Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ili maiti aweze kuoshwa vizuri hatua zifuatazo ziweze kupitiwa:
1. Maiti awekwe kwenye kitanda chenye tobo katikati kwa ajili ya kupitisha uchafu utokao tumboni kama upo.
2. Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda ili kuhifadhi uchafu utokao kwa maiti.
3. Maiti afunikwe na shuka kubwa iliyonyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.
4. Maiti ikalishwe kitako na makalio yake yaelekee kwenye tobo la kitanda.
5. Muoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili kutoa uchafu
6. Alazwe chali na aminyeminye tumbo lake kama hapo awali.
7. Aikalishe tena kisha apitishe mkono wa kushoto chini ukiwa umevalishwa kitambaa au gloves asafishe tupu mbili huku akijimiminia maji mkono wa kulia.
8. Ampigishe mswaki kwa kitambaa kilaini kilicho viringishwa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichove majini kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini kisha akitupe ufuoni.
9. Azungushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichove majini, kisha amsafishe nacho tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
10. Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake, iwapo ni ndefu na chafu.
11. Akiwa pia kamkalisha maiti amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha.
12. Kumuosha kichwa kwa sabuni.
13. Kisha kumuosha kwa ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma.
14. Kisha hivyo hivyo na ubavu wa kushoto.
15. Baada ya makosho hayo mawili la maji na sabuni na kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo.
16. Baada ya makosho haya matatu, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawa sawa kama alivyolazwa mara ya kwanza baada ya kufa. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti tayari kwa kivishwa sanda.
Hayo ni mafundisho katika imani ya kiislamu!Ahsante kwa somo, ila huu uoshaji unahusika kwa dini zote mbili?
Kukafini= maana yake ni kuvisha sanda na kumtia katika jeneza.Huku sio kuosha maiti, ni kukafini...
Nafikir waislam pekee ndio huoshaga maiti kutoka kweny Qur-aan , Hadithi na sunah za mtume Muhammad (s.a.w) sijui kwa upande Wa pili wanaweza wakaelezeaMkuu ungesema huyo maiti ni wa imani ipi maana sidhani kama imani zote zinapaswa kufanya hayo
Hii itabidi niikopi, maana haya majukumu hayakwepeki.
Mweeeeeh bora ungewaza kimoyo moyo tu
Ha ha ha, yaani hata kusoma nimeogopa, kwa hiyo nimekoment bila hata kuisoma!
Umeisoma?
Duh..! hata kale kajamaa kenye avatar ya mtoto aliyebemendwa kanakokuwaga kakwanza kukoment kila uzi leo hakajatia neno hapa ujue huu uzi ni balaa.Hivi una maana gani maana sielewi nia na dhumun lako,ngoja waje waoshaji
Ee nimeisoma hadi mwisho. Haiogopeshi bana(Mchana huu nasema tu usiku shughuli ndotoni)
Mshana Mwengine Kaja Jf
Sina uhakika, hivi wanawake wanaosha pia?