Nonda alipouzwa Yanga hawakuambulia hata sumni, tusidanganyane hapa. Tena alitoroshwa afadhali hata sasa hivi tuna huu utaratibu wa kinafki wa kutoa "Thank You". Sikilizeni niwambie, kwenye mauzo ya mchezaji, wakati mwingine unapewa option, kuna option ya ununuzi wa jumla au kama huu unaofanana na mkopo maana hauna umiliki wa 100% wa mchezaji huyo. Hii inasaidia kumpata mchezaji huyo kwa gharama nafuu zaidi ingawa option ya kumpata moja kwa moja kwa gharama kubwa zaidi bado unapewa. Tunaita mkopo kwa sababu hizo. Pia mchezaji wa mkopo hauwezi kumuuza bila idhini ya timu hiyo nyingine. Au nyie mnadhani kumpata mchezaji kwa mkopo kunafananaje? Mnadhani mchezaji unayempata kwa mkopo haumlipii chochote?
Hata Max amekuja Yanga kwa mkataba wa namna hiyo hiyo. Nilikuwa mtu wa kwanza kusema hili la mkopo wa Mayele kabla hata ya hawa kina Jemedari au mtu mwingine yoyote, nakumbushia tu.