Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Watu wanaogopa kufa. Huu ni ukumbusho kwamba sisi wote tutakufa tupo njiani . tutende yanayompendeza muumba.
 
Duh..! hata kale kajamaa kenye avatar ya mtoto aliyebemendwa kanakokuwaga kakwanza kukoment kila uzi leo hakajatia neno hapa ujue huu uzi ni balaa.
Huu uzi mkuu ni balaa,maana kuusoma si kaz ndogo,ndo maana nikamuuliza ana maana gani
 
Ili maiti aweze kuoshwa vizuri hatua zifuatazo ziweze kupitiwa:
1. Maiti awekwe kwenye kitanda chenye tobo katikati kwa ajili ya kupitisha uchafu utokao tumboni kama upo.
2. Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda ili kuhifadhi uchafu utokao kwa maiti.
3. Maiti afunikwe na shuka kubwa iliyonyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.
4. Maiti ikalishwe kitako na makalio yake yaelekee kwenye tobo la kitanda.
5. Muoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili kutoa uchafu
6. Alazwe chali na aminyeminye tumbo lake kama hapo awali.
7. Aikalishe tena kisha apitishe mkono wa kushoto chini ukiwa umevalishwa kitambaa au gloves asafishe tupu mbili huku akijimiminia maji mkono wa kulia.
8. Ampigishe mswaki kwa kitambaa kilaini kilicho viringishwa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichove majini kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini kisha akitupe ufuoni.
9. Azungushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichove majini, kisha amsafishe nacho tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
10. Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake, iwapo ni ndefu na chafu.
11. Akiwa pia kamkalisha maiti amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha.
12. Kumuosha kichwa kwa sabuni.
13. Kisha kumuosha kwa ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma.
14. Kisha hivyo hivyo na ubavu wa kushoto.
15. Baada ya makosho hayo mawili la maji na sabuni na kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo.
16. Baada ya makosho haya matatu, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawa sawa kama alivyolazwa mara ya kwanza baada ya kufa. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti tayari kwa kivishwa sanda.
Ahsante mkuu,kwanza ukimuosha maiti unajua on the spot mwanaadamu si kitu hapa duniani!Nilijifunza hili wakati na muosha marehemu babaangu,mungu ampe Kauli Thabit!
 
Namba 4 Kwa kiswahili cha kwetu Pwani.. Ni kumpondoa maiti
 
Duh..! hata kale kajamaa kenye avatar ya mtoto aliyebemendwa kanakokuwaga kakwanza kukoment kila uzi leo hakajatia neno hapa ujue huu uzi ni balaa.
Kale ni kajobless saiv kameenda kucheza
 
Hayo ni mafundisho katika imani ya kiislamu!
"Waislamu tunaamini ile ni nyumba ya kwanza miongoni mwa nyumba za mbinguni na ya mwisho miongoni mwa nyumba za dunia"
Yampasa maiti apelekwe hali ya kuwa ni msafi.
Sawa, lakini kwani hii ni elimu ya hadhara?
 
Back
Top Bottom