Battor
JF-Expert Member
- Mar 21, 2019
- 2,208
- 3,986
Upande wa ubora kiuchumi kati ya Mwanza na Arusha yote yana ubora tofauti kwa vipendele vifuatavyo;
Wigo mpana kwenye sekta za biashara, Kilimo na Uvuvi; Mwanza inaongoza kwani biashara zinafanyika sana zaidi ya Arusha ukizingatia ni kitovu cha mikoa ya kanda ya ziwa pia kupitia ziwa Victoria mwanza inaunganishwa na nchi jirani Kenya na Uganda. Hii inaleta wepesi wa kufanya biashara kwa kununua na kuuza bidhaa kwa hizi nchi za jumuiya ya E.A kwa urahisi zaidi. Arusha inapokea watalii na wageni wengi zaidi ya Mwanza, sekta za Utamaduni, Hoteli, sekta za Ulinzi na Utalii zinafanya vizuri sana mbali zaidi ya Mwanza.
Rasilimali watu wa Mwanza ni wachapakazi hapa inajumuisha jamii ya watu wa kanda ya ziwa pamoja na mikoa ya Kigoma na Tabora vijana wengi kwa kiasi kikubwa hufanya shughuli zao wakitegemea huu mji kibiashara hapo inapelekea population kuongezeka jijini Mwanza pia uzalishaji na mzunguko wa pesa kuongezeka.
Pia gharama za Maisha (Malazi, Chakula, Usafiri) Mwanza ziko chini ukilinganisha na Arusha mtu wakawaida anazimudu tofauti na Arusha huu ni mji wa kitalii kwaiyo inapelekea Maisha kuwa juu zaidi.
Mji wa Mwanza na Arusha kwenye upande wa usalama ni tofauti kidogo, Wezi na Vibaka wa Mwanza wapo tofauti na wa Arusha. Matukio ya uhalifu wa kutumia silaha Arusha iko juu ya Mwanza. Hii pia ina athari kwenye uchumi.
Bonus: Mwanza upande wa vyakula ina vyakula vingi sana na vinapatikana kwa bei nzuri ila upande wa kuandaa na kupika Arusha wako vizuri zaidi ya Mwanza.