Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

hayo masharti utadhani marehemu akioshwa hivo ataingia peponi
 
Ahsante mkuu,kwanza ukimuosha maiti unajua on the spot mwanaadamu si kitu hapa duniani!Nilijifunza hili wakati na muosha marehemu babaangu,mungu ampe Kauli Thabit!
Du pole dada kufiwa na baba ako,Ila wewe si binti ulimuoshaje sasa
 
Duh kazi mnayo. Sasa mnakamua uchafu ili iweje? Mwache aende na machakula yake...
 
Ili maiti aweze kuoshwa vizuri hatua zifuatazo ziweze kupitiwa:
1. Maiti awekwe kwenye kitanda chenye tobo katikati kwa ajili ya kupitisha uchafu utokao tumboni kama upo.
2. Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda ili kuhifadhi uchafu utokao kwa maiti.
3. Maiti afunikwe na shuka kubwa iliyonyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.
4. Maiti ikalishwe kitako na makalio yake yaelekee kwenye tobo la kitanda.
5. Muoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili kutoa uchafu
6. Alazwe chali na aminyeminye tumbo lake kama hapo awali.
7. Aikalishe tena kisha apitishe mkono wa kushoto chini ukiwa umevalishwa kitambaa au gloves asafishe tupu mbili huku akijimiminia maji mkono wa kulia.
8. Ampigishe mswaki kwa kitambaa kilaini kilicho viringishwa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichove majini kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini kisha akitupe ufuoni.
9. Azungushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichove majini, kisha amsafishe nacho tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
10. Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake, iwapo ni ndefu na chafu.
11. Akiwa pia kamkalisha maiti amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha.
12. Kumuosha kichwa kwa sabuni.
13. Kisha kumuosha kwa ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma.
14. Kisha hivyo hivyo na ubavu wa kushoto.
15. Baada ya makosho hayo mawili la maji na sabuni na kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo.
16. Baada ya makosho haya matatu, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawa sawa kama alivyolazwa mara ya kwanza baada ya kufa. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti tayari kwa kivishwa sanda.
Asante mkuu kwa kutumegea machache kuhusu uoshaji wa maiti. Wengi wetu hatujawahi kupractice hiyo kitu
 
Sina uhakika, hivi wanawake wanaosha pia?
Ndio katika imani ya kiislamu mwanamke humuosha mwanamke mwenzake na mwanaume vivyo hivyo.

Ila ni bora zaidi maiti ikaoshwa na mtu wa karibu yake kama mume kumuosha mke au mke kumuosha mume!

Ama ni vyema kuoshwa na mtu ndugu yako ili kuficha aibu itakayoonekana kwa maiti.Mfano harufu mbaya,vidonda visivyomithilika n.k.

Mungu ndie mjuzi zaidi.
 
Asante kwa taarifa mkuu, maana kujifunza haya mambo ni muhimu sana.
 
Ili maiti aweze kuoshwa vizuri hatua zifuatazo ziweze kupitiwa:
1. Maiti awekwe kwenye kitanda chenye tobo katikati kwa ajili ya kupitisha uchafu utokao tumboni kama upo.
2. Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda ili kuhifadhi uchafu utokao kwa maiti.
3. Maiti afunikwe na shuka kubwa iliyonyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.
4. Maiti ikalishwe kitako na makalio yake yaelekee kwenye tobo la kitanda.
5. Muoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili kutoa uchafu
6. Alazwe chali na aminyeminye tumbo lake kama hapo awali.
7. Aikalishe tena kisha apitishe mkono wa kushoto chini ukiwa umevalishwa kitambaa au gloves asafishe tupu mbili huku akijimiminia maji mkono wa kulia.
8. Ampigishe mswaki kwa kitambaa kilaini kilicho viringishwa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichove majini kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini kisha akitupe ufuoni.
9. Azungushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichove majini, kisha amsafishe nacho tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
10. Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake, iwapo ni ndefu na chafu.
11. Akiwa pia kamkalisha maiti amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha.
12. Kumuosha kichwa kwa sabuni.
13. Kisha kumuosha kwa ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma.
14. Kisha hivyo hivyo na ubavu wa kushoto.
15. Baada ya makosho hayo mawili la maji na sabuni na kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo.
16. Baada ya makosho haya matatu, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawa sawa kama alivyolazwa mara ya kwanza baada ya kufa. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti tayari kwa kivishwa sanda.
nini kitatokea endapo mtu atazikwa kama hajaoshwa...??
ni madhara yapi ya kiimani mtu au jamii itayapata kama hautaosha mwili wa ndgu yenu..?

naomba kuwakikisha make naona kuosha maiti kama ulazima flani hivi...
 
Mkimaliza kuosha nipeni hayo maji mlioshea huyo mtu nina kazi nayo...🙄
 
Mkuu, naona umemkosea HESHIMA Marehemu...

Mbona unafichua tena FARAGHA yake...!!?

Sio ubinaadamu huo..

Kila mtu anafahamu kama Maiti huoshwa toka ENZI NA ENZI...Ila hakuna taarifa rasmi za uoshaji..

Wazee waliiweka kama PRIVECY kwa kila MAREHEMU...

TUTAKE RADHI SISI MARAHEMU TARAJIWA...
achana naye, mleta mada hajui kuwa jambi hili haliwezi kufanyika mjini kama alivyoliainisha , mjini hakuna mashimo hayo ya kutupa uchafu
 
Back
Top Bottom