Jinsi matapeli wa mjini wanavyotumia "harusi" kupiga pesa; inauma sana

Mbona hii mbinu ni ya kizamani sana
Jack Pemba mimi namjua tokea utotoni tunaishi nae Upanga, na hii ndio njia ilimpatia nauli ya kwenda UK.
Mkuu Makebo huu ndio utapeli mpya wa mujini. Watu wanakunja hela kiulaini bila jasho. Ni kadi yako tu na sio lazima umpelekee hard copy. Unamtumia tu kwa WhatsApp unalamba hela.
 
Kama alikuchangia kwanini ww usimchangie hata akienda kubetia ni haki yake
 
Eeh bwana hii harusi ya mjini ni uwanja wa kukimbizana ubavu kweli. Wale MC wanauliza "mchumba wa mwisho ni nani" hivi watu wanatolea pesa kama si hela zao, kumbe usiku wanalia kwenye kona. Niliona juzi mmoja akitoa laki tatu huku amevaa kiatu cha kupasuka, akili iliniuma. ngoma
 
Mkuu watu maskini wanapenda sifa sana. Haya mambo huwezi kuyakuta kwa matajiri.
 

View: https://x.com/PresenterNoah/status/2089393879460028585
 
Mtu unakosa aibu ya kutaka michango tena unaweka na kiasi huku ndoa ni yako na unaenda kufaidi ama kuumia peke yako?

Ndoa sio msiba useme kwamba ni ghafla. Ndoa ni maandalizi ya muda mrefu hivyo muoaji jiandae pele yako ualike tu watu ama ufanye kivyako vyako usisumbue watu na michango ya kipuuzi.

Binafsi nilijiamdaa mwenyewe vya kutosha kuanzia mahari hadi sherehe yenyewe watu wakaja kula na kunywa basi.

Kama hujajipanga acha kusumbua watu na utapeli wa michango.
 
Binafsi najisikia aibu kumuomba mtu mchango eti kisa naoa. Hii ni maajabu yaani starehe zangu binafsi nisumbue watu hadi kusababisha watu kukopa na kujiweka kwenye madeni? Big No.

Nipo na wake wawili na wote nilijifanyia maandalizi mwenyewe kuanzia mahari, ukumbi hadi sherehe nzima watu wakaalikwa kuja kula na kunywa na walijiuliza hili limewezekanaje maana walizoea kuona watu wanachangishana michango ya harusi.

Ni aibu na fedheha mwanaume kuwa na mke ndani huku ukijua kabisa bila michango ya watu usingefanikiwa kuwa naye.

Matokeo yake unagongewa mke maana ni mke wa wengi walifanikisha wewe kumuweka ndani. Pathetic.
 
Manina mimi sijawahi mchangia mtu namimi nilipooa hakuna michango ni simple like that,, Kila mtu aishi maisha yake, an unaoa kwa budget ambazo hazipo ndani ya uwezo wako ili uibuke kimaisha,, hakuna wa kunipata uzuri maisha yangu na sherehe ni paka na panya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…