Jinsi ya kufungua kanisa 'la Mchongo' la kilokole na upige pesa Kwa Muda mrefu

Jinsi ya kufungua kanisa 'la Mchongo' la kilokole na upige pesa Kwa Muda mrefu

Ha haaa halafu unaambiwa utapata gari..ukijiangalia huna kipato cha kueleweka hata kula milo miwili ni shida.
Gari linashuka kimiujiza
Katika maisha hautakiwi kukata tamaa, wanakwambia hvo ili kukuhamasisha uone kuwa unaweza.

utajisikiaje pale utakapokuwa mgonjwa, alafu ukaambiwa "utakufa"
 
Hebu tuinuke tuombe Ooh haleluya bababashakalabobobo sakata tumbaa ai katumba aswaapapapa aswaaa papapaa sakataaa bolokoshokoloo gooooooooooooooooooooooooooooooooooloo hapanaa sio gooli wote tuseme ameen
Nyie hebu punguzeni, mnatuvunja mbavu wenzenu. Hakika, haya yanafanyika kuzuga waumini.
 
Hahaaa. Stori ni muhimu sana. "Nilifika pori moja, yapata usiku wa saa sita, pikipiki imeniharibikia, giza zito na wingu vimetanda. Pande zote ni msitu mnene. Nikasema bwana, kwa kuwa nimekuja kufanya kazi yako....." Endeleaa
Hakuna jambo litashindikana, kultokea kundi la simba wapatao saba 😂😂😂..,.Endelea
 
Ile si unanyofoa fyuzi ya aibu kichwani 😂😂😂
Ujue kuongea hadi uteme mvua ya mate.
Kuna mchungaji mmoja aliniombea anatema mvua balaa, nilitoka hapo nanuka mate
 
"Nikakumbuka kisa cha Danieli kwenye tundu la Simba. Nikapiga magoti, macho ya simba wale yamenizunguka kama tochi kali. Nikainua mikono juu, nikasema....." Endelea
Bwana wa majeshi ufanyae njia pasipo na njia, haujawahi shindwa na lolote hata ningalipo katika uvuli wa mauti, ulisema nena neno likawe basi naamuru katika jina la yesu "tawanyikaaaa" .....endelea
 
Me nitamfata tu MWAMPOSA anipe mbinu vzr[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Bwana wa majeshi ufanyae njia pasipo na njia, haujawahi shindwa na lolote hata ningalipo katika uvuli wa mauti, ulisema nena neno likawe basi naamuru katika jina la yesu "tawanyikaaaa" .....endelea
"Simba wale walirudi nyuma lakini hawakuondoka kabisa. Nikakumbuka jambo jengene, ngovo ya nyimbo katika maombi. Na hilo ndilo somo letu leo.

NGOVO YA NYIMBO KATIKA MAOMBI. Nikaanza kuimba, ni wimbo niliofundishwa na rafiki yangu kutoka Minnesota. Nitakwenda kuuimba, 'Rock of ages cleft for me, let me hide Myself in thee.' kabla sijaendelea jambo la ajabu lilitokea...." Endelea
 
Uongo si ni dhambi au?
hyo ni motisha! imani huja kwa kusikia, na kuona.

watoto tunawambia wasome kwa bidii kwamba watakuja kuwa maEngneer, form4 anatoka na "F"
"F flat" ~msemo wa mgogo
 
Jifunze kuongea kwa sauti kali na lafudhi ya nyanda za juu kusini,mtu muite mutu,mfano tamka mufano,kila ukihubiri ukiona wanaanza kusinzia tunga stori ya uongo ipakeoake mafuta,watu wanapenda mifano ya stori sana kanisani ,anza hivi siku moja nikiwa london,mutu mumoja akanishika bega,nikashangaa huu muji wa wazungu nani ananijuwa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
"Jifunze kuongea kwa sauti kali na lafudhi ya nyanda za juu kusini,mtu muite mutu,mfano tamka mufano,kila ukihubiri ukiona wanaanza kusinzia tunga stori ya uongo ipakeoake mafuta,watu wanapenda mifano ya stori sana kanisani ,anza hivi siku moja nikiwa london,mutu mumoja akanishika bega,nikashangaa huu muji wa wazungu nani ananijuwa.
Pia na kujifunza kutamka haya maneno kwa lafudhi ya hao manabii na mitume!

Badala ya kusema "mbingu zitafunguka"!! Unasema "mbengo zetafongoka"!! Oooh! Halleyuh!!
 
Back
Top Bottom