Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

ndugu zangu watanzania tungekuwa muda mwingi tunashare mada kama hizi na kujadili na kupeana mawazo badala ya kufuatilia mambo ya DIAMOND na WEMA tungekuwa mbali sana nashukuru sana uzi huu umenipa mwanga na nimeagiza bidhaa nyingi sana na zote zimefika hamna hata moja isiyofika

Umetumia campany gani kukuletea ?
 
Inamaana sikuhizi paypal wakirudisha hela inaingia kwenye acount tena? sababu hapo juu mliwahi kusema kwamba wakirudisha hua account bado haipokei kwamba tz bank hazina uwezo wa kupokea. hebu weka wazi vizuri hapa mkuu

Mdau hapo juu alisema kwa upande wa crdb, lakin barclays hakuna kusuasua
 
Account ya bank utakayotumia kujiunga na paypal ni lazima iwe ya USD au hata ya kibongo inafaa?

hata ya kibongo ila kuna changamoto fulani hivi. kuna ufafanuzi wa kina sehemu fulani ebu soma mwenyewe uone kuhusu swali lako hilo, soma website hii http://www.kalumbilo.co.tz/fahamu/fahamu_0006.html
 
Mkuu umefanya kazi nzur sana, vp kuhusu malipo ya ushuru kwa hapa kwetu?, yan mzigo ukifika vp kuhusu TRA?

Mkuu kuhusu ushuru TRA inategemea aina ya mzigo uliouagiza upo kwenye category gani. Huenda upo kwenye "zero rating" au "exempted supplies".

Kama mzigo upo kwenye exempted hautalipa ushuru wote ila VAT tu. Mifano ya subcategories ambazo zipo chini ya exempted supplies ni kama:
1. Food and crops
2. Pesticides and fertilizers
3. Educational supplies
4. Veterinary supplies
5. Transport services
6. Computers
7. Agricultural equipments nakadhalika.
Kwa hiyo utaangalia mzigo wako upo sehemu gani, huenda na computer au spea zake hiyo ipo pale kwenye namba 6. Au labda ni incubator, hiyo ipo kweny namba saba. Kwa hiyo ipo hivyo.
Kama mzigo wako haupo kweny category ya zero rating au exemped basi jiandae kulipa ushuru ufuatao.
1. Import Duty 25%
2. Excise duty 5% au 10%
3. VAT 20%

Kwa kifupi ni hayo. Ukitaka kujua mambo mengi zaidi kuhusu kuuza au kununua online, tembelea tovuti ya kiswahili inayotoa elimu maalumu kwa mambo haya
www.kalumbilo.co.tz/fahamu/
 
Wanajamvi, nimevutiwa sana na mada hii, lakini nadhani bado kdogo nahitaji kujua zaid. JZHOLO, Njunwa Wamavoko na wengne weng wenye weled wakina katika manunuzi kwa njia ya mtandao, tafadhar natamanim kujua maana nahitaji kununua na mm. e-mail yng josephchiwango@gmail.com, simu ya kiganjani 0712 698867. Tafadhali naomben msaada.

Pamoja na msaada utakaopatiwa na wataalamu uliowataja hapo, na mimi nimeona nijitokeze maana ni miongoni mwa watu wenye weledi. Nakualika tembelea tovuti maalumu ambayo inatoa miongozo mingi ya namna ya kuuza na kununua online.

Ni Tovuti ya kibongo na mada zimeelezwa kwa kiswahili, fungua hapa www.kalumbilo.co.tz/fahamu/
 
Wakuu nahitaji kusaidiwa namna ya kununua kwa hawa jamaa pamoja na masuala ya kusalama ya kuzingatia.

Asante.

Kama umeshajisajili, tafuta bidhaa unayoitaka kwa 'Gold suppliers' tu! Kama mitandao mengine yote, kuna matapeli pia. Baada ya negotiations nakushauri ulipe kupitia 'Alipay' (inachaji kidogo lakini inakuhakikishia usalama wa hela yako).

Kwa maswali zaidi kuna online customer service kwenye website yao, ukifata maelekezo yao huwezi kutapeliwa.
 
Ngoja waje wauza vitu feki watakujuza mkuu

Hahahahaa, wabongo tuna tabu sana! Jamaa kaomba msaada huna la kumsaidia kaa pembeni, lazima u-comment?
Hapo ulipo juu mpaka chini umevaa hivyo ulivyouziwa na 'wauza vitu feki'. Acha dharau dogo..
 
Wakuu nahitaji kusaidiwa namna ya kununua kwa hawa jamaa pamoja na masuala ya kusalama ya kuzingatia.

Asante.

Unawatumia tuu hela then wao wanakutumia kitu unachotaka hadi nchi uliyopo. Hawawezi kukuibia.

Ikiwa unachotaka kununua ni kitu kikubwa na cha gharama, nakushauri unicheki nikupe mtu afanye hiyo. Lakini uwe tayari kulipia.
 
Najaribu kuingiza adress yangu ya comgateaway ebay inaniletea hizo error. Help please.
1432976015791.jpg
 
Najaribu kuingiza adress yangu ya comgateaway ebay inaniletea hizo error. Help please.

utakuwa umekosea, watumie email comgateway uwambie wakusaidie ujue postal au zip code ni ipi watakuelekeza.
 
Hivi kuagiza camera mfano canon 5d na kisha utumie njia ya posta ya kawaida si risky kubwa sana?
 
wadau naombeni msaada kidogo hapa, nimefanya shopping amazon kwa kutumia anuani ya comgetway, na baada ya kujaza kila kitu, hapa mwisho kabisa amazon wameniletea order total tshs 170000, je hii fedha ina include shipping kutoka comgetway mpaka hapa bongo? au inabidi niwalipe tena comgetway kunifanyia shipping mpaka hapa bongo.

ASANTENI
 
Wajamvi kuna hii campuni ya china post air mail, naona inafanya free shipping from china to tanzania, vip inauhakika wa kupokea mzigo?
 
wadau naombeni msaada kidogo hapa, nimefanya shopping amazon kwa kutumia anuani ya comgetway, na baada ya kujaza kila kitu, hapa mwisho kabisa amazon wameniletea order total tshs 170000, je hii fedha ina include shipping kutoka comgetway mpaka hapa bongo? au inabidi niwalipe tena comgetway kunifanyia shipping mpaka hapa bongo.

ASANTENI

HAPANA mkuu, hiyo ni order total ya amazon. amazon wao ndio wataship kwenda kwenye address ya comgateway.. baada ya hapo mzigo wako utatumwa na amazon kwenda comgateway, wao comgateway watakutumia email wakipokea mzigo wako.. hapo ndio utapatiwa bei ya kutuma mzigo kuja tanzania..
 
nafulah san kupata mambo kam haya kwan ndio mla yang ya kwanza nimejifunza jap kiuchache2 nahitaji kujifunza zaid ili niwe miongone mwatu wngine zaid tunaweza kuwasilian kwa simu ya kiganjan 0655186071
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo. Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni 1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address 2:Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania) 3:Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1:CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2:KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3:KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4:KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?
hii iko hivi.... 1:Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted. 2:Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.comhii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.
Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao
Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2:COMGATEWAY
link-http://comgateway.com/ hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na uona wana policy nzuri sana,cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani,hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3:BORDERLINX
link- Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4:SHIPITO
link-USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5:STACKRY
link- Stackry - US shopping, global shipping hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi. STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU please evaluate kindly.

nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi . maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila ithink there r limits.. help Mwl.RCT

Mkuu umezungumza vizuri kuhusu kununua (Import) ila hujasema lolote kuuza bidhaa Amazon kwa FBA kutoka Alibaba. Nina uhakika kwa jinsi ulivyoeleza hata kuuza unajua. Sisi wengine tunajua ila kuelezea inakuwa shida kweli. Tafadhali wajulishe na jinsi ya kuingia kwenye soko kubwa Dunia linalouza karibia $100 Billion kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom