Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Sana tu, katukana viongozi kimyaa, kamtukana Rais kimyaa, Kawatukana police kimyaa sasa anataka kutest maji, Nadhani atawataja walioko nyuma yake very soon. Ana act kama vile ndio kahamia Tanzania juzi wakati jitu lina miaka 60 huko. Nchi zote duniani watakosoana lakini siku zote wanalipa jeshi lao heshima hata kama kuna mapungufu. USA walisema hakuna mwanajeshi wao atashtakiwa kwa kuvunja haki za binadamu japo wao ni machampion wa mambo hayo. Israel alikataa wanajeshi wake kushtakiwa.. na wengine wengi. Hawa sio wajinga. Sasa huyu kafika sehemu anataka kuhatarisha amani ya nchi. shida hapa ukiwakashifu jeshi au police na wakakulia kimya unafungua mlango na kufunga itakuwa too late. Mshughulikieni huyu haraka.
Umeelewa chochote alichoandika Mwabukusi??
 
Wewe jamaa mbona unapiga mayowe yasiyo na maana?!!!

Hivi mtu akikushtaki wewe amekubagaza utu wako ?!!!

Kuna kitu hukielewi....

Mashtaka yanapokuwa mahakamani ni kwa ajili ya "integrity" ya tafsiri ya "rule of law"....

Taasisi inaweza kushtakiwa....mashtaka si uadui....hivi hizi "mentality" za KUKARIRI ujinga tunazitoa wapi ?!!!

Wewe hujawahi kusikia wazazi wa askari wa USA waliopelekwa Vita vya Iraq" walikwenda mahakamani kutaka tafsiri ya sheria kwa kilichoitwa "false flag"?!!! [emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]
 
Mwabukusi yuko sahihi kumiliki sare rasmi za jeshi ni uharifu na si kazi ya jeshi kuanza kudeal na uhalifu huo ila ni kazi ya jeshi la polisi hao wanajeshi wasijipe kazi ambaye ni kinyume cha majukumu yao waliyopewa kikatiba.It seems wamekosa kazi za kufanya siku hizi
[emoji106]
 
WAKILI MWABUKUSI ANATAKA MKUU WA MAJESHI AZUIE UVUNJIFU WA KATIBA.

"Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba. Kazi ya kukamata wa halifu ni ya Jeshi la Polisi. Jeshi la wananchi halina mamlaka kisheria na kikatiba kuingia kufanya msako mitaani kwa kisingizio cha kutafuta sare zao. Jukumu lao ni kulinda mipaka ya nchi. Cha ajabu hawajatuambia walizipeleka lini huko mitaani au zilichukuliwa na nani au waliibiwa lini? This is more than a comic [Huu ni usanii]!

Mwanajeshi hana mamlaka ya kupekua mtu katika makazi yake au maungo ya raia. Hii ni kazi ya Polisi wetu. Isipokuwa pale kunapokuwa na hali ya hatari au tishio dhahiri la mapinduzi.

Sheria inaruhusu kukataa ukamataji haramu na iwapo jeshi litaingia kwa namna hii ni haki ya wananchi kukataa ukamataji au upekuzi haramu usiofuata sheria ikiwemo kumshtaki Mwanasheria mkuu na Mkuu wa Majeshi ili kulinda sheria na Katiba ya Nchi na kudai fidia ya usumbufu.

Kama jeshi limeibiwa sare zake likaripoti Polisi. Polisi wafanye uchunguzi na wakibaini kosa Polisi ndiyo wenye utaalamu wa kupeleleza uhalifu wa wizi. Jeshi au wanajeshi hawako juu ya sheria [hivyo] wapunguze mihemko.

Kumekuwa na ujasiri wa uvunjaji katiba na sheria na kuwatisha wananchi katika taifa letu katika uongozi huu wa sasa na kwa hili hatutakubali na tutalitolea tamko rasmi kupinga vurugu hizi katika utumishi wa umma.

Mkuu wa Majeshi awajibike haraka kuzuia ukora huu wanaotaka au kupanga kuufanya!

Najisikia aibu sana kuishi na kushuhudia viroja hivi. Mungu bariki Watanganyika! Mungu ibariki Tanzania! Mungu waadhibu na kuwakemea madhalimu wote.

Boniface Kajunjumele Mwabukusi!
Jeshi ni kama vile linaona raia ni waasi.

Je kwenye mafunzo yao wana kipengele cha kuzuia na kupambana na uhalifu?
 
wewe na ukoo wako hakuna siku mtajikomboa
Anayejikomboa hajifichi toka wazi wewe kama nani toa ID fake ndio tutajuwa uko serious. Bora ya huyo Mwambukusi anasema kama yeye naweza kumpa heshima. Wewe unajitia shujaa mbona umejificha kama sisi nyuma?
 
Mnaleta utani kwenye ulinzi wa Taifa, acheni upumbavu tutawafuata majumbani uniform za jeshi ni haramu kutumiwa na raia
Upumbavu detected kwenye hii post hapo juu
 
JWTZ wameshimu "rule of law"...

PT wako kikatiba kuzuia na kupambana na uhalifu....

Kumiliki sare za majeshi kwa wasiohusika huo ni UHALIFU....

Mwabukusi yuko sahihi....

JWTZ tunawakumbusha msimame katika mstari wenu.....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Ni vizuri upitie sheria za jeshi ujue military polisi ana wajibu gani na wakati gani anaweza fanya majukumu yake. Na majukumu yake nipamoja na nini. Natumai uwezi niuliza tena hilo swali!

Jeshi (JWTZ) lipo kwa ajili ya raia. Halipo kwa ajili yake binafsi. Lipo kulinda amani ya nchi na mipaka ya nchi. Sasa ikitokea uniform za jeshi zimeenea mtaani unadhani nini kinafuata?

Nimeishi Ethiopia, uniform za polisi ilitokea zikaenea sana kwa raia. kuna muda ilikuwa ngumu kutambuia polisi halali ni yupi kwa kuangalia. Hii ilileta madhara makubwa ktk amani ya nchi.

Walichelewa kuchukua hatua hivyo ilibidi wabadili mavazi ya jeshi la polisi nchi zima. japo madhara yalikuwa tayari yameisha tokea.

Kazi ya polisi ni maswala ya jinai na si vinginevyo.

Ebu nitajie kifungu cha sheria za jinai kinachoeleza kukutwa na mavazi ya jeshi la wananchi. Hapo ndo utajua kuwa unapokutwa na magwanda ya jeshi ufikishwi mahakamani. Bali magandwa ya JWTZ ni mali yao wanachofanya ni kuyachukua na kurejesha kwao.

Kwa maswala ya amani ya nchi ebu tuache siasa na ushabiki. Waacheni jeshi wafanye zoezi la kurejesha magwanda yao. Na uzuri wameomba watu warejeshe wao wenyewe.

Ila wale wabishi ndo wao jeshi watawafuata majumbani au kokote waliko kuyarejesha. Shida hiko wapi?
Unaelezea uzoefu wako wa nchi mbalimbali kwa ajili ya kujibu swali la matumizi ya military police kwa raia!! Nikikwambia uzoefu wangu pengine hutarudia tena kujibu swali namna hiyo. Mafunzo na weledi wa Jeshi lo lote katika nchi inayoendeshwa kidemokrasia hayaelekezwi kwa raia. Raia ye yote ambae ana afya na mzalendo ni jeshi la akiba endapo nchi inaingia vitani. Nadhani ulikuwepo na ulikuwa unajitambua yaliyofanyika Tanzania ilipombana na Idd Amin wa Uganda. Kwa sababu hiyo nguvu za jeshi kwenye nchi yo yote inayojitambua na inayothamini utawala wa sheria haiwezi kuelekezwa kwa jeshi lake la akiba. Suala la sare za Jeshi lishughulikiwe na polisi vinginevyo ni kulidhalilisha wanajeshi wetu na jeshi lenyewe. Serikali ilikuwa wapi mpaka sare za jeshi zinazagaa? kama zinakuja kama mitumba au zinaagizwa au kushonwa hapa nchini Serikali ndiyo inaweza kuwachukulia hatua wahusika. Governance! Governance. Governance!
 
Umemaliza kila kitu....

Asiyeelewa ulichosema basi tumsaidie kumkamata ,kumfunga kamba na kumuwahisha pale wodi na.14 ACUTE MIREMBE [emoji1787][emoji1787]
 
Unaelezea uzoefu wako wa nchi mbalimbali kwa ajili ya kujibu swali la matumizi ya military police kwa raia!! Nikikwambia uzoefu wangu pengine hutarudia tena kujibu swali namna hiyo. Mafunzo na weledi wa Jeshi lo lote katika nchi inayoendeshwa kidemokrasia hayaelekezwi kwa raia. Raia ye yote ambae ana afya na mzalendo ni jeshi la akiba endapo nchi inaingia vitani. Nadhani ulikuwepo na ulikuwa unajitambua yaliyofanyika Tanzania ilipombana na Idd Amin wa Uganda. Kwa sababu hiyo nguvu za jeshi kwenye nchi yo yote inayojitambua na inayothamini utawala wa sheria haiwezi kuelekezwa kwa jeshi lake la akiba. Suala la sare za Jeshi lishughulikiwe na polisi vinginevyo ni kulidhalilisha wanajeshi wetu na jeshi lenyewe. Serikali ilikuwa wapi mpaka sare za jeshi zinazagaa? kama zinakuja kama mitumba au zinaagizwa au kushonwa hapa nchini Serikali ndiyo inaweza kuwachukulia hatua wahusika. Governance! Governance. Governance!
[emoji2956][emoji2956][emoji2956]
 
Kama vita hamna,futeni JESHI hilo tubaki na majeshi mengine kuokoa gharama za matumizi yasio na lazima.

maana kazi hamna majeshi yameanza kusaidiana majukumu. sio mbaya lkn labda ni upendo.
 
Majeshi yenye akili yanapindua serikali mbovu na kufanya research zenye tija.

Jeshi letu tatizo wamejaa viraza wao wanadhani wakivaa mabaka yao wamemaliza kazi. Namuunga mkono Mwambukusi, hao wahuni waache mara moja mpango wao wa kijinga.
 
Back
Top Bottom