Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Ilikuwa inasemekana, sasa nimeanza kuamini yakuwa huwa mnamkamua marehemu kinyesi

D.A "Mwanaume mashine"
Hata mimi leo ndio nimehakikisha.du dunia ina mengi hii.pole yao.mmmh process yote hii halaf anaendazikwa mavumbini.kisha anuke na kuoza so soon.
 
Ili maiti aweze kuoshwa vizuri hatua zifuatazo ziweze kupitiwa:
1. Maiti awekwe kwenye kitanda chenye tobo katikati kwa ajili ya kupitisha uchafu utokao tumboni kama upo.
2. Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda ili kuhifadhi uchafu utokao kwa maiti.
3. Maiti afunikwe na shuka kubwa iliyonyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.
4. Maiti ikalishwe kitako na makalio yake yaelekee kwenye tobo la kitanda.
5. Muoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili kutoa uchafu
6. Alazwe chali na aminyeminye tumbo lake kama hapo awali.
7. Aikalishe tena kisha apitishe mkono wa kushoto chini ukiwa umevalishwa kitambaa au gloves asafishe tupu mbili huku akijimiminia maji mkono wa kulia.
8. Ampigishe mswaki kwa kitambaa kilaini kilicho viringishwa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichove majini kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini kisha akitupe ufuoni.
9. Azungushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichove majini, kisha amsafishe nacho tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
10. Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake, iwapo ni ndefu na chafu.
11. Akiwa pia kamkalisha maiti amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha.
12. Kumuosha kichwa kwa sabuni.
13. Kisha kumuosha kwa ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma.
14. Kisha hivyo hivyo na ubavu wa kushoto.
15. Baada ya makosho hayo mawili la maji na sabuni na kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo.
16. Baada ya makosho haya matatu, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawa sawa kama alivyolazwa mara ya kwanza baada ya kufa. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti tayari kwa kivishwa sanda.
Dhehebu gani linaloosha maiti kisenge namna hii? Quran na biblia zimekataza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbuka kuyabeba maji uliyooshea ni kipusa hapa town.
 
Nimeyabeba ya mhimu, ni habari ngumu kuisoma ila ndiyo hivyo hatuna jinsi maana tunafiwa watu mhimu sana ambao huwezi kukwepa jukumu hilo.
 
hapo nina swali huwa uchafu wa ndani ya tumbo mnautoa? kama mnautoa mbona hujaeleza hapo kiundani tuelewe
 
Ili maiti aweze kuoshwa vizuri hatua zifuatazo ziweze kupitiwa:
1. Maiti awekwe kwenye kitanda chenye tobo katikati kwa ajili ya kupitisha uchafu utokao tumboni kama upo.
2. Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda ili kuhifadhi uchafu utokao kwa maiti.
3. Maiti afunikwe na shuka kubwa iliyonyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.
4. Maiti ikalishwe kitako na makalio yake yaelekee kwenye tobo la kitanda.
5. Muoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili kutoa uchafu
6. Alazwe chali na aminyeminye tumbo lake kama hapo awali.
7. Aikalishe tena kisha apitishe mkono wa kushoto chini ukiwa umevalishwa kitambaa au gloves asafishe tupu mbili huku akijimiminia maji mkono wa kulia.
8. Ampigishe mswaki kwa kitambaa kilaini kilicho viringishwa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichove majini kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini kisha akitupe ufuoni.
9. Azungushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichove majini, kisha amsafishe nacho tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
10. Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake, iwapo ni ndefu na chafu.
11. Akiwa pia kamkalisha maiti amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha.
12. Kumuosha kichwa kwa sabuni.
13. Kisha kumuosha kwa ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma.
14. Kisha hivyo hivyo na ubavu wa kushoto.
15. Baada ya makosho hayo mawili la maji na sabuni na kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo.
16. Baada ya makosho haya matatu, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawa sawa kama alivyolazwa mara ya kwanza baada ya kufa. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti tayari kwa kivishwa sanda.
Allah akulipe ndugu
 
Huyo anaetukana mwambie asipanic ndio waisilamu haya tuelezee kwa wakristo na utupe andiko gani kwenye bible jinsi ya kuosha maana vitabu ndio miongozo yetu. Au mzungu
 
Ilimu iyo ni muhimu kwa waislamu na wote wanaoamini katka kufa na stara ya maiti
 
Hakika ni vyema kujiandaa kama kuoshwa twaogopa je tungeliyajua yale yanayotokea kaburini ingekuaje? Mwenyezi tufanye tuwe waja wema In Sha Allah
Hakuna yanayotokea kaburini boss,achana na hofu of unknown. Waogope wasiojulikana Tanzania make wanaweza kukutoa roho.
 
Katika ukimwengu uliojaa maradhi kama wetu sijyi inakuwaje kwa huo utaratibu hasa hiyo ya kumswakisha marehemu kwa kidole tu chenye kitambaa laini. Kuna hatari ya kuambukizana maradhi mwanzo mwisho. Anyway sisi wote tunaoita na njia yetu sote ndiyo hiyo japo wengine hatutapitia process zote hizo
yaan process zimekuwa ni conservative hazijaangalia variable 2 ambazo very important
1.time
2.environment

let say mtu kama na kipindu pindu o ugonjwa wowote hatari bila kuchukua precautional measure mtapukutika kijjin o mtaa mzima km majani ya kiangazi!

hizo hatua zinaeleza as if kila mait wako the same in character...eg mtu amekufa amejinyonga ameharibika o matumbo yako nje ameanza kutoa harufu unamkalisha?unampigisha mswaki?...sasa huo ni mswaki o kidole ulichoingiza mdomoni,sasa kidole kilichofungwa kitambaa kinatosha kuondoa uchafu bila mswaki halisi na dawa? ikiwa aim ni kuondoa uchafu?

====na kwanini kidole isiwe mswaki wa mti km aliyokuwa anatembea nao mudi?
 
Mkuu ungesema huyo maiti ni wa imani ipi maana sidhani kama imani zote zinapaswa kufanya hayo
kuosha maiti kuna imani kuuumbe.... ina maaana kuna wengine ambao wanazika hata na mavi....[emoji15] [emoji15]
 
Back
Top Bottom