Jinsi nilivyonusurika kung'atwa na nyoka wakati nataka kumuokoa

enzi nakua bana kijijini tumekaa tumetulia tunapia stori pembeni ya nyumba mara ghafra paka anakimbiza kitu kinamelemeta kinaelekea ndani ya nyumba,piga tochi kitu cheusi ndio kinamalizikia kuingia ndani kwenye kaupenyo ka mlango[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

tukakaa tumepanick tusielewe tunaanzia wapi operation fukuza nyoka,masaa yanakwenda nikajitolea kushika tochi kuingia ndani na mpini wa jembe,murika mlango wote na mazingira andamizi sioni kitu,ndani ya nyumba ni carpet la mpira haya ya aftatu mita[emoji1787]kulikuwa na watoto wa paka umri ule wa kuchezacheza na kila kitu,mama yao ndio yule aliyetuletea janga,baada ya kutukabidhi msala katokomea.
sasa nikawa naskia kama kitu kinachezewa kwa zamu huko chini kinapigwa kinateleza shaaa,kupiga tochi hivi nakuta nyoka wa kijani[emoji23][emoji23][emoji23]kumbukeni aliyeingia ni mweusi,na huyu ameshakufa kitambo,nyieeeeeeeee mnaweza otea hali ilikuwaje[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
ikabidi nitoe taarifa jamani chini ya kochi kuna nyoka paka wanamchezea lakini sio mweusi,na ameshakufa[emoji53][emoji53][emoji53]sister angu akaongea kwa wenge "nipeni mito ya makochi na funguo za darasa nilale darasani mimi ndani leo humu silali hata kwa dawa",tukamtoa kwa uangalifu,tukaanza kumtafuta huyo mweusi sasa,tafuta sana,mulika kwenye bati juu,lahaula[emoji2][emoji2]juu ya kuta pembeni mwamba huyu hapa,gues what wa kijani tena,tukaanza kutoleana macho mbona kama kuna mkono wa mtu hapa,sister hata morali wa kwenda kulala huko darasani umekata ameanza kukemea mapepo[emoji16][emoji16].naye akauwawa.
ikabidi lije wazo yamwangwe mafuta ya taa ndani ila tusilale tubebe mito na mikeka tukaangushe madarasani.mafuta ya taa yakapigwa sehemu ambazo anazaniwa anawezakuwa kajificha,wakati nahangaika kutoka mikeka na mito ya makochi,ghafla naskia paka anapurukusha,kumbe alikuwa anajaribu kutoka mafichoni akakutana na wale paka wadogo ndio wamemuweka kati,tukamalizia tukamtupa nje,ila kulala ilikuwa ni lazima tukalale darasani hakukuwa na namna.kumbe mchana kutwa kulikuwa na moto mapori ya jirani.

by the way nyoka wauaji wote ni ngumu sana kukutana na binaadam,na wao wanajificha sehemu pweke sana hawapendi muingiliano,hawa wengine wanasababisha wenge tu akikuuma.
 
Huyo ilitakiwa umwagie mafuta ya taa na si kumjengea ngazi. Tambua nyoka ni adui yako milele na milele
 
mtu anayependa nyoka na kuwaonea huruma huwa ninaona ana traces za ushirikina
You miss the point sir..sio kwamba nawaonea huruma nyoka tu bali ni viumbe wote hua siwaui kabisa. Except mbu
 
Ndiyo maana siafu hawana sumu mkuu..
Na hata nyoka hawa wa kitaa huwa hawana noma, sema wenge letu tu binadamu kutokana fikra zetu juu ya nyoka. Siafu wana madhara makubwa wakiingia usiku ukiwa usingizini kuliko nyoka alafu wamkute mtoto au mgonjwa hajiwezi anakwenda na maji lakini nyoka anapiga kimya hata mwezi na kama kuna panya na usafi na mpangilio wa vitu ni sifuri mtaishi nae vizuri anaweza akapita hata kwenye miguu kama ni giza na hakugongi
 
Kama unawarumia, mfano ukimuacha na akamuuma mtu, huoni ni kosa lako la kutokumuuwa? Nyoka ni nyoka tu ukipata chance muangamize.
 
Mkuu nashkuru Kwa Andiko zuri na lenye madini mazuri sana

ila nadhani kuna sehemu hatujaenda Sawa, unaposema uwezo wa kujua Mema na mabaya katika mada yako haina uhusiano na mtu kung'atwa na nyoka au kinyume chake

Ukisema Jema na Baya utapata tafsiri tofauti kutoka Kwa kila jumuiya, kwenu kitu kibaya kinaweza kikawa kizuri Kwa wengine, au katazo la kabira fulani linaweza kuwa sio katazo katika kabira lingine, kwahiyo hakuna definition sahihi ya Jema na Baya

Nadhani ulipaswa kuongelea HATARI/USALAMA, hiki ndio kinafanya either nyona akuduru au asikudhuru maana Kuna tofauti Kati ya JEMA/BAYA na HATARI/SALAMA, kujua kwako jema au baya hakukufanyi ung'atwe au using'atwe na Nyoka

Kinachokufanya using'atwe ni kujua either ni hatari au salama, mtoto mdogo haumwi na nyoka sio Kwa sababu hajui Jambo jema na Baya lahasha haumwi Kwa sababu hajui kutofautisha hatari na salama

Na wasioumwa na nyoka sio watoto tu bali ata wakubwa pia wapo ambao hawana hofu ya nyoka japokuwa wanajua Jambo jema na Baya, ukizoea kuwa karibu na nyoka hiyo hali itakufanya uwe una feel normal towards them

Na kama utakuwa kawaida kabisa mbele yao basi kupelekea mfumo wako wa hormone usi react kuzalisha hormone ya uoga hivo nyoka hatokuona kama wewe ni hatari kwake na kufanya asi react tofauti

Kuna muda sie tuliekuwa tunaenda kuchezea nyoka sehemu Fulani, wale wenyeji wetu wanatuelekeza ni namna gani ufanye ili nyoka awe kawaida kwako, na moja ya njia hiyo ni kupumua vizuri na kumfanya nyoka ajifeel yuko sehemu salama

Kama utaweza kubalance uhemaji wako na mapigo ya moyo ni hapo hormone ya uoga huondoka mwilini na utaweza kushika nyoka, ila endapo Kwa makusudi au bahati mbaya ikatokea mtu akakutisha ghafra ukiwa umeshika nyoka basi yule nyoka atakung'ata

Jambo zuri ni kwamba hiyo michezo tulikuwa tunaifanya kwa wale nyoka wasiokuwa kuwa na sumu kama pythons au wale ambao wameondolewa Meno, kwahiyo ata aki react kukung'ata anakuwa hajakudhuru

Kwahiyo nachelea kusema kwamba sio KWELI kwamba nyoka anang'ata/kugonga mtu Kwa sababu anajua Jema na Baya, bali atang'ata/kugonga mtu Kwa sababu anajua tofauti ya hatari na salama

Masai wanauwa Simba na kuogopwa na Simba sio Kwa sababu Masai hajui Jema na Baya ispokuwa kwakuwa Masai anabadirisha hali ya Hatari na kuitafsiri kinyume kuwa ni salama hivo endocrine system itakuwa normal muda wote na kupelekea Simba kuwa na hofu mbele ya Masai na yeye ndio kupoteza kujiamini

Mind you, kuna nyoka ambao wao by nature tu ni wakorofi kwahiyo hawaathiriwi na mfumo wa hormone zako, either adrenaline izalishwe au isizalishwe wewe unakuwa katika hatari ya kuzulika

na baadhi ya hao nyoka ni Black Mamba huyu hanaga usela na binadamu ata siku moja, yeye muda wowote yule anakuchenjia ata kama wewe ndio unamfuga na always unatakiwa kuwa makini sana unapokuwa karibu nao

Mwisho kabisa, katika ukoo wetu sie hatuuwi nyoka na hiyo kupelekea kuwa tunafeel normal pindi tunapowaona, japokuwa Kwa mara ya Kwanza naskia haya nilipoenda Kwa Bibi yangu nilikuwa muoga sana ila badae nikazoea
 
Unaweza ishi na Koboko(hata nyoka wengine pia) zaidi ya Miaka 100 asikudhuru ila sharti ni moja tu" nyoka ndiye ajue uwepo wa binadamu eneo ilo ila si binadamu ndiye ajue kuna nyoka eneo ilo".. Hii ni kwa uzoefu binafsi na kusoma maandishi kama haya.
Duu! Fafanua kdg
 
😁😁😁 Tabora kuna mahala tulikuwa tumeenda kufunga pump ( igombe ) kwa ajiri ya kusukuma maji enzi hizo, unaambiwa pale ambapo tunakaa au kulala juu yake kuna koboko wanaishi.. yani kule Tabora koboko kama gugwaa ( panzi ).


Singida nahisi itakuwa kuna maeneo na maeno yenye nyoka nimekaa ukiwa unatoka puma unaenda kushoto ndio ndio nilikutana na manyoka kula kama vitoweo, sikurudi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…