Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Hii ni story tu kama ya zari la mentali lakini haina uhalisia kabisa sema tu kujipoza uan uchungu wa maisha.. Story inafurahisha watu wanavuta picha wanaona wako South na dem mzuriii.... Lakini akili yao Inashindwa kuchanganua akina ya mtu anayeongelewa
Ww n Fanta tu mmoja
 
Mkuu huyu jamaa kwa maksudi anapotosha watu humu. Hakuna sehemu mimi nimesema Khumbu alikuwa anagongwa na madereva wa daladala. Khumbu alikuwa amezaa na boss wa daladala. Maana hiyo kama mtu anamiliki daladala kwa nchi kama South africa maana yake ana hela za kutosha. Sasa mtu ni mfanyabiashara wa daladala utasema hana hela? Jamaa kaniangusha sana. Anaharibu uzi wangu huyu mwamba.
Kuna watu wengine ni chawa tu so uwe unawakaushie tu.watu tunasoma story wao wanaleta ushamba .ujuaji na ujanja mavi[emoji777][emoji706] ebhanaa ukiona hupendezwi na story lala mbele kimya kimya
 
Kuna watu wanasema hii stori ni chai kwa kutokuamini kwamba Mayor hawezi kumdate Khumbu. Jamani kwanza Mayor ni diwani tu (local concilor) kama alivyokuwa Baba Levo wa Wasafi. Baba levo alikuwa diwani wa Kigoma hivyo baraza la madiwani lingeweza kumchagua kuwa mayor. Kwa hiyo mayor ni mtu mdogo tu. Pili wanasiasa wa nchi za wenzetu hawana makuu kama wa kwetu huku. Huyo mayor, binafsi namfahamu. Alikuwa ananyoa kwenye saluni ya mshikaji wetu mburundi. Kinyozi wake ndio alikuwa pia kinyozi wangu. Kwenye hiyo saluni tulikuwa tunanyoa bure tu. Mnamkumbuka yule mburundi tuliyekuwa tunaishi naye kule Rossburg pamoja na baba Isa? Huyo mburundi alikuwa ni mmojawapo wa vinyozi wa hiyo saluni.
Mayor wa zamani wa la Jiji London Kenn Livingstone alikua anaenda kazini kwakutumia Underground train(Tube) Tena kituo alichokua anapandia treni inakua imejaa so alikua anasimama anashika bomba mpaka anaposhuka.

Prime Minister wa zamani David Cameron kabla hajawa PM na Chairman wa Consevertive Party alikua anaenda kazini kwa kuendesha baiskeli
 
But still ni mayor... Haileti sense. Kabisa. Yaani mayor wa jiji la Durban akawe na chokoraa asiweza hata kujinunulia breakfast ya mama mtilie. Yaani mayor ana share dem na wauza mitumba? Yaani kibongo bongo ni mayor wa Dar ana share dem na wauza mitumba wa karume. Huku kapaki v8 lake. Kwanza huyo mayor anakutana wapi na kidemu kama hicho. Mayor wa jiji la Durban sio mchezo wandugu... Anyway watanzania tumezoea kudanganywa. Its ok
Mkuu mbona unakuwa hivi? Hujui mapenzi wewe kuwa hayataburiki? Kwani mayor ni nani?
 
Halafu huyu jamaa anayejiita Hesabu900 ni bonge la mshamba. Mayor ni diwani tu (ward councilor). Na yeye ni binadamu kama wengine na anavutiwa na pisi kali pia. Mayor alikuwa anakuja workshop kupiga misele kama raia wengine tu japo alikuwa na body guard. Kwa hiyo pisi kali kama Khumbu akikutana nayo kitaa lazima aiimbishe. By the way South africa kuwa na gari sio issue, kila mtu mwenye kipato au mwenye kazi ana gari. Hata hao anaowaita wauza mitumba wa Karume wanauza mitumba huku wamepaki magari ya maana pembeni. Mwambieni aache ushamba, Khumbu kuwa na gari sio big deal, angeweza hata kujinunulia mwenyewe kama angetaka. South africa wanatengeneza magari na kuna hela ya kutosha mpaka vijijini huko. Huko vyuma havijakaza kama huku bongo. Kifupi South africa kuwa na gari sio issue. Karibia kila familia ina gari. Hiyo exposure anayoiongelea sijui ni ipi kama anaona mayor kutembelea V8 ni kitu cha ajabu kwa nchi kama South africa. Shame on him!
Huyo jamaa hesabu900 ana element za Dokta shika, kwhyo tumpotezee tu.
 
Aisee Leo nimejifunza kitu kikubwa Sana kupitia comments za wadau juu ya kukatishwa story. KUFIKISHWA KILELENI. Hili Ni Jambo la msingi Sana Sana. Kumbe inahitajika kwa gharama yoyote Uhakikishe Mwenzio kafika KILELENI vinginevyo Ni kuzalisha Vita kubwa Sana. Kaka mkubwa Baharia wa kwa Madiba@Konda msafi Tafadhali pliz tufikishe KILELENI ona jinsi tunavyohangaika. Kama uliweza kumwangaikia Shemeji yetu Khumbu kiasi kile basi na siye twakuomba tufikishe mkuu
pia mim nmejfunza,n kwa namna gan wanawake hupata maumivu ya kutofikishwa kilelen
 
Back
Top Bottom