Mkuu Mimi wakati nimemaliza chuo nasoma CPA, nilikuwa naendesha Uber. Nimeendesha Uber kwa miaka 2. Dereva Uber ukiwa msomi, unajua kiingereza, una gari Kali, halafu dizaini ukionekana unafanana nao kwa maana ya elimu, sio maskini kivile (nilikuwa naishi goba kinzudi maghorofani), na una exposure ( Mimi nilisoma IFM) utakula sana maisha. Maana wateja wa kishua kwanza watakuheshimu na watakuamini sana.
Mimi nilipewa mpaka madili ya kwenda china na wateja.
Nimealikwa kwenye events za kifamilia na wateja wakike kama harusi, birthday party na nimewahi kupewa mwaliko na mbunge mmoja niende kwenye vikao vya bunge nikitaka kwenda bungeni baada ya kuongea naye na kuniona Nina interest na mambo ya siasa, na huyo mbunge nilimpakia kwenda airport, ndio tukafahamiana.
Nimewahi kuingia nyumba ya tajiri mmoja mkubwa sana tena sana kwasababu tu mtoto wake wa kike alikuwa mteja wangu.
Nimewahi kualikwa kwenye kutoa sadaka ya shukrani kanisa la UCC upanga na mke wa mkurugenzi mkuu wa shirika Moja kubwa la serikali, na kutambulishwa dereva wangu, jioni nikajumuika mbezi beach kwenye chakula Cha jioni, huyo mke wake tulijuana kwenye Uber.
Niliwahi kumpakia dada wa TBS anayeishi kota za TBS mikocheni pale karibu na kwa Mwinyi, yule dada ni mhasibu tukaja kutengeneza bond kubwa sana mpaka Leo, sasa wakati nakaribia kufanya mitihani ya CPA akaniambia njoo tukae wote mikocheni ili nimsaidie maana alinikubali sana, ndani tukawa tunaishi watu watatu tu, Mimi, yeye na mdogo wake, angekuwa tuna umri sawa ungenikuta ni shemeji Yako now, sema amenizidi kama Miaka 8 hivi, nimeishia kumfanya dada, ila mpaka Leo nikitaka kulala pale kota za TBS nalala.
Na kwasababu nilikuwa naishi Goba kinzudi maghorofani request zangu za asubuhi ilikuwa lazima ziwe goba, mbezi makonde, mbezi afrikana etc
Kuhusu kupeleka wanawake kugongwa hilo nimelifanya sana, nimewapeleka sana hotel za hapa bongo, nje ya mji bagamoyo, morogoro na kuwasubiria na kurudi now, anakupigia gharama za kwako kwa siku, mzungu analipa. Ni kawaida sana.
Kuhusiana na tenda za kupeleka watoto shule nilipataga hiyo tenda kupeleka watoto Kila siku pale Liberman, kuhusiana na kupeleka mtu kazini nilipataga ya kumpeleka mdada kazini asubuhi daily. Huyu dada ni mfanyabiashara wa kariakoo aliwahi ku-process mkopo bank ya access mil 80, ili aende kufuata spare za magari china, na siku hiyo alichomoa mil 20 alitaka kuongeza working capital dukani mil 10, na mil 10 akaenda kumalizia installment ya mwisho ya kiwanja hukohuko goba ili apate hati, na pesa hiyo mil 10 nilikuwa nayo Mimi kwenye gari, na kwenye kukabidhi Mimi ndio nilikabidhi na nikasaini mkataba wa mwisho wa kumalizia installment, ( Leo hii Mimi ndio namwandalia financial statements za biashara zake ) Huyo dada alikuwa ananishirikisha utadhani Mimi ndio mume wake, kumbuka ameolewa na ana watoto wawili. Kila safari ya china akienda airport na akirudi Mimi ndio nilikuwa nampeleka, ndio huyu akataka nijipange nianze kwenda china.
Hapo sijazungumzia connection za foreigner wakikujua wewe ni msomi na unajua vizuri kiingereza. Nimewahi kwenda mbuga za wanyama na foreigners wawili.
Narudia tena, dereva wa Uber ukiwa
[emoji3581] Unajua kiingereza
[emoji3581] Una elimu nzuri
[emoji3581] Ukionekana sio mswahili , ila ni lower-middle class economy.
Hayo mambo aliyoyasema
INSIDER MAN utayaamini