Hongera Sana Venance Mabeyo kwa hili“[Hiki] kilikuwa ni kipindi kigumu kidogo. Lakini tulisimama kidete, kwa utulivu mzuri, kama jeshi, tukitimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Katiba, kuilinda nchi yetu [na] kuilinda Katiba.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hongera Sana Venance Mabeyo kwa hili“[Hiki] kilikuwa ni kipindi kigumu kidogo. Lakini tulisimama kidete, kwa utulivu mzuri, kama jeshi, tukitimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Katiba, kuilinda nchi yetu [na] kuilinda Katiba.
Acha kutengeneza fikra za udaku ndani ya story nzuri ya CDF. 🙏🙏🙏Hapo kasema yeye akiwakilisha JWTZ inamaana DIGIS na IGP wao walisimamia upande gani?? najaribu kuwaza tu.
Acha uongo CIA inajitegemea wao na NSA etc wote wanajitegemea, japo CIA wapo jeshiniWapo chini yake. Hata CIA ni kitengo cha Jeshi la Marekani
Kuna msemo maarufu wa kiingereza usemao, " let sleeping dogs lie"Story za vijiweni na kusadikika
Alikuwa assassinated na nani?He talks too much mpaka atatoa na siri za jinsi Jiwe alivyofariki. Anamaliza muda wake basi aondoke tu kwa amani....Utumishi uliotukuka!
View attachment 2270187
Huyu mnafiki alizidiwa kete na kina JK, ndo maana akasimama kidete, mbona alikuwa anapeleka wajeda kusafisha barabaraNadhani anastahili pongezi badala ya dhihaka.
Asingesimama kidete hakika hii Tanzania tunayoiona leo na kufurahia amani ingekuwa nyingine kabisa.
Hongera CDF Mabeyo [emoji437]
Tofauti ipo kubwa, utekaji na mauaji vimeisha na wahuni kama Sabaya wametumbuliwa na kupelekwa mahakamaniReally!!?
akili yako haijaona tofauti Magufuli akiwa hai na akiwa amekufa?
unaelewa maana ya power vacum?
Utata upi? Ugonjwa wa moyo ndio utata?Ku facilitate Smooth transition naona bado sio issue ya Kujisifia, They were deserve to do that, what am i worried ni kuwa hawa seniors officials waliopo kwenye izo Intelligence communities walifanya nini kumlinda The late mpaka anakufa kifo tata vile
acheni kumsingizia mzee bashiruBashiru Ally Kakurwa
Wewe unatoa.matusi,uliwahi kuona general yupi kwenye nchi.hii kila kukicha anatafuta mahali pa kuongea...?jinga kubwa wewe. kila kitu mnaingiza siasa.
Kuna wengine humu mwaka huo wa 2005 hata chekechea hawajaanza.unahangaika kuusumbua kichwako bulu mkuu.muache siku akimuuliza babu yake akiambiwa ukwelu ataona aibu atarudi.kufuta uzi wake.cdm wagombea
mbowe -2005
dr slaa 2010
lowasa - 2015
lisu -2020
Naweza kurekebishwa km nimekosea
samia ana degreeAlichofanya alizuia maccm yaliyotaka kumpindua Samia kisa Hana degree kama Sheria inavotaka wakati Mzee magu amedanji. Lakini ccm kila siku wanavunja Sheria yeye ameufyata. Asituchuze
Mkuu Ni kweli kuwa mama samia Hana degree? Hiyo masters yake aliyonayo kaipate sasa?? Tuache uzushiAlichofanya alizuia maccm yaliyotaka kumpindua Samia kisa Hana degree kama Sheria inavotaka wakati Mzee magu amedanji. Lakini ccm kila siku wanavunja Sheria yeye ameufyata. Asituchuze
2005 ulikuwa na umri gani?. Ulikuwa unaelewa nini kinaendelea duniani?.mbowe hakuwahi kugombea urais.
kumbe na wewe ni kila,za
Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
Wapuuzi tu hawa , hiyo katiba walikuwa wapi kuilinda Kule Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu huyo kengevwao alipokuwa anawatumia kama condom kuua wapinzani na kuvuruga uchaguzi 2020 Zanzibar na Bara ?View attachment 2270035
====
Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) anayemaliza muda wake Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ametaja kifo cha Rais wa awamu ya tano John Magufuli, na matukio yaliyofuata baada ya tukio hilo, kama moja kati ya changamoto kubwa alizokabiliana nazo kwani Jeshi lilipaswa kusimama kidete kuilinda Katiba ya nchi.
Mabeyo, aliyeanza kutumikia wadhifa huo mnamo Februari 6, 2017, baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli, akichukua nafasi ya Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange, alieleza hayo wakati wa mahojiano maalum na kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha ITV hapo Juni 22, 2022.
“Nadhani [Watanzania] ni mashuhuda [kwamba] kwa mara ya kwanza, [Tanzania] tukampoteza Rais aliyekuwa madarakani,” Mabeyo, 65, alisema wakati wa mahojiano hayo.
“[Hiki] kilikuwa ni kipindi kigumu kidogo. Lakini tulisimama kidete, kwa utulivu mzuri, kama jeshi, tukitimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Katiba, kuilinda nchi yetu [na] kuilinda Katiba.
“Na hilo likapita salama. Tukampokea Rais mpya, ambaye tunaendelea naye mama Samia Suluhu Hassan, na naamini kwamba tunaendelea vizuri. Nchi iko salama mpaka sasa. Wananchi wako watulivu, wanaendelea kufuata miongozo kama inavyotolewa na Serikali,” aliongeza Mabeyo.
Rais Magufuli alifariki mnamo Machi 17, 2021, kutokana na matatizo ya moyo, tukio lilioandika historia mpya kwa taifa la Tanzania ya Rais kufariki akiwa madarakani. Habari za kifo cha Rais huyo aliyekonga nyoyo za watu wengi na kuwakera wengine zilitangazwa usiku wa Machi 18, 2021, na aliyekuwa Makamu wake wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Samia aliapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita mnamo Machi 19, 2021, huku Jeshi la Ulinzi (JWTZ), ambalo kazi yake kuu ni kulinda Katiba na mipaka ya nchi, likipongezwa kwa kiasi kikubwa kusimamia uhamisho huo wa madaraka kwa utulivu mkubwa.
Matishio ya ugaidi
Mabeyo, ambaye aliagwa rasmi bungeni hapo Juni 14, 2022, huku Spika wa Bunge Tulia Ackson akimshukuru kwa “utumishi wako uliotukuka” kwa Tanzania, alitaja matishio ya ugaidi ambayo Tanzania imekuwa ikikabiliana nayo kwa miaka ya hivi karibuni kama moja ya “milima” aliyopaswa kuipanda wakati wa uongozi wake.
Matukio haya ni pamoja na yale ya Amboni, mkoani Tanga; Kibiti, mkoa wa Pwani; ugaidi huko mkoani Mwanza; na huko Mtwara kwenye mpaka na Msumbiji ambako magaidi wamekuwa wakifanya maisha ya jamii za karibu na mpaka huo kuwa magumu kwa kutokuwa na uhakika wa usalama wao.
“Kwa kweli, kipindi hicho kilikuwa kigumu sana lakini tunashukuru ushirikiano na wananchi, ushirikiano na vyombo vingine vya usalama, tumeweza kuhimili,” alibainisha Mabeyo kwenye mahojiano hayo.
“Lakini ni bahati mbaya kwamba majirani zetu [Msumbuji] wanakabiliwa sasa na tishio hilo [la ugaidi] kwa kiasi kikubwa. Na sisi kama sehemu ya ukanda wetu huu wa [Nchi za Kusini mwa Afrika] tumekubaliana kwamba tuwasaidie wenzetu,” aliongeza Mabeyo.
Migogoro ya ardhi
Kwenye mahojiano hayo pia, Mabeyo alikiri uwepo wa migogoro ya ardhi baina ya jeshi na wananchi, akisema mingi ya migogoro hiyo inatokana na Serikali kushindwa kulipa fidia kwa wakati lakini pia uvamizi wa maeneo ya jeshi na wananchi.
Migogoro ya ardhi kati ya jeshi na wananchi ni tatizo kubwa ambalo mara kadhaa Serikali imeahidi kutafuta namna bora za kukabiliana nalo.
Hivi karibuni, kwa mfano, Waziri wa Ulinzi Dk Stergomena Tax alikiambia kituo cha habari cha Dar24 kwamba Serikali iliandaa mpango wa miaka mitatu – 2020/2021 mpaka 2022/2023 –kwa ajili ya kutatua migogoro hiyo.
“Kwa sasa wataalam wapo sehemu mbalimbali za nchi ambazo zimeainishwa na kuna baadhi migogogoro imeshatatuliwa na kuna sehemu bado inaendelea kutafutiwa ufumbuzi,” Dk Tax amenukuliwa akisema.
Kwenye mahojiano yake na ITV, Mabeyo alisema jeshi linafanya kila linalowezekana kuhakiksha migogoro iliyopo sasa inatatuliwa na kwamba hakuna migogoro mipya inazalishwa.
Alipoulizwa anatamani kuona jeshi la aina gani muda huu ambao anaenda kustaafu, Mabeyo alisema kwamba anatamani Jeshi la Tanzania liwe la kisasa zaidi, huku likijitegemea na kutoa mchango zaidi katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
“Kwa nini wenzetu wanatengeneza zana wanatuletea kutuuzia sisi?” anauliza Mabeyo. “Kwa nini na sisi tusitengeneze zana za kututosheleza sisi wenyewe? [Wenzetu] wana hoteli, wana nyumba nzuri ambazo watu wanakuja wanakaa wanaongeza uchumi wa nchi. Na sisi jeshi letu liwe hivyo.”
Lukelo Francis ni mwandishi wa The Chanzo kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Anapatikana kupitia lukelo@thechanzo.com.
Ambapo na kesi ya mwisho ikiishaakaachiwa manake mahakama imemsafisha si ndio!Tofauti ipo kubwa, utekaji na mauaji vimeisha na wahuni kama Sabaya wametumbuliwa na kupelekwa mahakamani
Mpaka tuone itakuwajeAmbapo na kesi ya mwisho ikiishaakaachiwa manake mahakama imemsafisha si ndio!
Unajitekenya na kucheka mwenyewe, raisi akipita kwa wizi wa kura mbona hawaingilii kati na kutangaza uhalisia? Wizi na ufisadi mkubwa unapofanyika na kulipotezea taifa rasilimali zake huwa wanakuwa off kazini au! Tena kazi yao ni kulinda nchi na mipaka yake yote, twiga, Tanzanite na vitu vyote vilivyomo ndani yake.Tatizo kubwa hamuelewi changamoto kubwa iliyokuwepo baada ya kifo cha Magufuli.
Hamjui kuwa kuna watu ambao wapo mpaka sasa, walijitayarisha kuuteka urais.
Nyie mnaona jeshi lipo lipo tu, hamjui kuwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama vilisha tekwa na kuwa compromised.
Mama Samia siku ya kuapishwa alipelekwa Ikulu na Jenerali wa jeshi.
Hongera jeshi letu, lilifanya kazi nzuri.