Jinsi ya kufungua kanisa 'la Mchongo' la kilokole na upige pesa Kwa Muda mrefu

Jinsi ya kufungua kanisa 'la Mchongo' la kilokole na upige pesa Kwa Muda mrefu

1:Anzia kijijini. Kule utapata wafuasi wengi wasio na uwezo wa kuhoji kipindi uwezo wako wa kushawishi Bado mdogo.

2: TUMIA Muda mwingi kusoma vitabu vya uchawi ili ujue watu wanalogwaje, vitabu vya migogoro ya ndoa, magomvi ya familia na ukoo...
Aisee
 
Mgee namba zangu mwakani tulianzishe,
Ukianzisha kanisa jichangechange siku moja safiri nchi yoyote ya Amerika ya Kusini tafuta kanisa uchwara anza nao undugu waalike waje afrika kutoa huduma.

Siku utakaposhusha mzungu kanisani kwako WAMBIE MHUBIRI KUTOKA MAREKANI .... najitahidi siku moja ukienda kwao ongoza maombi kwa ufupi ila piga picha nyingi.

Kanisa lako tayari litakua limesimama na utaona MBENGO ZINAVUOFUNGUKA
 
Kalumanzila anakupeleka msituni, anafanya yake nawe unasema "alleluia ×3 " utasikia kwa umbali mti mmoja unaitika Aaaaamen! Anakupeleka kwenye mti ulioitika na kutambika.

Tafuta mtaji kidogo uanzishe kanisa na utafute jina ulilopewa na kalumanzila mf. "Kanisa la kujimaliza" utapata wateja wengi na sadaka kwa wingi mpaka ushangae.

Biblia unakariri tu mistari michache, mistari mingine watatafuta waumini. Piga mzigo, ila kalumanzila unamlipa kwa mwezi kwa maelewano.
 
hyo ni motisha! imani huja kwa kusikia, na kuona.

watoto tunawambia wasome kwa bidii kwamba watakuja kuwa maEngneer, form4 anatoka na "F"
"F flat" ~msemo wa mgogo
Ndo maana watu wanye akili zao hawaamini tena, uongo wa wazi wazi
 
Mchungaji Mwangosi kutoka Kyela, oh Hallelujah
 
Sio rahisi hivyo

Kama unadhani rahidi jaribu uone

Kama hujawaho pata ugonjwa wa moyo.utapata

Mtu kupata wafuasi ujue sio mtu wa kawaida
 
Hakika kuna ulazma wa kutunga sheria ya kudhibiti haya makanisa
Serikali haina dini haiwezi kudhibiti dini

Ni kinyume pia cha katiba ya nchi inatamka wazi kuwa mambo ya dini yatakuwa swala la mtu binafsi

Wewe mwenyewe ndie ujidhibiti
 
Ha haaa halafu unaambiwa utapata gari..ukijiangalia huna kipato cha kueleweka hata kula milo miwili ni shida.
Gari linashuka kimiujiza
Katika maisha hautakiwi kukata tamaa, wanakwambia hvo ili kukuhamasisha uone kuwa unaweza.

utajisikiaje pale utakapokuwa mgonjwa, alafu ukaambiwa "utakufa"
 
1:Anzia kijijini. Kule utapata wafuasi wengi wasio na uwezo wa kuhoji kipindi uwezo wako wa kushawishi Bado mdogo.
Unaota makanisa mengi vijijini hata ya zamani matupu

Watu wengi hawasali wanaishi kishirikina tu

Ukipata waumini hata kumi una bahati

Kuanzisha kanisa sio mchezo iwe mijini au vijijini

Usione watu wanafurika mahali.ujue.kuna kitu cha ziada kipo pale zaidi ya mayowe ya vifungu vya Biblia
 
Katika maisha hautakiwi kukata tamaa, wanakwambia hvo ili kukuhamasisha uone kuwa unaweza.

utajisikiaje pale utakapokuwa mgonjwa, alafu ukaambiwa "utakufa"
Watupe mbinu za kutafuta na kutokata tamaa, ukiniambia nikeshe kwenye maombi huo muda wa kutafuta pesa nitatoa wapi?
Watufundishe kiuhalisia...hakuna miujiza tunadanganyana
 
Back
Top Bottom