Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Waulizeni mods kama inaruhusiwa kutupia picha ya mtu hapa. Kuna moja nataka niitupie yupo na bikini tu. Tulikuwa kwenye swimming pool. Wale masela niliokuwa naishi nao waliingia kwenye business ya sembe hivyo hela ikawa sio shida tena tukahamia kwenye nyumba bab kubwaa yenye swimming pool na kila kila kitu ndani, maeneo ya watu wanene.
Mm ni adm mpya....tupia fasta nakuruhusu
 
Jamaa ananiumiza sana ....nimetumikia taifa usiku mzima..nimelala kidogo tu notifications za uzi wake asubuhi zimeniamsha.


Nataka kulala muda huu anasema anatuma picha.

Atume basi watu tumuone khumbu.
Lala muda huu maana lindo la usiku sio mchezo
 
Tupia tunakusuhiri....mm adm nakuruhusu tupia picha fasta
 
Nilitegemea muda huu utakua umejipumzisha! Anyway naingia road, ikitokea jamaa katupia picha sipo hewani I download kabisa kabla mods hawajafanya yao then tutashare hiyo picha., samahani lakini!
Pamoja sana mzalendo mwenzangu .
 
Inaendelea,
Nikiwa nimepigwa na butwaa nikijaribu kutafakari nini kinaendelea hapa baada ya kile kidirisha kupasuliwa ikaingia msg kwenye simu yangu. Hapo natamani msg yoyote au simu yoyote itakayoingia iwe inatoka kwa Khumbu. Kweli nilopoifungua hiyo sms nikakuta "Please call me' kutoka kwa Khumbu. Roho ikalipuka kwa furaha. Kabla sijampigia nikawa najiuliza maswali mengi mengi. Kwanza nikawa najiuliza kwa nini simu yake alikuwa hapokei na baadae kuizima kabisa? Je nimwulize? Roho nyingine inaniambia "ukimwuliza tu unaweza kusababisha songombingo kama la siku ile ukajikuta tena umemuudhi akamua kukupotezea tena, ukajikuta tena unahangaika kumbembeleza. Hapa sijamtia machoni wiki sasa inaisha. Nikimtibua tena kwa maswali ya kishari shari si inaweza kwenda wiki ya pili tena kabla hatujaweka mambo sawa? Idea ya kuanza kumhoji nikaipotezea.

Concern nyingine ni hiki kidirisha kilichopasuliwa, je akija akute haya mazingira, atakubali kuliwa kwenye hiki chumba? si ataniona naishi kimaskini sana? Je, haitakuwa ndio mwanzo wa kunipotezea mazima? Anyway nikaona acha nimpigie tu then nisikie anasemaje.

Nikachukua simu, nikascrow jina lake nikabonyeza kitufe cha kupigia simu. Hapo nimekuwa mpole balaa hadi akauliza alipopokea simu why I sound like that? Alipopokea simu akaniuliza "mjengoni kuna mtu, nipo kwenye taxi nakuja? Ilikuwa ni kawaida yake kuja moja kwa moja getoni kama kupo wazi, namaanisha kama kuna mtu. Kama hakuna mtu alikuwa na kawaida ya kupita workshop kuchukua funguo na kutangulia getoni. Jioni nikirudi namkuta tayari keshapika na yupo poa kabisa. Hivyo alivyouliza kuna mtu geto, nikamwambia leo nipo tu nyumbani wewe njoo moja kwa moja. Kwanza alishangaa kusikia nipo nyumbani kwa mida hiyo maana nilitakiwa niwe workshop, pili tone yangu ya upole na majonzi aliihisi hivyo akauliza "Babe what is the matter? Why you sound like that?" Nikamjibu "babe I'm missing you terribly". Akajibu, "I'm on my way my love, see you just now". Baada ya kukata simu nikawa na furaha kichizi. Ila swali likabaki, hii hali ya hiki chumba itakuwaje?

Wale mademu wa Isa wakawa bado wanachambana. Huyu mwingine anamtaka mwenzake afungue mlango, mwingine anatukana akiwa kwa ndani hataki kufungua mlango. Hapa nawaza Khumbu anakuja, hilo songombingo la hawa mademu analikuta likiwa bado linaendelea itakuwaje? Nikapata wazo, yule demu aliyekuwa anabamiza mlango nikamfuata nikamwambia "ujue unachofanya sio sahihi. Hapa umevunja dirisha, hii gharama ya kurekebisha dirisha sisi ndio tutakaolipa. Halafu unavyoendelea kubamiza mlango kama hivi utajikuta umeuvunja na kutusababishia matatizo ya kufukuzwa hapa, wewe ondoka bhana. Nenda kadili na bwana ako. Yule demu akanielewa akasepa.

Baada ya yule demu kusepa, nikaanza kufanya usafi wa kuvifagia vile vipande vya glass haraka haraka ili angalu Khumbu akute hakuna machupa chupa. Muda kidogo nikasikia mlango wa kuingilia unagongwa, nikajua tu tayari Khumbu keshafika.

Itaendelea, acha nipumzike kidogo. Kutype nako kazi mjue.
 
Inaendelea.
Nikaenda kufungua mlango, kweli alikuwa ni Khumbu. Siku hiyo alikuwa amebeba begi kubwa kidogo tofauti na siku zingine. Moja kwa moja akaenda chumbani kuweka begi na kupunguza baadhi ya nguo mwilini. Mie nikawa pale sebuleni nimekaa kwenye makochi nikisubiria atoke chumbani tuone tunaanzia wapi kuongea. Kama dakika mbili hivi kupita, akaniita, "Konda msafi hebu njoo mara moja" nikajua tu hapa kidirisha kimemshangaza. Nikazama dani. Akaniuliza, hili dirisha limekuwaje? Nikamwambia weka kwanza begi chini, punguza hizo nguo then twende sebuleni nikakupe mkasa mzima. Nikamuona kasimama katika ile hali ya kuduwaa, huku kama anaguna hivi. Tukaenda sebuleni nikaanza kumwelezea kilichotokea. Uzuri wale mademu wa jamaa alikuwa anawafahamu maana walikuwa wanakutana. Tofauti na matarajio yangu hakuonyesha kujali sana.

....baadaye kidogo kuna kitu nahitaji kukifanya.
 
Baada ya kuona ndugu zako wameingia kwenye ishu ya kusukuma kete na kupata pesa nyingi vipi hukutaka na wewe kuungana nao kama ulivyofanya kwenye kuuza viatu ili mpige pesa pamoja na ikiwezekana na wewe umliki apartment yako umnyang'anye khumbu mazima jamaa aliyekuwa anamiliki Taxi?
Hapana hiyo biashara nilikuwa naiogopa sana. Hata kuyasogelea hayo makitu nilikuwa sitaki kabisa. Kwenye huu mkasa kuna scnerio ilitokea kidogo wazee wapite na mimi (wazee ni polisi), nitakuja kuelezea nini kilitokea.
 
Inaendelea.
Nikaenda kufungua mlango, kweli alikuwa ni Khumbu. Siku hiyo alikuwa amebeba begi kubwa kidogo tofauti na siku zingine. Moja kwa moja akaenda chumbani kuweka begi na kupunguza baadhi ya nguo mwilini. Mie nikawa pale sebuleni nimekaa kwenye makochi nikisubiria atoke chumbani tuone tunaanzia wapi kuongea. Kama dakika mbili hivi kupita, akaniita, "Konda msafi hebu njoo mara moja" nikajua tu hapa kidirisha kimemshangaza. Nikazama dani. Akaniuliza, hili dirisha limekuwaje? Nikamwambia weka kwanza begi chini, punguza hizo nguo then twende sebuleni nikakupe mkasa mzima. Nikamuona kasimama katika ile hali ya kuduwaa, huku kama anaguna hivi. Tukaenda sebuleni nikaanza kumwelezea kilichotokea. Uzuri wale mademu wa jamaa alikuwa anawafahamu maana walikuwa wanakutana. Tofauti na matarajio yangu hakuonyesha kujali sana.

....baadaye kidogo kuna kitu nahitaji kukifanya.

Ushauri:-

Andika story yako hadi Mwisho then utakuwa unapost vipande vpande kila baada ya dakika 10 mpaka mwisho sio ukipost unaanza kuandika nyingine inazingua.
 
Back
Top Bottom