaji huo kwa kuwa ameelewa kuwa hili halifai na si kuwa ameogopa na kukandamiza au ku transform tabia yake kwenye tabia mpya Ili tu, ajisikie kashinda game. Mbaya sanaKupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.
Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
Hawana tabia ya kuchapa sawa ila watoto wamekuwa shaped na civilization. Mtoto ana ratiba maalum ya maisha na kujitegemea kwa 100%. Hivi kwa sisi wabongo mtoto gani ana ratiba ya maisha ilionyooka zaidi ya wale wanaokulia ushuani ambao ni kundi dogo sana.Nimeishi na waarabu hawana tabia hizo za kuchapa na watoto wao wamenyooka balaa! Wajapani nao pia hawana tabia hizo ila ndio wanaongoza duniani kuwa na discipline. Mi nadhani waafrica hatutaki kutoka nje ya box kifikra kufikiria njia mbadala za malezi isiwe lazima fimbo pekee yake. Halafu pia si waafrica muda wa kukaa na watoto wetu sometimes unakuwa ni changamoto sana nadhani hii pia inachangia
Kisayansi unaweza kuwa ulifanikiwa kujenga hofu na si kung'oa mzizi na kina cha tatizo. Na mwili ukiwa na stress, hujitengenezea tabia mbadala ya kumalizana na stress hiyo ama hata baadae. Kina cha migogoro ya mahusiano na kutoamini kwenye kuongea Hadi mpigishane kelele na hatimaye mpigane, ni matokeo ya ubongo kukosa mbadala wa Imani kuwa, mambo yanaweza kwisha kwa kuongea tu maana, haukuzoea hivyo na ukaacha kutengeneza skills.....mimi nawakanda vizuri tu na wananyooka mbona? ukimnyima mtoto mboko tarajia kituko
Civilization hakuna na uniformity ya maadili. Kwa familia zingine hayo matendo ni dhambi na yanapingwa kiimani ila kwa baadhi ya familia zinazofuga watoto hizo tabia zinakuwa overlooked.Mbona nchi zetu tunazochapa wototo zimejaa rushwa, uongo, ufisadi, kesi za kubambikia, ukwepaji kodi, uchepukaji, uvivu n.k?!
Yaani umemaliza. Sisi kwa kweli tunahitaji kuanzisha hii mijadala na kufungua wengine maeneo mengi Sana kwenye malezi na makuzi. Mungu akinipa muda, kabla ya mwisho wa mwaka tupige mijadala mitatu hivi ya mambo kadhaa tumekuwa tunatoa ahadi ila kamuda tu.Nimeishi na waarabu hawana tabia hizo za kuchapa na watoto wao wamenyooka balaa! Wajapani nao pia hawana tabia hizo ila ndio wanaongoza duniani kuwa na discipline. Mi nadhani waafrica hatutaki kutoka nje ya box kifikra kufikiria njia mbadala za malezi isiwe lazima fimbo pekee yake. Halafu pia si waafrica muda wa kukaa na watoto wetu sometimes unakuwa ni changamoto sana nadhani hii pia inachangia
Sisi huku watoto siyo wanachapwa, wanapigwa na kupigana na wazazi wao. Ngumi, mateke, wengine wanafungwa kwenye miti, wengine wamwagiwe maji ya moto, sad... Halafu mtu huyu anasifiwa na jamii....Hata huko magharibi kuna wachache wanatamani maisha ya kupiga watoto na wanawake ila ndio hivyo wanazidiwa nguvu na wale waliostaarabika zaidi kwa hiyo wanabaki kutamani wangeishi kama nyie
Kupiga mtoto at first hand naona haijakaa sawa isipokuwa tu kwenye attempts za uzembe. Mtoto alishafanya kosa hilo hilo mara mbili au zaidi hizo ni signs of negligence of which sio tabia nzuri kwa mtoto kukua nazo. Mara zote ulishamkanya ila anakuwa mzito kuelewa ni lazma umshtue kidogo.Mtoto hupewa adhabu akifanya makosa Kwa dhamiri.
Bahati mbaya Watoto wengi HUFANYA Makosa Bila dhamiri yàani Bila kujua ni Makosa.
Hivyo unapompiga inamtengenezea chuki zaidi ya kujifunza.
Kwa Bahati mbaya zaidi Wazazi wengi ni Wabinafsi, wakatili àmbao hujijali waô wènyewe.
Mzazi lazima uwe na Sifa ya Ualimu. Kumpiga Mtoto mara nyingi huleta matokeo Hasi kuliko matokeo chanya.
Fikiria Mtoto chini ya Miaka 14 unampiga mafimbo mengi kisa hajafua nguo Zake. Kumbe Mtoto mwenyewe hajafanya kusudi kutokufua Bali amesahau.
Sasa wewe kama siô chizi ni nini?
Au unampiga Mtoto Kisa kapoteza au kuangusha Pesa uliyomtuma akanunue maandazi. Mtoto hajafanya makusudi.
Kûna namna ya kudili na Makosa ya Mtoto hasa Yale àmbayo hajafanya kusudi.