Jinsi ya kupika chapati za maji ambazo hazina viungo vingi

Jinsi ya kupika chapati za maji ambazo hazina viungo vingi

๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€Hatari sana mm nashukuru Mungu wakija rafikizangu au wageni hata nijikaushe utasikia kwani Leo hupiki Cha ajabu hata Sina Cha maana nachopika vyakula vya kawaida tu๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
Au ndo kama vile siku hyo unasingizia unauwamwa ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
Au ndo kama vile siku hyo unasingizia unauwamwa ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Hahha najifanyaga Nina safari ila uzuri lazima hata bites ziwepo wanakula wanaridhika ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Natumaini mkopoa
Tujifunze namna ya kupika chapati za maji Kwa njia rahisi na haraka pia ni moja ya vitafunwa ambavyo havina mambo mengi
Mahitaji
Ngano robo au kias unachopenda Kulingana na familia Yako
Iriki au vanilla
Sukari /chumvi ni vile upendavyo
Yai moja au mawili
Maji ya baridi
Hatua
Chukua bakuli safi na kavu weka ngano na sukari Changanya kidogo Kisha Anza kuweka Maji ya baridi kidogo kidogo huku unakoroga had utapoona ngano Yako imekuwa uji mzito hakikisha hauna mabonge
Ongezea mayai pamoja na iriki au vannila endelea kukoroga kama itakuwa Bado nzito ongezea maji kidogo Ili upate uji ambao sio mzito Wala mwepesi Sana
JINSI YA KUPIKA
Weka pan Yako jikoni subir ipate moto hakikisha moto sio mkali
Kama pan sio non stick ipake mafuta kidogo ikipata joto
Weka uji wako wa ngano katika pan acha Kwa dakika 1 au 2 had uone Inakuwa kavu kidogo geuza upande wa pili nao acha kidogo Kisha weka mafuta nusu kijiko Chakula upande mmojaKisha geuza upande mwingine nao hivo had uone imebadilika rangi
Toa chapat zako jikoni zitakuwa tayari
Sio mjuzi sana wa mapishi karibuni pia kuongezea maoni

Unaweza kunywa na chai ya rangi hata maziwa View attachment 2791077
Nitapika weekend ๐Ÿฅฑ
Thanks for sharing ๐Ÿ™โ˜บ๏ธ
 
Tatizo me nikizipika sijui nakosea wapi,zinakuwa rojo rojo
Uji unakuwa mwepesi Sana pia paka mafuta pan Yako na uzisubir zikauke ule upande wa kwanza ndo ugeuze
 
Acha tu atakayenioa namuonea huruma ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Kumbe bado acha nikutaftie kijana, nina kijana wangu mstaarabu mpole ,hana makuu ana kila sifa mrefu kidogo ila hana hela ebu mfikirie , katika orodha mwandike alafu unipe jibu kwa kuninong'oneza
 
Niandalie na maini rosti na maziwa freshi Sawa Aaliyah kama hutojali lakini
 
Back
Top Bottom