Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lasitisha mafunzo ya kujitolea

Tumeficha korona sasa tunaficha na ukata wa fedha, kweli tunaongozwa na vilaza!
 
Natumai wapo kufanya tafiti na watakuja na majibu ya kuwa walelopitia hayo mafunzo je nifaida gani wameiachia Tanzania na Watanzania kwa ujumla ikiwa hiyo programu kama imeingiza faida itaendelea na kama itia hasara ndo bye bye.
 
Nashangaa sana kwanini Mtu anatoka jeshini halafu anakuja kuwa jambazi au kibaka wakati jeshini tunafundishwa nidhamu na uzalendo
Anza kumshangaa yule afande aliyekutwa na viroba na vitu vyenye ncha kali.
 
Mafunzo ya JKT yamesitishwa na wanafunzi wameambiwa warudi nyumbani, na wale ambao walikuwa hawajaripoti wameambiwa wasiripoti hadi hapo itakapotangazwa tena.

Je, ni sababu za kiuchumi, COVID-19 au?
 
Sababu ya kusitishwa mbona haisemwi?
 
Nidhamu na Uzalendo feki haulipi BILL.
Unataka nani akulipie bill mkuu.

Jeshini watu wanafundishwa pia ujasiriamali ukitoka hapo unaweza kuwa mkulima na mfugaji mzuri tu ila vijana wanataka waoneshane nani mbabe mjini hapa.
 
Uzalendo ni ukipata kilichokupeleka jeshini, sio upewe mafunzo kisha utelekezwe.
Jeshini watu wanafundishwa ujasiriamali pia mkuu ukitoka hapo unaweza mkulima na mfugaji mzuri tu

Kwanini mtu atumie mafunzo aliyopata ya kutumia silaha tu ila asitumie mafunzo aliyoyapata ya ujasiriamali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…