Jeff Leah: Yanga itafungwa 3-0 na Marumo na nina uhakika haitofuzu Fainal wala kuchukua kombe

Jeff Leah: Yanga itafungwa 3-0 na Marumo na nina uhakika haitofuzu Fainal wala kuchukua kombe

Mchambuzi nguli mwenye kujua vizuri kiingereza Goeff Leah kutoka sports headquarters Efm amesema ana uhakika Marumo atashinda tena goli kuanzia 3-0 na Yanga hatofuzu na hivyo ndoto za ubingwa zitaishia hapo.

Mimi kama mjumbe siuwawi, njooni mtoe ya moyoni, mtiririke na kuserereka
Tegeta Sec School ndo ajue kiingereza kweli.
 
Mchambuzi nguli mwenye kujua vizuri kiingereza Goeff Leah kutoka sports headquarters Efm amesema ana uhakika Marumo atashinda tena goli kuanzia 3-0 na Yanga hatofuzu na hivyo ndoto za ubingwa zitaishia hapo.

Mimi kama mjumbe siuwawi, njooni mtoe ya moyoni, mtiririke na kuserereka
Endelea kuvuta tu kama inavyoonekana picha yako
 
Nyie ndiyo mnao waangusha wachambuzi ikiwa kinyume utakuja na uongo mwingine ila ujuwe yanga bingwa.
 
Anajua kiingereza? Hajui kiingereza kabisa anachojua kiswangish,hayo mambo ya nani kufungwa tusubiri mpira ukiisha
Kaa kimya mambo mengine kama huyajui!!mtu toka chekechea hadi form six amesomea shule za kingereza tu,leo useme hajui kingereza?!!
Kwani hayo si maoni yake? Kosa liko wapi,?hebu jaribuni kuwa mnaheshimu mitazamo ya watu hata ikiwa ni tofauti na wako.Povu la nini sasa?!!
 
Mnapenda ku catch feelings kwenye vitu vidogo.

Mchambuzi anaongea kupitia takwimu na sio kuridhisha upande eti kwasababu ni timu ya nyumbani au namna gani.

Hakuajiriwa kwa kazi hiyo na isingependeza boss wake kuona kila siku unajadili mlengo mmoja tu wa kimaoni.

Huyo Geaf Leah ni mshabiki mkubwa wa Mayele tena sana na anamuelezea kwa namna ya kiukubwa sana pengine tofauti na wachambuzi wengine wote ambao mimi nimewasikiliza chambuzi zao.

Hapo umem attack kupitia tittle tu ya uzi lakini naimani hujasikiliza sababu za msingi kwanini yeye ameona hivyo.

Huwa nashangazwa sana sometimes unakuta matokeo yamekuja kinyume na wachambuzi walivyobashiri basi kila mtu anaanza kuwarudia kuwatukana.

Hiyo sio fair na ukitaka kuona jaribu kufatilia tu hata hapo studioni wanakuwa wachambuzi wenyewe kwa wenyewe wanatofautiana maono.

Lakini angalia namna wanavyo argue kisomi kukosoa maoni ya mchambuzi mwezake kwa kutoa sababu za mashiko kuonesha namna gani mwezake hayupo sahihi.

Huwezi kukuta wanatukanana kwa hiki kiwango ambacho sisi mashabiki tumekuwa tukiwafanyia.
Kaongeza kupitia ya takwimu haya mtakwimu ..lete hizo takwimu za kufanya yang afungwe tatu bila...
 
Kibu ni Bora kuliko Mayele..... Imejiandika tu
Watu walisema na ilifaa tuwaheshimu maoni yao.

Vile vile kuna watu waliwahi kusema na matokeo yakaja vile vile kama walivyosema, hatuwezi tukachukua hiyo kama fimbo ya kuanza kuwatusi.

BTW mimi niliwakataa Rivers United mapema siku ile ile ilipotolewa draw.
 
Screenshot_20230517-082056~2.png

Scars ... Kama unamuani ... Odds hizo hapo weka laki Marumo afikishe goli 3 uamke na laki5 ... Acha uzwazwa weka mzigo ...
 
Wengi humu mna mahaba yaliyopitiliza kwa timu yenu, mchambuzi kusema timu yako itafungwa akatoa na sababu zake.sio jambo la ajabu, ndivyo ilivyo hapa duniani.

Inaweza kutokea au isitokee, kwasababu mwisho wa siku wachambuzi nao ni binadamu sio malaika, msiende mbali mpaka kuwachukia, hapo mnakuwa mmevuka mipaka kihisia.
 
Back
Top Bottom