Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Baada ya kuwa umeshaagiza mzigo wako unapokea kwa njia ipi???na hawa ebay ofisi zao hapa dar au dodoma ziko wapi???
Mzigo unapokea kwa njia posta, unaenda kuufata posta na kama utahitaji kufanyiwa valuation na Customs TRA utajulishwa. Na kuna wengine wanatuma via DHL au Fedex au EMS au China Post and so on depends na muuzaji. Ila wengi ebay naona go for cheaper options ambazo ndio za postal address boxes(posta) kama una mabavu na unahitaji mzigo wako kwa uharaka unaeza tumia Amazon au ukaagiza kitu kupitia Easybuy Africa ofisi zao zipo Dar wao ni concierge service ila kama hutaki mfuko utoboke unaenda kusurvey ebay. Tho soko limekua saturated sana kupata vitu vya quality nzuri na kwa gharama nafuu imekua kazi. Sahivi Quality is expensive.
 
Mzigo unapokea kwa njia posta, unaenda kuufata posta na kama utahitaji kufanyiwa valuation na Customs TRA utajulishwa. Na kuna wengine wanatuma via DHL au Fedex au EMS au China Post and so on depends na muuzaji. Ila wengi ebay naona go for cheaper options ambazo ndio za postal address boxes(posta) kama una mabavu na unahitaji mzigo wako kwa uharaka unaeza tumia Amazon au ukaagiza kitu kupitia Easybuy Africa ofisi zao zipo Dar wao ni concierge service ila kama hutaki mfuko utoboke unaenda kusurvey ebay. Tho soko limekua saturated sana kupata vitu vya quality nzuri na kwa gharama nafuu imekua kazi. Sahivi Quality is expensive.
Na mzigo unapokuwa njiani naweza u-track
 
NAUZA BIASHARA YA CAR WASH:

LOCATION: KINONDONI BLOCK 41
NAMBA YA SIMU: 0717 26 33 77

MAELEZO:

MACHINE ZOTE, UJENZI, VYOMBO, SIMTANK, KODI n.k JUMLA: TZS 7,000,000
NIMEBAHATIKA KUPATA KAZI SERIKALINI NA KITUO CHANGU KIKO MKOANI, SO NIMEAMUA KUUZA HII BIASHARA.
 
Niliona kuna bidhaa kama memory card nyingine min order ni 10 je nafanyaje nafanyaje kwasababu walinambia wanamtaka ajenti wa AirCargo na mm sielewi naweza nikampata vp?

tumia unique aircargo china to tanzania 0758656656
 
Wajuzi wa Alibaba naomba mnijuze hapa Bei halali hapa ni ipi maana naona Kuna tsh 9956 , na Tsh 60285
Screenshot_20210521-223206.jpg
 
Mkuu 1800, wamarekani hawatumii EMS nadhani, wao wanatumia USPS ambayo kwa tz mzigo utashughulikiwa na local post office, kwa maana ya tanzania post corporation, hasa kitengo cha EMS ndio watakao kupatia mzigo wako.

Nimeeleza hivyo, baada ya kunitokea mimi kitu hicho, niliagiza pea ya kiatu toka states seller akasema shipping ni kupitia USPS na ilikuwa na tracking number, na hata mzigo ulipofika nikaenda EMS na tracking number yangu na kupewa mzigo na kulengeshwa kwa watu wa customs kuwa natakiwa kulipia ushuru.

Nawakilisha
Ulitozwa Ushuri bei Gan Na EMS na Mzigo ulikuwa una uzito gan
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?

Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop the US Online and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT
Naomba kujuzwa Hivi Hakuna Hayo makampuni ya Usafirishaji yaliyoko India,Kwa sisi Tunaotaka Kuagizia Mzigo Kutoka India kuja Tanzania
 
Kwa wazoefu wa kununua bidhaa kutoka Alibaba au Ebay nielekeze inakuaje na gharama zipoje mpka nipate mzigo wangu.

Nataka kununua flat screen alibaba nimeona bei zao ni rahisi sana, anaefahamu anieleweshe kidogo hapo.
 
Kwa wazoefu wa kununua bidhaa kutoka alibaba au ebay nielekeze inakuaje na gharama zipoje mpka nipate mzigo wangu.
Nataka kununua flat screen alibaba nimeona bei zao ni rahisi sana,anaefahamu anieleweshe kidogo hapo.
Alibaba wanauza vitu kwa jumla. Yani kama unataka pc 100 au 1000 hivi..

Angalia aliexpress ndio wanauza kwa bei rejareja
 
Pia naomba kujua ni carrier gani wa uhakika unaweza mtumia kama ukinunua kitu alliexpress unaweza upata mzigo wako bila longolongo yoyote
 
Kwa wazoefu wa kununua bidhaa kutoka alibaba au ebay nielekeze inakuaje na gharama zipoje mpka nipate mzigo wangu.
Nataka kununua flat screen alibaba nimeona bei zao ni rahisi sana,anaefahamu anieleweshe kidogo hapo.
Ila kua Makini Mkuu,
Mwengine mnachart kupitia Alibaba/Aliexpress anaanza kukuomba Contacts za Whatsapp au email. Ukijitusu tu ukampatia means mnahama kutoka Alibaba/AliExpress kuhamia maongezi binafsi ambako huko ndo unaenda kupigwa. Hao wa bei chee ndo wapigaji hao. Hukawii kukuta PS5 kwa US$100.00 tena unatamanishwa Buy 2 get 1 extra free
 
Ila kua Makini Mkuu,
Mwengine mnachart kupitia Alibaba/Aliexpress anaanza kukuomba Contacts za Whatsapp au email. Ukijitusu tu ukampatia means mnahama kutoka Alibaba/AliExpress kuhamia maongezi binafsi ambako huko ndo unaenda kupigwa. Hao wa bei chee ndo wapigaji hao. Hukawii kukuta PS5 kwa US$100.00 tena unatamanishwa Buy 2 get 1 extra free
Nited.thanks
 
Kuna vifaa vya maabara havioatikani tz huwa natamani kuviagiza nje ila nashindwa
 
Back
Top Bottom