Jinsi tunavyoishi wakristo hapa Zanzibar kipindi hiki cha mfungo

Mara nyingi mtu hujikuta hautambui unachohitaji hasa ni nini. Tangu mwez mtukufu umeanza wengi mnakuja na malalamiko ambayo hayaeleweki hasa mnahitaji nini.
kwamba mnalalamika kwa sababu ngozi nyeupe wanaruhusiwa kula hadharani na ninyi hamruhusiwi? kwamba ikitokea na ngozi nyeupe wakakatazwa kula hadharani bas hapo hamtalalamika tena?
 
Kama ni kweli basi wazenji ni wapuuzi kiwango cha PhD.

Hakuna thawabu inapatikana kwa upumbavu kama huo, baadhi ya waislamu wamechagua kuwa wapumbavu na kuingiza dini kwenye upumbavu wao ili ionekane wote tulioko kwenye uislamu hatuna akili.
 
Ukiwa umefunga na ukamuona mtu anakula wewe unaathirika nini?
Tuache mambo ya kijima wakuu
 
Napata wasi wasi na uwezo wako wakufikiri kuzika mbona wengi wana zikwa na manspaa
 
Kila sehemu kuna mila, taratibu, desturi, tamaduni, silka zake. Zanzibar ilitawaliwa na waarabu na kwa asilimia 99 ya wazanzibari ni waislam. Kama sikosei walitaka kujiunga na OIC miaka ya nyuma huko kitu ambacho kingeitambulisha Zanzibar kama taifa la Kiislam. Muungano wa Zanzibar na Bara ndio uliosababisha hadi leo hii Zanzibar kukwama kuwa taifa la Kiislam. Hivyo basi kulingana na maelezo hayo mafupi utaona ni jinsi gani Zanzibar ilivyo. Hivyo basi wapo Wakristo ambao nao pia wamezaliwa na kukulia Zanzibar lakini wanafuata mila, taratibu, desturi, tamaduni, silka za kizanzibar. Sasa basi ikiwa umekwenda ugenini kwa watu jaribu sana kuelewa ni kipi wenyeji wako wanapenda na kipi hawapendi ili kuweza kuendana na sehemu husika na sio kutaka kufanya vile unavyoona kwako inafaa wakati huo huo ukiwaudhi wenyeji wako.
Kama ukiona unashindwa au unanyanyasika unaweza kurudi nyumbani kwa maana hujafukuzwa. Lakini pia kwanini uteseke na una kwenu? Vile vile kuharibika kwa mila, taratibu, desturi, tamaduni, silka za kwenu kusisababishe ukataka na ugenini kwako kuwe hivyo hivyo.
 
Kuruhusu ngozi nyeupe kula na kukataza nyeusi kula ni jambo moja na kukataza mtu ambaye hajafunga kula ni jambo jingine, na hii ndo sehemu uislamu unakofeli sana kama dini
 
Wakristo bwana!! Sasa hizi propaganda za uongo zinasaidia nini,??? Mbona sehemu za kula kwa wasio Waislamu ziko nyingi..
Ukenda Maisara sehemu moja inatwa CCM inapata chakula unachotaka..

Anyway, Zanzibar iko hivyo miaka nenda miaka rudi mbona Wakristo wazawa wa Zanzibar hawajalalamika!!!!?
 
Nenda walipo wazungu na wewe ukale huko very simple
 
Usijali next1 week ni sikukuu yao mwezi wa ramadhan unaisha
 
Nikupe kaushauri tu. Elewana na hao waliokuajiri kuwa; Ikifikia mwezi mtukufu, wakupe likizo au upelekwe bara mpaka tumalize mfungo. Wewe unasaidiwa ili upate rehma bado inakuwa taab. Kweli kipofu mkaidi hafaidiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…