Jenerali Ulimwengu: Hakukuwa na Uchaguzi huru na haki

Anaye amini kuwa kulikuwa na uchaguzi, apelekwe mirembe mara moja.. -Mbowe!
Mbowe huyuhuyu aliyesema anakuwa waziri mkuu ndani ya saa72? Baada ya kukosa ubunge anasema kulikuwa HAKUNA uchaguzi. Sasa imekuwaje kaacha ubunge bila uchaguzi?
 
Mtukane tena kwa matusi motomoto. Nilidhani ingekuwa vyema ungejikita kwenye kukikosoa kile alichokiongea kwenye mahojiano, wewe umeenda kwenye kufanya personal attack
 
Jenerali amesema ukweli, tena ukweli uliokuwa wazi kwa kila mtu. Huu haukuwa uchaguzi bali uchafuzi.

Mwisho Jenerali ametoa angalizo muhimu, kitakachofuata sasa ni siasa za chini chini ambazo sio afya kwa taifa letu.
 
Maji yamejaa jangwani kisa wapinzani
 
Hapo zamani akiwa kijana na njama zao akijidai mwanamapinduzi na mfuasi mkubwa wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea hivi leo kila akifungua mdomo kwenye vyombo vya nchi za kibeberu ni kukandia tu chama na nchi iliyomlea.
Jibuni hoja sio kukimbilia kukemea.
 
Nioneshe kituo kilichobandikwa mstokeo
 
Internet imerudishwa na nyinyi mataga mnafurahi sasa malaika kairudisha
 
Hizi ndio akili za Watanzania walio wengi. Inasikitisha sana
 
Haingii akilini kuwa Majimbo na Kata zote nchini iaminike, kwa hoja yake kuwa maeneo kadhaa nchini zilionekana kura feki na kwamba mawakala wa vyama vya upinzani walio wengi waliondolewa vituoni. Sababu zote hizo ni za kitoto kutolewa na mwandishi nguli kama Jenerali Ulimwegu. Anajiaibisha kutokuthibitisha madai hayo kwa takwimu na ushahidi.

Upinzani hata kama kwa miaka 5, kwa hoja yake kuwa wapinzani walitendewa mambo ambayo kimsingi ukiyaangalia siyo fair kabisa, wakiwa ni viongozi wanaotaka kuchukuwa madaraka ya kuongoza nchi, walipaswa kutumia njia mbadala na kujiandaa ili wapiga kura wawaamini. Lakini badala yake kwa kauli na matendo yao wapiga kura waliwasikia na kuwaona na mwisho wake wakawaadhibu kwenye sanduku la kura.
 
Jenerali alimtia ndimu Membe na online Tv yake kwa ma interview Membe akakolea akanyea kambi wenzake wakammwaga kisha Jenerali na Dotto Bulendu nao wakamzimia connection mzee wa watu akapotea siasani ndani ya siku 65 tu.
 
Wewe unamvamia ulimwengu badala ya kuvamia hoja yake. Jamani tujifunze kujielekeza kwenye hoja badala ya kutoa vihoja.

Ulimwengu kaeleza sababu za yeye kusema Uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Wewe tuambie uchaguzi ulikuwa huru na wa haki kwa sababu hizi na sio ku-introduce noise kwenye mjadala kwa kung'ang'ana na personality ya mtoa mada badala ya main issue.
 
Jambo zuri kila mmoja wetu ataulizwa mbele ya Mungu. Kila ukifanyacho hata kidogo kama sisimizi kiwe kizuri au kibaya lazima utaulizwa tu.

Mwalimu wangu mmoja wa madrasa aliwahi niambia omba sana Mungu ukipewa vitu vitatu, elimu, madaraka na pesa na lia usiku kucha ukipewa vyote vitatu maana ni mtihani mzito kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…