Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

sio kua mtoto anapigwa kila dakika au kila kosa, kuna kosa unaona kabisa hapa bila kumkanda huyu hatutasikilizana vizuri ili iwe wakat mwnegine akikosea ukimwambia anaelewa, ukimlea mtoto akakosea ukawa unasema tu ntakupiga ntakuchapa utanitambua huyu anakua anajua huna cha kumfanya zaidi ya maneno matupu kiboko sometimes ni kizuri.
Naungana na wewe Mwaisa.
 
Kupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.

Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
Mimi nilishapigwa sana, sasa ni zamu ya watoto wangu kuchezea mbalata hasa first born ni mtundu kinoma. Nawaza tu kama na mimi niliwasumbua wazazi kama yeye anavyonivuruga mimi basi Mungu awabariki wazazi wangu 😁
 
Ahsante Sana kwa mada yako. Ndiyo Iko x usiku kucha jana na inaendelea.

Naongezea; tuna wazee wengi hawatunzwi na watoto wao waliowachapq Sana kwa madai ya kuwatengeneza. Je hii siyo MOJAWAPO ya athari ya mpasuko wa mahusiano ya watoto na Wazee ? Kwamba nguvu kubwa ilitumika kuumiza mwili badala ya ku transform akili ya ndani ya mtoto? Sasa mtoto kawa mkubwa, Tabia zake zilizokandamizwa kwa hofu ya kipigo, sasa zinaanza kushamiri na kumea maana hakuna wa kumpiga tena?

Nini maoni yenu?
Mtoto kama hana kazi atamtunzaje mzazi wake🤣? Baba alikuwa mwajiriwa akalea familia. Mtoto kamaliza shule ni afisa ubashiri au boda boda. Atatunzaje familia yake na mzazi kwa pamoja?
 
Unawajengea nidhamu ya uwoga watoto wako .

Ikiwa hawawezi kukusikiliza mpaka utumie viboko basi ujue hata wakikusikiliza ni kwakuwa wanaogopa viboko.
Mtoto mtundu unaweza ku discuss naye kitu gani?😁 Nyie endeleeni na negotiations tu. Mtoto wangeni wamekuja anaanza kuchezea vyakula vyao mlivyowatengea kwenye sahani na wewe unacheka cheka tu eti junia usifanye hivyo bana.
 
sio kua mtoto anapigwa kila dakika au kila kosa, kuna kosa unaona kabisa hapa bila kumkanda huyu hatutasikilizana vizuri ili iwe wakat mwnegine akikosea ukimwambia anaelewa, ukimlea mtoto akakosea ukawa unasema tu ntakupiga ntakuchapa utanitambua huyu anakua anajua huna cha kumfanya zaidi ya maneno matupu kiboko sometimes ni kizuri.
Ahsante Sana kwa neno. Nadhani pia, katika kutoa adhabu kwa watoto, wengi wetu hatuna kabisa ufahamu kuhusu hata Sheria ya mtoto inasemaje na tafiti kuhusu mengi kwenye malezi na makuzi. Mara ingine tunasahau kuwa, huenda kuna watoto wagumu kwa Sababu zingine ambazo zinahitaji mtaalamu kuzibaini, kuna wenye shida ya afya ya akili, utapiamloa ulioathiri makuzi ya mifumo ya akili, kuna wazazi na Walezi pia Wana dhida zao vilevile, yaani unaweza Kuta mambo ni vurugu na mtoto haelewi na mzazi haelewi na vipigo vikizidi mtoto anakimbia nyumbani anaingia mtaani anajifunza mabaya zaidi basi mzazi naye anasema nimemsusa.

Mara ustawi wa jamii wakimchukua wakimpeleka kwenye program za marekebisho ya tabia mtoto anasimulia mambo makubwa, hatimaye anafunguliwa anarekebishika, kumbe tunaweza kutoa adhabu fulani za kiwango cha mtoto na ikishindikana basi tukumbuke kuna sayansi nyuma ya malezi na makuzi ya mtoto na kuna program za marekebisho ya tabia kitaalamu. Ngoja niwape hapa kipande cha Sheria kwa wale wanao amini kwenye ukibisha nakupiga tu Bora nifungwe👇 naamini itafunguka.
 

Attachments

  • IMG-20241020-WA0006.jpg
    IMG-20241020-WA0006.jpg
    94.3 KB · Views: 2
Mtoto mtundu unaweza ku discuss naye kitu gani?😁 Nyie endeleeni na negotiations tu. Mtoto wangeni wamekuja anaanza kuchezea vyakula vyao mlivyowatengea kwenye sahani na wewe unacheka cheka tu eti junia usifanye hivyo bana.
Kuna kliniki za watoto watundu na watukutu. Utakuja umuumize bure na sisi tuje na hii hapa 👇
 

Attachments

  • IMG-20241020-WA0006.jpg
    IMG-20241020-WA0006.jpg
    94.3 KB · Views: 3
Waafrica na wazungu

Kuhusu maadili hatuwafikii

Ebu tazama tu viongozi wetu wanaiba mpaka unaogopa sasa unajiuliza maadili ya MTU mweusi ni yapi hayo

Sisi ni wahuni Sana hatuna maadili yoyote

Tumebaki kusema kuwa hatufanyi ushoga basi hayo ndo maadili
Kuiba ni subjective. Mkiamua kuchagua mtoto ambaye hana malezi mkampa uongozi ndiyo yanatokea haya yaliotokea.

Hujiulizi kwanini Nyerere alipokuwa madarakani wizi haukuwa praised? Ila walipokuja viongozi ambao wana tamaa ya madaraka na mali ndio wakaanzisha mifumo ya wizi serikalini na waliofuata wote waka adopt tabia ya wizi na unyang'anyi of which sio maadili ya kitanzania but ni influential behaviours.

What made things worse was getting out of the office unshackled made possible through creation of cartels and gangs. Hili halitaisha bila mother of all governing laws kuwa revised. Kuna loopholes nyingi ambazo zinafanikisha hawa wasio na maadili kuendelea kuwepo na kupandikiza vizazi vyao kwenye mfumo. We gotta get rid of it first.
 
Sisi wa africa bila kunyukwa hatuendi jamii nyingi tunazotamani kuziiga nao wana mambo yao ya ajabu , sio kitu cha ajabu watoto wakizungu kuwaambia wazazi wao wanavutiwa na mahusiano ya jinsia moja na kwao ni kawaida tu.

Mda mwingne tusipuuze desturi zetu na kuiga za watu ambazo kiundani zina madhara yake pia.
Mtoto analelewa na mikono mingi na Sasa kuna Hadi program za malezi na makuzi na marekebisho ya tabia. Adhabu za watoto tuwe makini nazo hasa watu wengi wanaoamini kwenye kupiga na kutoa frustration watoto kumbe mtoto naye ana yake mengine ikiwemo ya afya ya akili nk na mzazi naye anaweza akawa na yake vilevile, kisha likazaliwa janga jipya kumbe kliniki za kufanya. Diagnosis zipo.

Hivyo, mzazi anayesema nitatoa adhabu ya kipigo, pia awe makini na uwepo wa hii hapa👇
 

Attachments

  • IMG-20241020-WA0006.jpg
    IMG-20241020-WA0006.jpg
    94.3 KB · Views: 2
Kupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.

Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
Hakika, na ndiyo maana watoto hukandamiza tabia zao kwa hofu tu, ila wakiwa wakubwa wanaibuka nazo kwenye ndoa huko, Kila siku kupigana. Maana zinakuwa zilikandamizwa kwa hofu badala ya kung'olewa na mwenye tabia kumiliko ung'oaji huo kwa kuwa ameelewa kuwa hili halifai na si kuwa ameogopa na kukandamiza au ku transform tabia yake kwenye tabia mpya Ili tu, ajisikie kashinda game. Mbaya sana
 
Nimeishi na waarabu hawana tabia hizo za kuchapa na watoto wao wamenyooka balaa! Wajapani nao pia hawana tabia hizo ila ndio wanaongoza duniani kuwa na discipline. Mi nadhani waafrica hatutaki kutoka nje ya box kifikra kufikiria njia mbadala za malezi isiwe lazima fimbo pekee yake. Halafu pia si waafrica muda wa kukaa na watoto wetu sometimes unakuwa ni changamoto sana nadhani hii pia inachangia
Hawana tabia ya kuchapa sawa ila watoto wamekuwa shaped na civilization. Mtoto ana ratiba maalum ya maisha na kujitegemea kwa 100%. Hivi kwa sisi wabongo mtoto gani ana ratiba ya maisha ilionyooka zaidi ya wale wanaokulia ushuani ambao ni kundi dogo sana.
 
mimi nawakanda vizuri tu na wananyooka mbona? ukimnyima mtoto mboko tarajia kituko
Kisayansi unaweza kuwa ulifanikiwa kujenga hofu na si kung'oa mzizi na kina cha tatizo. Na mwili ukiwa na stress, hujitengenezea tabia mbadala ya kumalizana na stress hiyo ama hata baadae. Kina cha migogoro ya mahusiano na kutoamini kwenye kuongea Hadi mpigishane kelele na hatimaye mpigane, ni matokeo ya ubongo kukosa mbadala wa Imani kuwa, mambo yanaweza kwisha kwa kuongea tu maana, haukuzoea hivyo na ukaacha kutengeneza skills.....

Lakini pia, unapofanya hayo ya kupiga piga tu, basi ukumbuke kuna 👇 ambayo siku moja itakupiga na wewe.
 

Attachments

  • IMG-20241020-WA0006.jpg
    IMG-20241020-WA0006.jpg
    94.3 KB · Views: 2
Mbona nchi zetu tunazochapa wototo zimejaa rushwa, uongo, ufisadi, kesi za kubambikia, ukwepaji kodi, uchepukaji, uvivu n.k?!
Civilization hakuna na uniformity ya maadili. Kwa familia zingine hayo matendo ni dhambi na yanapingwa kiimani ila kwa baadhi ya familia zinazofuga watoto hizo tabia zinakuwa overlooked.

Ndio maana ulipoanza kazi hukuwa na mawazo kuwa utakujaga kuandaa activity za uongo ili tu upate fedha za kufanyia starehe za weekend. Ila ulikutana na watu wanafanya hayo kama jambo la kawaida tu wakakushawishi. Tabia mbaya huwa ni influential.
 
Nimeishi na waarabu hawana tabia hizo za kuchapa na watoto wao wamenyooka balaa! Wajapani nao pia hawana tabia hizo ila ndio wanaongoza duniani kuwa na discipline. Mi nadhani waafrica hatutaki kutoka nje ya box kifikra kufikiria njia mbadala za malezi isiwe lazima fimbo pekee yake. Halafu pia si waafrica muda wa kukaa na watoto wetu sometimes unakuwa ni changamoto sana nadhani hii pia inachangia
Yaani umemaliza. Sisi kwa kweli tunahitaji kuanzisha hii mijadala na kufungua wengine maeneo mengi Sana kwenye malezi na makuzi. Mungu akinipa muda, kabla ya mwisho wa mwaka tupige mijadala mitatu hivi ya mambo kadhaa tumekuwa tunatoa ahadi ila kamuda tu.
 
Hata huko magharibi kuna wachache wanatamani maisha ya kupiga watoto na wanawake ila ndio hivyo wanazidiwa nguvu na wale waliostaarabika zaidi kwa hiyo wanabaki kutamani wangeishi kama nyie
Sisi huku watoto siyo wanachapwa, wanapigwa na kupigana na wazazi wao. Ngumi, mateke, wengine wanafungwa kwenye miti, wengine wamwagiwe maji ya moto, sad... Halafu mtu huyu anasifiwa na jamii....

Wanasahau kuna kliniki za malezi na makuzi na 👇
 

Attachments

  • IMG-20241020-WA0006.jpg
    IMG-20241020-WA0006.jpg
    94.3 KB · Views: 2
Mtoto hupewa adhabu akifanya makosa Kwa dhamiri.
Bahati mbaya Watoto wengi HUFANYA Makosa Bila dhamiri yàani Bila kujua ni Makosa.

Hivyo unapompiga inamtengenezea chuki zaidi ya kujifunza.

Kwa Bahati mbaya zaidi Wazazi wengi ni Wabinafsi, wakatili àmbao hujijali waô wènyewe.

Mzazi lazima uwe na Sifa ya Ualimu. Kumpiga Mtoto mara nyingi huleta matokeo Hasi kuliko matokeo chanya.

Fikiria Mtoto chini ya Miaka 14 unampiga mafimbo mengi kisa hajafua nguo Zake. Kumbe Mtoto mwenyewe hajafanya kusudi kutokufua Bali amesahau.

Sasa wewe kama siô chizi ni nini?

Au unampiga Mtoto Kisa kapoteza au kuangusha Pesa uliyomtuma akanunue maandazi. Mtoto hajafanya makusudi.

Kûna namna ya kudili na Makosa ya Mtoto hasa Yale àmbayo hajafanya kusudi.
Kupiga mtoto at first hand naona haijakaa sawa isipokuwa tu kwenye attempts za uzembe. Mtoto alishafanya kosa hilo hilo mara mbili au zaidi hizo ni signs of negligence of which sio tabia nzuri kwa mtoto kukua nazo. Mara zote ulishamkanya ila anakuwa mzito kuelewa ni lazma umshtue kidogo.

Africa genetically tuna hizo element za kufanya mambo ya uzembe ikiwa hakutakuwa na gharama za maumivu kwa namna fulani.

Wazungu wao wana condition watoto in another way round. Hawa impose physical disturbance ila psychologically kama ku deny mtoto kufanya michezo flani kama way of punishment. Hawaruhusiwi kupiga ila adhabu wanatoa.
 
Back
Top Bottom