Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 73,773
- 102,126
Wale ambao tunawasiliana PM na tumebadlishana namba tutaendelea kuwasiliana tuko pamoja, ila niseme biashara ya Uber ilinipa mafanikio sana na mpaka sasa naendelea kunufaika.
Mkuu kwa niaba na heshima ya waungwana wote tuliokuwa pamoja nawe kila hatua, nakuomba umalizie mkuu...
Wabongo wengi hawajaumbiwa uvumilivu lakini wewe kupitia stori hii katika hayo unayoyasimulia yaonesha ni mtu mvumilivu, hivyo wapuuzie wanaosema ni chai...
JamiiForums na Maxence Melo kama kuna uwezekano, wekeni functionality kwa mleta mada kuwa na uwezo wa ku-admin uzi wake ikiwemo kuban au kuhide uzi wake kwa baadhi ya watu...
JF ya sasa ina tabaka fulani la watu wenye kujawa na matusi, kauli mbaya mbaya, kujihesabia haki na wote wa namna hiyo...