Jerry Silaa: Watu wote wanaozungumza kwa kufoka kwenye suala la Mkataba wa DP World wamenunuliwa

Kwa mood walionayo wapiga kura wake,atadhubutu kuwaomba wamchague Tena? Ni Bora angefata wenzie walionyamazia jambo hili
 
Mkataba bado haujasainiwa, kilichosainiwa nai makubalianao kwa ajili ya kuja kutengeneza mikataba hapo baadaye. Huwezi ukaweka ukomo wa muda kwenye makubaliano, kwa sababu kila mkataba utakuwa unakuwa na timeframe yake
Acha kupotosha, bungeni hakupelekwi makubaliano, bali mikataba. Soma katiba ya Jamhuri ya Muunga ya Tanzania ibara ya 63, kifungu cha 3, kifungu kidogo e. Nakiweka hapa chini.



Sasa wewe Makanyaga niwekee kifungu chochote cha sheria kinachosema bungeni (Tanzania) unaweza ukapeleka makubaliano yakapitishwe.

 
Kaja na shehena ya mabuku, nyaraka na bahasha zenye dokumenti "siri" za kamati ya bunge ...






TOKA MAKTABA

Mwaliko kwa wadau wafike Dodoma kutoa maoni

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
Simu: +255 026 23222761-5
Fax No. +255 026 2322624
E-mail: cna@bunge.go.tz
TAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 941,
DODOMA.

Kamati ya Pamoja (Joint Committee) ya Bunge ya Miundombinu na ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai
kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023(Intergovernmental Agreement – IGA , between the United Republic of Tanzania and the Emirate of Dubai concerning Economic and Social Partnership for the Development and Improving Performance of Ports in Tanzania).

Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Jumanne tarehe 06, Juni saa 7:30 mchana katika Ukumbi wa Msekwa ‘D’, Ofisi ya Bunge, Jijini Dodoma.

Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Azimio hilo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.

Vilevile Kamati itapokea maoni kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:-

Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli
DODOMA.
Baruapepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz

Azimio hilo linaweza pia kupakuliwa katika tovuti ya Bunge,
www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya
hatua za kiutawala.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA
 
Jerry mbunge wangu tumia muda mwingi Sana kujikita bungeni, Barabara za mitaa yako iko shida. Huko kwenye mikataba unapoteza muda. Ungekuwa makini ungeniandaa kwenye vifungu na Sheria badala ya kupiga siasa .wanasheria wame base kwenye Sheria wewe unaleta siasa. Feeling sorry for you.
 
Mkataba bado haujasainiwa, kilichosainiwa nai makubalianao kwa ajili ya kuja kutengeneza mikataba hapo baadaye. Huwezi ukaweka ukomo wa muda kwenye makubaliano, kwa sababu kila mkataba utakuwa unakuwa na timeframe yake
Jerry Kasema - Mkataba huu upo kisheria, umeingiwa kwa kurejea Vienna Convention.
 


Kipumbavu kweli
 
Jerry Kasema - Mkataba huu upo kisheria, umeingiwa kwa kurejea Vienna Convention.
Kama ni mkataba, DP World wamesha-invest kiasi gani kwenye mkataba huo? Mkataba usiokuwa na Value, ni agreement na hauko enforceable by law. Wakisitisha makubaliano hayo muda huu kwa mmoja wao kutoridhika, hakuna aliye na haki ya kwenda kushtaki mahakamani. Naongea hapa kama mtaalamu
 
Walio nunuliwa Hawa hapa na Jerry soma huu ujinga hapa.

Tulikuona wa maana kumbe mjinga tu kama mimi.
 

Attachments

  • B6292693-57CD-4FFD-ADD8-06269C377301.jpeg
    37.4 KB · Views: 1
  • CAB5C35A-A5E0-47A1-ADA7-9AC1D7CC294D.jpeg
    55.1 KB · Views: 1
  • DB8464B3-FC18-4BB2-B10C-B0EBEBA2C19D.jpeg
    75.7 KB · Views: 2
  • 60BC94CE-B7F0-4FC6-B34D-F6ECA0D935AC.jpeg
    131.1 KB · Views: 2
  • 3E759F10-8819-4DF1-AF8D-B5700319AF5A.jpeg
    150.5 KB · Views: 2
  • D65F6315-16E5-4167-89E8-A89694621929.jpeg
    55.3 KB · Views: 1
  • 7A8FC710-0ED5-4695-8139-C725C0979588.jpeg
    32 KB · Views: 2
  • 6966B8C2-C042-4048-AF5E-E2057579F7C6.jpeg
    58 KB · Views: 1
Bunge lina madaraka ya kuridhia makubaliano? Nijuacho, bunge lina madaraka ya kujadili mikataba, na si makubaliano
 
Serikalini kama unakiri imeshindwa kusimamia bandari mengine mtayaweza?

JPM ungeweza kumwambia eti unabinafsisha bandari au mnatutania?
 
Kijana yupo busy kutafuta Uwaziri huyu apuuzwe kama wengine haya mambo ya Vienna yanaruhusu kutoa ardhi yetu.
Slaa ni mmoja ya wabunge waliobebwa hakustaili kabisa kubeba jimbo hilo la ukonga ni wale wale wabunge vilaza wanaoshindwa kuisimamia serikali

Yeye kazi yake alishaimaliza bungeni anaongea nini tena nini tena namuona ni mtu mwenye hofu
 
Hata mollel ni dr lakini unaona mambo yake ?
 
Wewe na Mbunge Jerry nani anaujua huu mkataba zaidi ya mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…