Jeshi la Urusi ni dhaifu sana, ni dhaifu mno


Okey,, iraq ilivamiwa na nchi ngapi? Na ikachukua muda gani, na mpaka leo nchi haijatulia!

Libya ilivamiwa na nchi ngapi?? Na ikawachukua muda gani??

Syria ilivamiwa na nchi ngapi?? Na ikaenda muda gani bila mafanikio?

Russia yupo alone bila msaada wa mtu, na pale ameenda kwa operation maalum,,na sio kuuwa watu hovyo kama wafanyavyo marekani na mashoga zake.
 
Russia ni Kama hamasi wao wanajua kurusha makombora.ndio maana anapiga makombora mpaka shule za chekechea.
 
Haya ngoja tuwape muda
 
Hana tofauti na N.Korea ndio maana mda wote anategemea hiyo nukes kujihami πŸ˜†πŸ˜†





 
huna akili na hujui kuwa ww ni tailaaa , mwanume timamu haeza shabikia uvamizi
 
adui ni nan alivamia au aliyevamiwa ?
 
Ndio mana Finland na Sweden wakaona muda ni sasa wa kujiunga na NATO baada ya kuona huu udhaifu wa Russia kwa nchi kama Ukrean, kabla Finland na Sweden walimuogopa Russia kama mdudu na wakati operation inaanza kule Ukrean Putin aliwaonya na finland wakasema hawana kabisa mpango wa NATO lakin juzi juzi wamesema hapana tunajiunga na NATO tena bunge lao sasa linajadili kujiunga na NATO asilimia kubwa wamekubali mpango
 
Jichanganye ukutane na m-russia, wana nguvu zaid ya unavyofikiria, pia wamepitia mafunzo ya kila namna, ila wao wanachofanya pia ni kukutia hasara na kupoteza taswira ya miji.
Nguvu ya m-russia ni ipi sasa mwezi wa 2 umekatika bado anapapatua donbas pembeni mwa ukrean na karibu anaelekea kufurushwa kabisa kabisa
 
Watu mna muda...

Yaan mtu anakupiga kila sehemu katika nchi yako bado unamuona dhaifu?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Ameuwa raia sana lakini vita strategically russia ametupwa mbali sana, mimi nikiisikia russia apo zamani niliwaza kuwa itakuwa na nguvu kuliko Marekani, lakini ni tofauti sana

Alipoivamia ukraine akatangaza majimbo ya Donbas kuwa huru halafu akaenda zake mbele Kyiv, ghafla sijuwi kapatwa na nini Kyiv ilimshinda karudia kule kule Donbas ambako saivi ndio anarusha mabomu ya mbali kuangusha majumba yaani tunapata shida sana kujua lengo la russia ni lipi lakini ni lipi amefanikiwa hadi sasa mwezi wa 2 unaingia wa 3.,
 
Wasamehe wanajeshi wa Urusi, sababu vifaa vyao vina tatizo la Teknolojia. Ni kwamba Vifaa vingi vya Urusi havina shabaha. Wanaweza kusema hili bomu litue bunju, likatua Goba. Ndo maana Katikati ya nchi Ukraine walikimbia. Waliona wanakufa wao tu. Sasa wameleta wanajeshi wa Kukodi

2. Wanajeshi wa Urusi hawana Uchungu na hii vita bali wanatii amri ya kijeshi matakwa ya Putin hivyo wakina wanazidiwa wanaondoka zao hata kabla adui hajafika. Hawa wa kukodia wao wapo Vitani sababu kila siku hela inaingia hivyo wanapiga makombora Ovyo ovyo ilimradi waonekane wapo kazini. Wanasema Ukraine tumewachakaza kumbe wamechakaz majengo. Kila Mtu wa Ukraine mwenye Nyumba ana Handaki chini ya nyumba, Ndo maana hapo wamebomoa nyumba zote hizo wakafa Waukraine nane tu
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sijui unaongea vitu gani, ila sio mbaya, umefanikiwa kuiponda Urusi, jukwaa huru hili.
 
sasa kama mnapigana kwa kujificha kwenye majengo yeye afanyeje kama sio kuyashusha majengo chini kama huko Allepo
 
Duh kumbe Russia Ni dhaifuuu?
Nchi inayoogopwa na Marekani kuliko nchi zote duniani?
Nb. Tafuta picha za Baghdad ya 2003 ya sadam. Na pia baadae tafuta picha za Baghdad baada ya 2003. Ndo utajua Kwamba adui atafutwapo haijalishi kasimama kwenye Mali ya thamani kiasi gani. Na ndo maana hata waukren wangepata nafasi wangeiflatisha Moscow ili tu kumtafuta Putin. Wazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…